BAADA ya kumchakaza Canelo Alvarez, bondia Floyd
Mayweather ‘Cash Money’ anamtaka bondia wa England, Amir Khan katika mpambano
unaofuata.
Kituo kinachoonyesha mapambano ya ngumi ya
Mayweather cha Showtime Sports kimetoa taarifa kuwa kuna uwezekano wa bondia
huyo kupambana na Khan ambaye anayatajia kutetea taji lake la IBF uzito wa welter
na Devon Alexander mwezi Desemba mwaka huu jijini New York.
Mapambano mawili kati ya sita ya Mayweather yataonyeshwa
moja kwa moja kupitia kituo hicho na Mkurugenzi wa Showtime Sports, Stephen
Espinoza alisema kuwa wanapenda kuona mpambano huo unafanyika.
Mkurugenzi huyo amepoendekeza mpambano huo unaweza
kufanyika Uingereza. "Amir Khan ni mpinzani mzuri wa Floyd Mayweather, kwa
sababu ana kasi ulingoni," alisema Espinoza.
"Mpambano huo wa kuvutia unaweza kufanyika
Uingereza au New York. Floyd amezungumzia uwezekano wa kufanyika kwa mpambano
huo sehemu moja kati ya hizo mbili.
Kama Khan akikubali kupambana na Mayweather, analipwa
fedha nyingi sana ambazo anaweza kuwa hajawahi kupata katika maisha yake ya
ngumi.
Alvarez alipata pauni 7.9 milioni poamoja na
kupoteza mpambano huo. Espinoza alisema kwamba Khan anaweza kuwaongezea soko
kubwa katika mpambano huo kuliko ilivyokuwa kwa Alvarez.
No comments:
Post a Comment