
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata utepe
kuzindua rasmi Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara
maarufu nchini, Said Salim Bakhresa katika eneo la Uwanja wa Chamazi,
Mbagala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa Makampuni
ya SSB, Said Salim Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo
Julai 4, 2014, ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana na wengineo.




No comments:
Post a Comment