Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 11, 2012

Nicolas Mgaya wa (TUCT) kuvaa viatu vya Tido Mhando



KATIBU Mkuu wa Shiriko la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Nicolas Mgaya amejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza (MDTF), akitaka kuvaa viatu vya mtangulizi wake, Tido Mhando.
Mgaya ameingia katika kinyang'anyiro hicho akiwa ndiyo mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya Sekretarieti iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Tido, kumaliza muda wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari jijini Dares Salaam na Katibu Mwenezi wa MDTF, Ramadhan Semtawa uchaguzi huo wa kupata sekretarieti mpya utafanyika kesho kwenye Kanisa la Mtakatifu Albano, lililopo karibu na kituo cha Posta mpya.
"Chama Cha Maendeleo cha Watu wa Muheza kinapenda kiwaarifu wana Muheza wote kwamba keshokutwa siku ya Jumamosi, tarehe 12 mwezi huu kutakuwa na uchaguzi mkuu wa kuchagua sekretarieti mpya ya chama. Hivyo, wana Muheza wote mnaopenda maendeleo ya wilaya yenu  mnaombwa kufika bila kukosa. Uchaguzi utafanyika kuanzia saa 3:30  asubuhi," alisema Semtawa
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hadi jana mchana nafasi ya mwenyekiti ilikuwa ikiwaniwa na Mgaya huku ile ya Makamu ilikuwa ikiwania na Mwanaidi Ngoda, Katibu Twaha Msenga, Mweka Hazina na Semtawa akiwania tena nafasi hiyo ya uenezi.
MDTF ni chama kilichosajiliwa kwa madhumuni ya kuleta maendeleo ya Muheza ambayo huchochea pia maendeleo ya taifa kwa ujumla katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, afya, maji na kilimo. Baadhi ya miradi mikubwa ya MDTF ni visima vya maji katika sekondari za Kelenge huku pia mfuko huo ukiwa umejenga Shule ya Kidato cha Sita ya Muheza (Muheza High School).
Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho ni  Edward Mhina akifuatiwa na Hurbet Mtangi ambaye ni mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu  na anayemaliza muda waake ni Tido ambaye aliongoza Sekretarieti ambayo makamu wake alikuwa ni Merry Chipungahelo, Katibu ni Albert Semng'indu, mweka hazina Nehemia Mchechu na Katibu Mwenezi, ni Semtawa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...