NA MWANDISHI WETU
WAREMBO wanaowania taji la Miss Tanzania wametakiwa kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa
Kiwanda cha Tanzania Distilleries (KONYAGI) Bw. David Mgwassa wakati
akiongea na Warembo 30 wanaowani taji la Miss Tanzania walipotembelea
kiwanda hicho jijini Dar es salaam.
"Nyinyi
ni mabalozi wazuri wa kutangaza bidhaa za humu ndani hivyo nawaomba
sana mzipende na kuthamini sana bidhaa zote zinazozalishwa na viwanda
vya ndani" alisema Bw. Mgwassa.
Amesema
kuwa TDL kupitia kinywaji cha Zanzi imeamua kudhamini shindano la Miss
Tanzania kwa kiasi cha Milioni 40 ikiwa na lengo la kutangaza kinywaji
hicho na pia kuboresha shindano hilo.
Kwa
mujibu wa Bw. Mgwassa shindano la Miss Tanzania ni kielelezo muhimu kwa
taifa hili na kuwataka warembo hao kutangaza milima kilimanjaro na pia
kuitangaza Zanzi kuwa ni bidhaa bora kwa Watanzania kwa lengo la kuinua
uchumi wa nchi.
"Nyinyi
warembo naombeni sana Zanzi iwe kwenye mawazo yenu kila siku na
muitangaze Zanzi baada ya mlima kilimanjaro kwa kufanya hivyo basi
uchumi wa nchiu pia utakua mzuri zaidi." alisema
Kwa
upande wake meneja masoko wa TDL, Bw. Vimal Vaghmaria aliwataka warembo
hao kuwa na nidhamu kubwa wanapokuwa kambini kwa lengo la kupata mrembo
mwenye viwango vya juu na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
kimataifa.
"Sisi
kama TDL kupitia kinywaji cha Zanzi tumemua kudhamini shindano hili la
Miss Tanzania tukiamini kuwa nyinyi ni mabalozi wazuri wa kuitangaza
kinywaji hichi na kuiletea sifa Tanzania" alisema Bw. Vaghmaria.
Katika
ziara hiyo warembo walipata nafasi ya kujione shughuli mbalimbali za
kiwanda hicho kuanzia mwanzo wa vinywaji vinapozalishwa hadi kwenye
sehemu ya mwisho ya upakiaji.
No comments:
Post a Comment