4..Meneja
wa kinywaji cha Ndovu special Malt Pamerla Kikuli akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya udhamini wa bia ya ndovu
kwenye kilele cha siku ya siku ya Tembo kitaifa ambapo kilele hicho
kitafanyika katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siku ya Taifa ya Tembo, Profesa Mng’ongo akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya udhamini wa bia ya
ndovu kwenye kilele cha siku ya siku ya Tembo kitaifa ambapo kilele
hicho kitafanyika katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar Es Salaam,
kushoto ni meneja wa kinywaji cha Ndovu Special Malt Pamela Kikuli na
kulia ni Meneja Habari na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi.
Meneja
wa kinywaji cha Ndovu Special Malt Pamerla Kikuli akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya udhamini wa bia ya ndovu
kwenye kilele cha siku ya siku ya Tembo kitaifa ambapo kilele hicho
kitafanyika katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tathimini ya Rasilimali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IRA), Profesa Amos E. Majule.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Ndovu Special Malt,
imeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kusaidia usambazaji habari na
elimu juu ya uhifadhi wa tembo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Ndovu
Special Malt, Pamela Kikuli alisema, kampeni hiyo maalumu itafanyika
Siku ya Taifa ya Uhifadhi wa Tembo, inayotarajiwa kufanyika Jumapili.
“Kwa
siku wastani wa tembo 30 wanauawa na majangili, hivyo kasi ya kutisha
ya kutekekezwa kwao inayofanywa kwa wanyama hawa wapole na wakubwa,
inahitaji jitihada zetu sote,” alisema.
Pamela
alisema, wanataka kutumia mitandao ya kijamii katika kufanikisha hilo
na watatumia njia iitwayo ‘Ndovu Defender app’ katika kuhakikisha wengi
wanapata taarifa sahihi na kushiriki katika kampeni ya kuwahifadhi
wanyama hao.
Alifafanua
kuwa mpango huo wa ‘Ndovu Defenders’, utapatikana katika kurasa ya
facebook ya kinywaji cha Ndovu, ambao utakuwa ni mchezo maalumu, ambapo
kila mshiriki mpya atalazimika kuchangia Sh 1,000 ambazo zitakusanywa na
kutumika katika kampeni ya uhifadhi wa Tembo.
“Wapenzi
wa bia ya Ndovu wanaweza kutoa mchango wao katika kampeni hii kwa
kutembelea kurasa ya facebook ya Ndovu na kushiriki mchezo huo, kumbuka
kurasa yetu ina mashabiki zaidi ya 44,000 hivyo itakuwa njia rahisi
zaidi ya kuwapa ujumbe.
“Mbali
na hilo, tutatumia njia nyingine za ukusanyaji wa fedha na katika hili
bia ya Ndovu inaamini itafanikiwa kuwalinda na kuwatetea wanyama hawa,”
alisema Pamela ambao pia walikabidhi fulana na kofia zitakazotumika kwa
washiriki siku hiyo.
Naye
Meneja Habari na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha
Mushi alisema, mkakati huu wa kuelimisha jamii juu ya uhifadhi wa Tembo
ambapo bia ya Ndovu Special Malt inashirikiana na wadau wengine
kufanikisha mpango huo.
Akiongelea
umuhimu wa maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Taifa ya Tembo, Mwenyekiti
wa Kamati ya Siku ya Taifa ya Tembo, Profesa Mng’ongo alisema, kwa sasa
Tembo wanateketea mno, hivyo siku hiyo ni muhimu zaidi.
“Siku
hiyo ni muhimu zaidi kwetu, kwani mnyama huyo kwa sasa anawindwa kila
siku, hivyo ni muhimu kutambulishana taratibu na mikakati ya jinsi ya
kulinda idadi ya tembo waliobaki hapa nchini kwa manufaa ya kizazi cha
sasa na kijacho,” alisema.
Naye
Mkurugenzi wa Tathimini ya Rasilimali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(IRA), Profesa Amos E. Majule, alisema, kwa sasa tembo wanateketea mno,
hivyo siku hiyo ni muhimu zaidi kwa Watanzania kuungana katika hili.
Siku
hiyo inatarajiwa kutanguliwa na maandamano yanayotarajiwa kuanza Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuishia katika Ukumbi wa Mlimani City,
ambapo wadau wa uhifadhi watatoa hotuba na kutafanyika maonyesho ya
kuifahamisha jamii umuhimu wa uhifadhi wa tembo walio hatarini kutoweka.
UDSM ndio walioandaa siku hiyo kwa kushirikiana na kituo chake cha IRA, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii, World
Wide Fund for Nature (WWF), Wildlife Conservation Society (WCS), Tume
ya Sayansi na teknolojia Tanzania (COSTECH) pamoja na wadau wengine.
Kinywaji cha Ndovu Special Malt kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment