Masumbwi ni miongoni mwa
michezo nchini Tanzania iliyowahi kuiletea nchi hii medali nyingi kutokana na
umahiri wa watupa makonde kujituma vilivyo wawapo ulingoni katika mapambano yao.
Ninapozugumza hivi
ninawakumbuka baadhi ya makocha na waliopo kwenye benchi kwenye mchezo wa soka
wakati mwingine hutaka kurusha makonde pindi waonapo hali ni ngumu kwa timu
zao.
Unamkumbuka kocha Jose Mourinho?
kama sio sheria za FIFA kuwa kali angemtwanga kocha wa zamani wa Barcelona, marehemu
Tito Vilanova aliyefariki mwaka huu kwa matatizo ya kansa akitoka kuachiwa
mikoba na kocha wa sasa wa Bayern Munich, Pep Guardiola.
Mwingine ni German Burgos,
kocha msaidizi wa Atletico Madrid akiwa na mtata mwenzake mwenye wenge la
hatari, Diego Simeoni wote wakiwa waargentina waliotoka mbali lakini kwenye
suala la kurusha ngumu hawajambo.
Unaweza kusema waache
kufundisha soka waje, kipande hiki cha urushaji wa makonde, ha ha haaaa!
Unacheka?
Hapa nchini tuna wanamasumbwi
wengi ambao wamekuwa wakijitahidi kufanya mazoezi lakini hatma yao huwa ni kazi
bure wafikapo katika medani ya kimataifa kutokana na mipango mibovu ya kuukuza
mchezo huu.
Wapo mabondia wakali nchini
wakitiwa moyo kama ilivyo katika soka wanaweza kuitangaza Tanzania kimataifa
kwani hakuna kinachoshindikana.
Hata hivyo kuna madaraja ambayo
mwanamasumbwi ni lazima apambane ili aweze kusonga hadi kujulikana kimataifa yakiwemo
Superfeatherweight, Lightweight, Junior welterweight, welterweight, na Super
welterweight.
Sijui kama watoto wetu wanajua
haya!
Nchini Marekani miaka ya nyuma
kabla ya mwaka 1950 kulitokea kizazi cha warusha mawe wa ukweli Willie Pep,
Chalky Wright miaka ya 1944 na rekodi zinaonyesha mchezo huu ndio ulikuwa wa
kwanza kurushwa moja kwa moja (live) katika luninga.
Walikuwepo George Foreman, Joe
Frazier, na Muhammad Ali waliofanya vizuri katika medani hii na kulitangaza
taifa la Marekani baada hapo kikaja kizazi cha kina Mike Tyson, Evander
Holyfield na sasa ni kina Floyd Mayweather.
Kimataifa zaidi wengineo ni
Amir Khan, Manny Pacquiao, Marcos Maidana, Rocky Marciano na Oscar de la Hoya.
Leo, tutamwangazia bondia
Alibaba Ramadhani wa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro anayetarajiwa kutifuana na
bondia Thomas Mashali wa Dar es Salaam hapo Jumapili Oktoba 5 mwaka huu katika
pambano litakalofanyika Mkwakwani Mkoani Tanga.
HISTORIA YA ALIBABA
RAMADHANI
Jina kamili anaitwa Alibaba
Ramadhani (37), alizaliwa katika Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi, mkoa
Kilimanjaro t
arehe 23 Machi 1977.
Alianza elimu ya msingi mwaka
1984 na kuhitimu mwaka 1990 katika shule ya msingi Korongoni iliyopo Manispaa
ya Moshi.
Mwaka 1991 aliingia kidato cha
kwanza katika Shule ya Sekondari ya Mlite iliyopo wilayani Rombo mkoni humu.
Hata hivyo hakufanikiwa
kuhitimu elimu ya sekondari kwani mwaka 1992 alifukuzwa shuleni hapo kutokana
na utovu wa nidhamu.
Baada ya hapo ajitupa katika
shule ya ufundi na udereva mjini Moshi akisomea masuala ya ufundi makenika
katika gereji moja ambako alifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika fani hiyo.
