Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa
Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa (kushoto) alipotembelea banda la NMB
katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini
Tanga 26-27/9/2013. Walioambatana naye ni Waziri wa Uwekezaji na
Uwezeshaji Mhe. Dr. Mary Nagu, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Mh.
Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Mkutano wa Uwekezaji Nd. Salum Shamte
pamoja na viongozi na washiriki wengine. Naibu
Waziri TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri akisaini kitabu cha wageni baada ya
kutembelea banda la NMB katika maonesho hayo. Kutoka kulia ni Meneja wa
Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo, Meneja Mawasiliano wa Benki
ya NMB Bi. Josephine Kulwa pamoja na wafanyakazi wa NMB Tawi la
Madaraka Tanga.
Mkurugenzi
Ukaguzi wa ndani wa Makampuni ya Impala Bw. Julius Makara (kushoto)
akipewa maelezo ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa
Meneja Mahusiano Mwandamizi wa Wateja Wakubwa Bw. Nsolo Mlozi baada ya
kutembelea banda la NMB Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo (kulia)akibadilishana mawazo na
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo baada ya
kutembelea banda la NMB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Pangani Farms Bw. Charles Makoi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Pride (T) Limited Bw. James Obama (kushoto) akipewa maelezo
ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa Meneja wa Kanda ya
Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo. Pembeni yake ni Meneja wa Tawi la
NMB Madaraka Tanga Bw. Juma Mpimbi, Meneja Uwekezaji wa NSSF Bw.
Abdallah Mseli na Meneja Mahusiano Wateja Wakubwa Bi. Shilla Senkoro
katika maonesho hayo. Mkuu
wa Wilaya ya Lushoto Mh. Majid Mwanga (kati) akibadilishana mawazo na
Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa, Meneja wa Kanda
ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo baada ya kutembelea banda la NMB
katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini
Tanga. Mbunge
wa Kilindi Mh. Beatrice Shelukindo akiwa na maofisa wa NMB
alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya
Kaskazini.
No comments:
Post a Comment