Rais wa Kamisheni
ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akiwakumbusha baadhi
ya sheria zitakazo tumika katika mchezo wa ngumi utakaofanyika kesho
katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Dar es salaam
NA Mwandishi Wetu
MABONDIA Meshack Mwankemwa na Hamisi
Mwakinyo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 66
unaotambuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchi mkanda uho uliokuwa
umeachwa wazi na bondia Selemani Zogo kwa kuto utetea kwa wakati sasa
utapiganiwa na mabondia hawo kesho
akizungumza wakati wa upimaji wa uzito
promota wa mpambano uho Shomari Kimbau amesema mkanda uho utapiganiwa
na mabondia hawo ili apatikane bingwa mpya wa uzito wa kg 66
mpambano uho utasimamiwa na kamisheni
ya ngumi za kulipwa nchini chini ya rais wake Chauremba Palasa aliongeza
kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo pia kutakuwa na ngumi za
utangulizi za mabondia mbalimbali
Said Mayanga atamenyana na Gido Selemani wakati Mohamed Amir atapambana na Hemed Hemed
na mpambano mwingine wa kusisimua
utakuwa ni wa akina mama ambapo bondia mnaschachali Asha Nzowa 'Asha
Ngedere' atapambana na Joyce Awino ambambao ambao unasubiliwa kwa hamu
kubwa na mashabiki wanawake wa mchezo wa masumbwi
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo
vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia
watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na
kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
|
No comments:
Post a Comment