Na Elizabeth John
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT),
linasubiri barua kutoka Shirikisho la Ngumi Duniani (AIBA) kwaajili ya kujulishwa
tarehe mpya ya mashindano ya ubingwa wa Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika
huko Mauritius.
Awali
mashindano hayo yalipangwa kufanyika Septemba mosi hadi 7 nchini humo kabla
AIBA hawajahairisha kutokana na sababu ambazo zimeelezwa kwamba zipo nje ya
uwezo wao.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema timu ya
taifa inaendelea na mazoezi ya kujifua kwaajili ya mashinndano hayo katika
uwanja wa ndani wa taifa.
“Timu ipo
vizuri kwaajili ya mashindano hayo, bado inaendelea na mazoezi kama kawaida
bado hatujajua ni lini mashindano hayo yataanza tunasubiri barua kutoka AIBA
tukipata taarifa tutatangaza,” alisema.
Mashaga aliwaomba watanzania wajitokeze zaidi kusaidia timu yetu ya taifa ili uwakilishi katika mashindano ya kimatifa uwe wenye tija kwa kuzingatia kuwa watanzania wote ndio wanachohitaji na ili kitimie mabondia lazima waandaliwe vema.
No comments:
Post a Comment