Wakati akiendelea na mafunzo ya
ufundi na udereva, Alibaba alijitumbukiza katika michezo mbalimbali ikiwemo
utunishaji wa misuli kwa wanaume ambapo mwaka 1998 alishiriki shindano la
kumtafuta Mr. Kilimanjaro na kumaliza nafasi ya 5.
Akiwa katika michezo mbalimbali
ikiwemo kurusha tufe, mpira wa kikapu mwaka 1999 alikutana na Mwalimu Yasint
ambaye alimshauri atinge CCP kwa ajili ya masumbwi.
Ndipo Oktoba 1999 alipoanza
mazoezi makali, ilipofika Desemba 1999 alifuzu kushiriki michuano ya masumbwi kwa
timu za majeshi yaliyofanyika CCP mjini Moshi na kuishia Nusu fainali.
Mpambano anaoukumbuka ni ule
aliomchana sehemu ya jicho bondia Stanley Ernest katika raundi ya nne, hivyo
kushinda kwa TKO hii ilikuwa mwaka 2000 na kutwaa mkanda wa mkoa.
Pia amewahi kupambana na Joshua
Onyango mzaliwa wa Kenya anayeishi Marekani hii ilikuwa mwaka 2008, pambano hilo
la kirafiki lilivunjika katika raundi ya tano.
Mwaka 2014 amepambana na Erick
Mwenda katika ubingwa wa UBO-Africa raundi 10 na kumtwanga kwa pointi katika
ukumbi wa YMCA mjini Moshi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Alibaba amepambana mapambano 22
akitoka sare pambano moja tu mengine akifanya vizuri.
BONDIA WA KIMATAIFA
KIVUTIO
Akizungumza Alibaba alisema
bondia Floyd Mayweather (37) wa nchini Marekani ndiye anayemvutia zaidi na
hujisikia vizuri akimwona akishinda mapambano yake, hasa ikizingatiwa kwamba
majuma machache yaliyopita amemtusua Muargentina Marcos Maidana.
KUELEKEA PAMBANO DHIDI
YA THOMAS MASHALI
Wakali hawa watakuwa wakiwania
mkanda wa kimataifa wa UBO uzito wa kilogramu 72 “lightmiddleweight”.
Viunga vya mji wa Tanga
vitarindima vigelegele na vifijo pale mabondia Ali Baba na Thomas Mashali watakapopanda
ulingoni.
WITO KWA MABONDIA
MAPROMOTA
Alibaba aliwataka mabondia
wenzake kufanya mazoezi na kuacha
starehe na kujikita kufanya mazoezi kwa bidii zote ili kuurudisha mchezo huu
kwenye zama zake.
Pia aliongeza kusema
wanamasumbwi za zamani na wa kizazi cha sasa kuna utofauti mkubwa sana ikiwemo
kupunguzwa kwa raundi kutoka 15 hadi kuwa chini ya 12 kutokana na wengi wao
kukosa chakula cha kutosha na kujikita katika starehe badala ya mazoezi.
Hata hivyo Alibaba anayenolewa
na Kocha Pascal Bruno kutoka Nairobi aliwataka mapromota wa mchezo kuacha tamaa
ya fedha na badala yake wajikite kuwasaidia mabondia wao hali ambayo itaongeza
hamasa kwa chipukizi.
WITO KWA SERIKALI
Aidha bondia huyo aliitaka
serikali kuangazia mikoani na sio Dar es Salaam pekee kwani mikoani kuna wengi
wenye uwezo wa kutosha hivyo mazingira yakiboreshwa yatasaidia kuinua mchezo huo
kimataifa na kuachana na tabia ya kuwa wasindikizaji michuano mbalimbali.
Alibaba alihitimisha kwa
kuwataka wakazi na wadau wa mkoa wa Kilimanjaro kuachana na dhana ya michezo
hailipi na badala yake wawekeze katika m
chezo wa masumbwi badala ya kujikita katika
masuala yasiyo ya kimichezo ili kuendeleza masumbwi.