Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kuunga mkono kuwepo kwa ndoa za jinsia mmoja na kuwa rais wa mwanzo kufanya hivyo.
Katika
mahojiano yake na kituo cha luninga akiwa Ikulu ya Marekani, rais Obama
ameeeleza kuwa alikuwa makini sana kuhusiana na suala hilo, kwani kwa
watu wengi neno “ndoa” linamaanisha kitu ambacho kina hisia kali za
kimila, kidini na kiimani.
Amesema sasa ni muhimu kwake “kujitokeza binafsi na kuthibitisha kwamba wapenzi wa jinsia moja waweze kufunga ndoa.”
BUSARA ZA MO BLOG:
Viongozi na watawala wa Mataifa barani Afrika ikiwemo Afrika Mashariki
na nyumbani Tanzania nini msimamo wenu kuhusiana na hilo..?? Kama
mnapinga au kukubali wadau wanaomba sababu. Nanyi wadau wetu hapo je..??
Mnalakuongeza..??
No comments:
Post a Comment