Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 7, 2010

TAASISI YA BYPORT YAWASAIDIA WANAFUNZI WAWILI CHUO KIKUU


Na victor Mkumbo

TAASISI ya kifedha ya Bayport jana imetangaza washindi wawili waliopata udhamini wa kusomeshwa chuo kikuu na taasisi hiyo kupitia mchakato wa kutafuta wanafunzi hao wa 'Bayport University Scholarship'.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja masoko na uhusiano wa taasisi hiyo Bw. Ngula Cheyo alisema mchakato wa kutafuta wanafunzi hao ulianza mwezi Julai mwaka huu ambapo jumla ya wahitimu wa kidato cha sita 62 waliingia katika mchakato huo ambapo sambamba na matokeo hayo wlitakiwa kuandika insha fupi kuhusu uelewa wao kuhusu taasisi za mikopo ikiwa ni pamoja na mtu anaye muhamasisha maishani.

Alisema, baada ya kuaptikana kwa wanafunzi hao kamati ya Bayport University Scholarship ikiwa chini ya mwenyekiti wake Bw. Ken Kwaku iliweza kuwachagua wanafunzi wawili ambao ni Bw.Hassan Rajab na Bi.Rodness Milton ambapo watasomeshwa na taasisi hiyo.

Bw.Ngula alisema, Bi.Rodness atapelekwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa ajili ya kusomea uhandisi ambapo alichagua nafasi hiyo baada ya kusema amehamasika kupitia Waziri wa ardhi Anna Tibaijuka kupitia insha yake huku Bw. Hassan atasoma katika chuo cha mzumbe akichukua kozi ya utunzaji wa fedha 'Bachelor in account and finance'.

Alisema, udhamini huo umegarimu kiasi cha sh. milioni 2 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka ikiwa ni pamoja na gharama za mafunzo ya ziada, malazi, lap top ikiwa ni pamoja na gharama za vifaa vya kielimu sambamba na matumizi mengine yatakayotakiwa chuoni hapo.

Alisema, kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na jamii katika nyanja mbalimbali ili kuweza kufikisha malengo ya wanajamii katika kukuza na kuendeleza uchumi wao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...