Mrembo
Prsica Clement, kutoka Kitongoji cha Sinza (katikati) akipunga mkono
kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Talent
kwa mwaka 2013, na kufanikiwa kupata tiketi ya kuingia hatua ya 15 bora
ya shindano la Redd's miss Tz mwaka huu.
Washiriki
wa shindano la kumtafuta mshiriki wa kuingia katika hatua ya 15 bora ya
Shindano la Redd's Miss Tanzania kwenye shindano la Redd's miss tz
Talent 2013 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi
wa hatua ya tano bora.
***********************************************
Na Mwandishi Wetu
WAKATI
homa ya shindano la Redd’s Miss Tanzania ikiwa inapanda kwa washiriki
wote, mrembo Prsica Clement juzi usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s
Miss Tanzania Talent lililofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo
Kunduchi, Dar es Salaam.
Kutokana
na ushindi huo, Prisca ambaye anatokea Sinza akiwakilisha Kanda ya
Kinondoni, amefanikiwa kuingia katika hatua ya 15 Bora ya Redd’s Miss
Tanzania.
Majaji
wa shindano hilo walilazimika kumpa ushindi Prsica kutokana na uhodari
wake wa kucheza na moto, hivyo kuwashinda washiriki wote 30 wa shindano
hilo.
Watazamaji wengi waliofurika katika ukumbi wa hoteli hiyo, walikubaliana na uamuzi wa majaji wa kumpa ushindi huo.
Shindano
la Redd’s Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki katika
Ukumbi wa Mlimani City, uliopo Mwenge, Dar es Salaam ambapo mshindi
ataondoka na gari dogo lenye thamani ya Sh milioni 15 na kitita taslimu
cha fedha cha Sh milioni 8.
Mbali
na mshindi kutwaa zawadi hizo, mshindi wa pili atapata Sh milioni 6.2,
mshindi wa tatu Sh milioni , mshindi wa nne Sh milioni 3, mshindi wa
tano Sh milioni 2, mshindi wa sita hadi 15 atapata Sh milioni 1.2 na
waliobaki watapata Sh 700,000 kila mmoja.
Akizungumzia
ushindi huo, Prsica alisema hiyo ni dalili njema kwake ya kutwaa taji
hilo na ana uhakika mkubwa atafanikiwa kuwa mshindi.
Naye
Meneja wa Redd’s Original, Victoria Kimaro alisema, shindano la mwaka
huu limekuwa na msisimko mkubwa zaidi kutokana na washiriki wote kuwa na
sifa zinazolingana.
“Mwaka
huu Redd’s Miss Tanzania imepata washiriki bomba zaidi na naamini
litakuwa na ushindani mkubwa na wa aina yake,” alisema Victoria.
Taji
la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred
aliyelitwaa taji hilo mwaka jana na kukabidhiwa gari aina ya Noah pamoja
na kitita cha Sh milioni 8.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.
No comments:
Post a Comment