|
Burudani ya mabinti |
|
Tenga na Mgongolwa wakifurahia |
|
Tenga na Mgongolwa |
|
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kushoto, katikati mama Juliana Yassoda na kulia Robin |
|
Wadau wa soka,
Msafiri Mgoyi Mjumbe wa TFF, beki wa zamani Taifa Stars na Meneja wa
timu hiyo, Leopold Mukebezi, Fred na kocha Joseph Kanakamfumu |
|
Mwandishi wa Nipashe Somoe Ng'itu na kocha Jamhuri Kihwelo |
|
Makamu wa kwanza wa rais wa TFF, Athumani Nyamlani na Mdau Salim |
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL), jioni hii imeingia mkataba wa kuidhamini timu ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wa miaka mitano, wenye thamani
ya Sh. Bilioni 23.
Uzinduzi
huo ulifanyika katika hoteli ya Kempinski, Dar es Salaam na kuhudhuriwa
na viongozi wote wakuu wa TFF, TBL na wadau mbalimbali.
Stars,
ambayo tangu mwaka 2006, ilikuwa ikidhaminiwa na kampuni nyingine ya
Bia Tanzania, Serengeti (SBL) sasa itakuwa ikivaa jezi zenye nembo ya
bia ya Kilimanjaro, ambayo pia ni wadhamini wa Simba na Yanga.
Rais
wa TFF, Leodegar Chillah Tenga alitiliana saini mkataba huo na
Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche katika hafla iliyopambwa na
burudani nyepesi nyepesi.
Katika
hafla hiyo liyofana, utiaji saini wa mkataba huo, ulishuhudiwa na
mawakili wa pande zote mbili, TFF ikiwakilishwa na Alex Mgongolwa.
No comments:
Post a Comment