Mdau wa mchezo wa ngumi nchini
Chaurembo Palasa akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau wa mchezo
wa masumbwi nchini kushoto ni Chuku Dusso Ally Bakari na Yassin Abdallah Picha na SUPER BOXING NEWS
BAADHI YA WADAU WALIOJITOKEZA KATIKA
MKUTANDO WA KUNUSURU MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA MWENENDO WAKE MZIMA
KUTOKA KULIA WALIO SIMAMA NI sHOMARI kIMBAU,SHABANI KAONEKA,CHUKU DUSO Mkali Kaizum CHAUREMBO PALAS NA WALIOKAA KUTOKA KUSHOTO NI FIDEL HYNES ALLY BAKARI NA RATIBU WA MKUTANO UHO SADICK KINYOGOLI
Mdau
wa mchezo wa masumbwi nchini Yasin Abdallah katikati akiongea katika
mkutano wa wadau wa mchezo wa masumbwi nchini kushoto ni Chuku Duso na
kulia ni Chaulembo Palasa Picha na SUPER BOXING NEWS
Katika miaka ya hivi
karibuni takwimu zinaonesha kuwa masumbwi ndio mchezo wenye kuingiza
pesa nyingi kuliko mchezo wowote duniani, ambapo kwa hivi sasa kinara wa
utajiri kupitia mchezo huo ni bondia Floyd Mayweather.
Mkali huyo
anafuatiwa na Manny Paquaio ambao wote ni mabondia wanaoshikilia nafasi
mbili za juu za utajiri michezoni, huku michezo mingine ikifuata.
lakini kwa hapa kwetu Tanzania kumekuwa na kilio cha kawaida sana kwa wapenzi na washabiki
wa mchezo wa ngumi kusikika wakilia kuomba usimamizi wa serikali katika
mchezo wa ngumi za kulipwa.
Licha ya jitihada za wadau kupambana na kuhakikisha ngumi
zinafikia mahali panapo vutia lakini bado kumekuwa na matatizo kila kukicha.
Tatizo kubwa ni watu kujiendesha bila ya kuwa na usimamizi wenye mamlaka kutoka chumbo cha juu kinachosimamia michezo nchini.
Baada ya kutokea hayo kwa takribani miaka 20, Serikali ya
Rais DR.John Magufuli imekuja na mkakati wa kuwaundia chombo cha
kutengeneza sera na kanuni za kuusimamia mchezo huo wa ngumi za kulipwa nchini.
Kamati hiyo inayoundwa na watu Sita iko chini ya Mwenyekiti
Habibu Kinyogoli Katibu mkuu kwa sasa ni
Chaulembo Palasa baada ya Emanuel Mlundwa kusimamishwa kufanya kazi za masumbwi nje na ndani ya nchi.
Kamati ilipata baraka za Katibu wa baraza kwenda kuandaa miongozo na kanuni za kusimamia ngumi za kulipwa nchi nzima.
Kinachostaajabisha watu hawa baada ya kupewa uhuru wa
kujichaguwa wakatumia uhuru huo kujipanga wao wenyewe huku wakijuwa kati
yao hakuna maelewano.
Mlundwa ambae alikuwa katibu wa kamati hiyo hana maelewano mazuri
na katibu wa sasa Chaulembo Palasa mpaka kufikia kupelekana
mahakamani.
Historia inaonyesha kuwa Mlundwa ndie aliyempa Chaulembo
pesa na wakiri wa kusimamia kesi iliyokuwa imefunguliwa na Onesmo Ngowi
baada ya Chaulembo kuwa akimfanyia visa katika shughuli zake.
Dhumuni la kumpa pesa hiyo ilikuwa ni kumuondoa Ngowi
kwenye Uwenyekiti kwa sababu kulikuwa na mwingiliano wa kimaslai kati
yao.Hivyo akichukuwa Chaulembo, Mlundwa atakuwa huru kufanya biashara
zake.
Cha kushangaza baada ya Chaulembo kushinda kesi uadui ukahama kutoka kwa Ngowi ukaja kwa mtu aliyemuweka yeye mwenyewe.
Kutokana na historia hiyo mvutano kati ya Mmiliki wa
kampuni ya Puglistic Syndicate of Tanzania (PST) na Tanzania
Professional Boxing Commition (TPBC), umeendelea kuwa kikwazo katika
mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
Baada ya mpasuko huo Serikali kwa kupitia Waziri wa Michezo
Nape Nauye aliamuwa kuwaita wahusika wote wa Makampuni na Chama ili
kutaka kuweka mambo sawa.
Chakushangaza ndani ya kamati hiyo iliyopewa kazi kwa miezi
kadhaa tayali kunampasuko,mpasuko huo unakuja baada miongoni mwao
wanaounda hiyo kamati wanamgongano wa kimaslai.
Juzi aliyekua katibu wa kamati hiyo Emanuel Mlundwa alijikuta kwenye
kashfa ya kuwatumia watoto wadogo waliochini ya miaka 18, katika mchezo
kati ya Thomas Mashali na Sajjad mehrab.
Nikweli watoto walitumika kinyume na taratibu maana hakuna
sheria inayoruhusu watoto kuwa eneo la starehe mpaka usiku wa Saba na
pia kuwatumia katika ngumi za kulipwa.
Wakati huo tayali alikwisha andikwa na Baraza la michezo
yenye kumbukumbu namba- KVJM/MIC/SR/1/28/87 iliyokuwa ikimtaka ajieleza
kwanini asichukuliwe hatu kwa kuwachezesha utangulizi watoto Mawazo
Leonard na Mbaraka Ally, katika mechi ya Monica Mwakasanga Tanzania na
Marischa Sijauw wa Uholanzi.
Hivyo kitendo cha kuwatumia watoto katika michezo Mlundwa amezoea ndio maana hakuwa na hofu kuwapandisha tena kwenye ulingo.
Kitendo cha kuwapandisha watoto kwenye ulingo
kilitafasiliwa kuwa ni ukiukwaji wa haki za watoto ambazo ni kinyume cha
mikataba ya umoja wa mataifa inayokataza ajira kwa watoto.
Chakushangaza Mlundwa anasema Mataifa makubwa yanawatumia watoto katika ngumi za kulipwa ikitolea mfano Cuba na Marekani.
Tukio hilo lilifanya vyombo vya habari kumtaka Yasin
Abdallah (Ustadhi) mmiliki wa Kampuni ya Tanzania Boxing Proffesional
Organisation (TPBO) kutolea ufafanuzi suala la kutumia watoto katika
ngumi za kulipwa.
Ustadhi alitolea ufafanuzi kuhusiana na hilo kuwa nimakosa
kuwatumia watoto kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa na ni hatalishi kwa
afya zao na malezi kwa ujumla.
Lakini Mlundwa alikuja juu na kumtolea lugha chafu Yasin
Abdallah (Ustadhi) kitu kilichoibuwa mtikisiko kati ya wadau wa ngumi na
kupelekea wadau hao kukutana wiki moja baadae.
Mlundwa alisema sio ajabu kuwatumia watoto kwenye ngumi za kulipwa kwani mataifa makubwa yanawatumia katika huu mchezo.
Swali la kujiuliza kama Mlundwa anasema Mataifa makubwa
yanawatumia watoto katika ngumi za kulipwa,sisi tanzania tunafuata
Sheria gani ya kimataifa?
Ukichunguza kwa undani utagunduwa kuwa Mlundwa ni wakala wa
kutekeleza Sheria, Kanuni na Sera za mataifa ya ulaya, ambazo hapa
kwetu bado hatujaanza kuzitumia na pengine tusizitumie.
Mlundwa alienda mbali zaidi kwa kusema kama yeye amewatumia
watoto na kila mtu ameona anaomba atua zichukuliwe dhidi yake lakini
hao wanaomshambulia kwa kufanya vikao anaomba wasitumie kisingizio cha
watoto kumziba mdomo asiseme siri zao.
Alisema wanaomchafuwa ni wale wote ambao wamekuwa na
utaratibu wa kupeleka mabondia nje huku wakiwa sio mambondia na kuishia
huko huko.
Mludwa alisema miezi michache iliyopita Chaulembo Palasa
alitoa vibali kwa bondia watatu, na mtu mmoja ambae si bondia ambae
alitambulishwa kwa hao mabondia kuwa ni Meneja wao.
Mbali na ayo Mlundwa alisema kama wao ni wasafi kwanini
hawatoi maelezo ya kwanini Shomari Kimbau alirudia uwanja wa Ndege
nchini Urusi, nini kilimfanya arudi ikiwa kila kitu kiliratibiwa huku
Dar es salaam
Mwandishi wa makala hii hakuishia hapo aliamuwa kumtafuta
Rais wa TPBC Chaulembo ili aseme huyo mtu mmoja aliyebaki Russia ni nani
na kwanini Meshack Mwankemwa waliishia uwanja wa ndege Urusi
alipopatikana alisema hajui hizo taarifa na anamshangaa Mlundwa kusema
kunamtu kabaki Rusia.
Lakini pia suala la Kimbau na Mwankemwa kurudia uwanja wa
Ndege lilitokana na Shomari kutokuwa na mawasiliano mazuri na promota wa
mechi ya mwankemwa.
Embu tujiulize mtu anawezaje kutoka Tanzania mpaka Urusi
bila kuwa na mawasiliano na mwenyeji wake, je hizo nyaraka walizopeleka
ubalozini ili wapewe kibali cha kukaa Urusi zilikuwa hazionyeshi
tarehe,mwenyeji wao na dhumuni la wao kwenda kule?
Mbali na hayo kawaida ya ngumi za kulipwa ukishakuwa na
mchezo lazima utaonekana kwenye ubao wa matangazo wa kimataifa (Box rec)
na ukweli mchezo wa Mwankemwa ulikuwa unasoka tarehe usika.je nini kilitokea akaishia uwanja wa ndege.
Ukiangalia kwa kina utaona kunauondokaji wa kiholela wa
watanzania kwenda nje, je safari za mabondia hawa Ofisi za uhamiaji
wanapata taarifa au nao huwa wanaacha watu wajiondokee hasa mabondia.
Kutokana na mlolongo huu uliojaa ubabaishaji mwandishi wa
makala akapiga hodi Ofisini kwa Katibu wa baraza la MichezoAbdallah
Kiganja.
Mwandishi: Ndugu Kiganja unafahamu nini kuhusiana na huu mvutano wa Kamati ya kuunda katiba ya kusimamia ngumi za kulipwa.
Kiganja: Sijapata taarifa yoyote inayohusu hii kamati iliyoundwa.
Mwandishi: Hunataarifa za Emanueli Mlundwa kutumia watoto katika mchezo wa mashali Sajjad mehrab?
Kiganja:Sina taarifa kuhusiana na ule mchezo maana sikuwepo Ofini nilikuwa safarini.
Mwandishi: Sheria za nchi kwenye masuala ya michezo inawataka watoto washiriki michezo mpaka saa ngapi?
Kiganja: Watoto mwisho saa 12,jioni,wanapaswa kuwa
wamemaliza michezo yao.ikitokea wameshirikisha watoto katika michezo yao
basi wazingatie taratibu zinataka nini.
Ikitokea ikadhibitika waliwatumia watoto katika mchezo ule
Baraza litachukuwa hatua kwa wale wote waliohusika katika kuwatumia hao
watoto.
Kutokana na maelezo ya kiganja anapenda michezo ishirikishe
watoto lakini izingatie kanuni.Je kwa matumizi yale ya mtoto wa kike
(Red Card) je ni utaratibu upi mpaka usiku wa saa Saba?
Ifikie mahali sasa Serikali ionyeshe makucha yake kwa watu wa mchezo wa ngumi maana wamejisahau wanajiendesha wanavyojisia.
Sio ajabu kusikia Gloves zikatumiwa na wachezaji wote,sio
ajabu kuona watazamaji wakilaani maamuzi mabaya yanayotolewa na waamuzi
wakati wa mchezo,sio ajabu kuona bondia anashuka ulingoni hajavishwa
mkanda kisha kujibiwa "Mkanda hata mbwa anao".
Kama serikali imeshindwa kudhibiti huu mchezo bora iufute
ili kutoa nafasi ya kujipanga upya kuliko kuuwacha ubaki kuwa wa watu
binafsi.
Huwezi kusema eti umeunda kamati ya kuandaa katiba huku
walioteuliwa ndio wamiliki wa haya makapuni yaliyotufikisha hapa mbali
ya kuwa wao wenyewe hawaelewani kila siku malumbano.
Tusipokuwa makini kwenye hili watamponza Waziri wa Michezo
atumbuliwe kwa sababu ya njaa na uhasama wa kati ya wamiliki wa haya
makampuni na chama.
hata
hivyo mimi binafsi napendekeza kuwe na chombo kitakacho ratibu mchezo
wa ngumi za kulipwa kwapamoja ili kusiwe na mgongano na migogolo kwa
watendaji wake ila chombo kitoe ruhusa kwa mawakala wa mchezo wa ngumi
kutafuta michezo mingi zaidi nje a nchi ili mabondia wapate kunufaika na
mchezo wauchezao wakati wangali na nguvu zao
ni siwe mwingi wa maneno kwa leo naomba kuishia hapo ili utaratibu na maamuzi ya busara ufuate mkondo wa uongozi wa pamoja