Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiushauri Uongozi wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa na kara kana ya kisasa ya vyombo vya
moto wakati alipoitembelea kara kana ya wizara hiyo iliyopo Maruhubi. Kulia kwa Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mohd Said Dimwa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua hatua
zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar ya
kukifufua upya kituo cha upandishiaji Ng’ombe kiliopo eneo la Maruhubi
. Kushoto kwa Balozi Seif ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi hiyo Dr. Kassim Gharib . Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
********************************
Wizara
ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar iko katika harakati za kukifufua upya
Kituo cha kupandishia Ngombe kilichopo katika eneo la Maruhubi nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar ili kirejee katika utaratibu wake wa kutoa
huduma bora kwa wafugaji wa Ngo’mbe wa kisasa hapa Nchini.
Kituo
hichoanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwanzoni mwa miaka
ya 70 na kusitisha huduma zake kutokana na mabadiliko ya sera ya
ufugaji kwa kuachiliwa suala hilo kuendeshwa na wananchi moja kwa moja.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dr. Kassim Gharib alieleza
hayo wakati wa ziara fupi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi aliyefika katika eneo hilo kukagua juhudi zinazochukuliwa
na Wizara hiyo katika kukifufua tena kituo hicho.
Dr.
Kassim alimueleza Balozi Seif kwamba Wizara hiyo imeanza na hatua ya
kuzunguusha ukuta eneo hilo ili kuzuia uvamizi wa ujenzi holela wa
nyumba pamoja na uchimbwaji ovyo wa mchanga uliokuwa ukitishia uchafuzi
wa mazingira.
Alisema
hatua hiyo itakapokamilika itatoa fursa kwa wafanyakazi wa Mifugo
kuendelea na hatua ya pili ya upandaji majani kwa ajili ya malisho ya
madume ya ng’ombe watakaotumiwa kutoa mbegu na kuendelea kusambazwa kwa
wafugaji kwenye maeneo mbali mbali nchini.
Dr.
Kassim alifahamisha kwamba licha ya matatizo na changamoto mbali mbali
zilizokuwa zikikikabili kituo hicho lakini bado kinaendelea kutoa
huduma za upandishiaji ng’ombe kikiwa na Madume Sita bora ya kisasa
hivi sasa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif pia alipata fursa ya kukagua
kara kana inayohudumia matengenezo ya dharura ya vyombo vya moto vya
Wizara hiyo ya Mifugo na Uvuvi iliyopo jirani na kituo hicho.
No comments:
Post a Comment