Mabalozi wa tamasha hilo, Vincent Kigosi 'Ray' na Elizabeth Michael 'Lulu' ndiyo watakaonogesha tamasha hilo kwa siku hizo tatu kabla ya kufungwa Alhamisi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dk Funella Mukangara.
Akizungumza na MICHARAZO mapema leo, mmoja wa waratibu wa tamasha hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano wa mtandao wa filamucentral na kampuni ya Haak Neel Production. Myovela Mfwaisa, alisema tamasha hilo litafanyikia viwanja vya Chuo cha Posta.
Mfwaisa alisema mbali na semina hiyo ya mafunzo pia leo kwenye uzinduzi kutakuwa na uonyeshwaji wa filamu nne za kibongo na utaratibu huo utafanyika siku zote tatu.
"Tamasha letu la DFF litazinduliwa rasmi Jumanne kwa semina ya mafunzo juu ya uigizaji, uandishi wa miswada, utayarishaji na uongozaji wa filamu chini wa wakufunzi toka Chuo Kikuu na jioni kutakuwa na uonyeshwaji wa filamu nne tofauti," alisema.
Mfwaisa alisema mabalozi wa tamasha hilo ni Mtayarishaji na Muongozaji Bora wa 2011-2012, Vincent Kigosi 'Ray' na Elizabeth Michael 'Lulu' ma kwamba watatumia kuonyesha kazi za kitanzania za lugha ya Kiswahili tu kwa mwaka huu .
Alisema kesho itakuwa zamu ya makampuni ya kuzalisha na kusambaza filamu nazo zitakuwa na wasaa wao wa kutangaza kazi zao kwa wadau kabla ya siku ya mwisho kutakuwa na mjadala wa mustakabali wa filamu nchini utakaohusisha taasisi kama TRA, Bodi ya Ukaguzi wa Filamu, wasambazaji wa filamu na taasisi nyingine.
No comments:
Post a Comment