Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 1, 2016

MNUFAIKA WA AIRTEL FURSA AMZAWADIA MKURUGENZI MKUU WA AIRTEL


Kijana Theresia Maliatabu  mmoja kati ya kijana anaejihusisha na ubunifu wa sanaa za uchoraji aliyenufaika na  mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” akiongea na wafanyakazi wa Airtel (hawapo pichani ) alipofika kwenye ofisi za Airtel makao makuu kukabidhi picha yake aliyoichora baada ya  airtel Fursa kumpatia Kijana huyo vifaa vya kidigital katika semina iliyofanyika  miezi miwili iliyopita na  kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo kwa ajili ya kuboresha kazi zao.
Kijana mjasiriamali Theresia Maliatabu (Kulia) akimkabidhi picha aliyoichora kwa ubunifu wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso (Kushoto) kama shukrani yake kwa Airtel  baada ya kuwezeshwa kupitia mpango wa Airtel FURSA "Tunakuwezesha" kwa kupatiwa vifaa vya kuboresha biashara yake. Katikati ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi. Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya mkutano wa mwezi wa wafanyakazi Airtel uliyofanyika katika ofisi za Airtel Makao makuu Morocco jijini Dar es salaam.
XXXXXXXXXXXXXXX

DAR ES SALAAM

Kupitia mradi wa Airtel fursa ambao umekuwa ukitoa misaada mbalimbali kwa vijana nchini kwa kuwawezesha kufanikisha ndoto zao, ambapo mmoja kati ya kijana anaejihusisha na ubunifu wa sanaa za uchoraji aliyenufaika na mradi huo, Bi, Theresia Maliatabu  leo Juni 01. 2016, amemtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bw. Sunil Colaso na kumzawadia picha yake aliyoichora mara tu Airtel Fursa kumpatia Kijana huyo vifaa vya kidigital katika semina iliyofanyika  miezi miwili iliyopita na  kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo kwaajili ya kuboresha ubunifu wao.
Akikabidhi zawadi hiyo Theresia alisema” vifaa hivyo vinanisaidia kubuni baadhi ya michoro ambayo ni ya kisasa zaidi, lakini hasa inanisaidia mazoezi katika kuchora na vile vile inanisaida kama sehemu ya kutangaza biashara yangu kupitia social media”.
“Napenda kuwaambia vijana wenzangu kwamba wajiamini na vipaji walivyokuwa nazo wasikate tamaa kwani kila kitu kinawezekana na wasiache kuchangamkia fursa kama hizi zinapojitokeza, aliongeza Theresia
Mpaka sasa Airtel imefanya semina nyingi sana za mafunzo ya biashara ya ujasiriamli hapa nchini katika mikoa mbali mbali na kuweza kufikia vijana wapatao 4000. Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA utaendelea kutoa warsha hizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha inafikia vijana wengi zaidi. 

Vijana wanahamasishwa wanaposikia nafasi kama hii popote walipo , kuchangamkia kwa kuhudhuria kwani  elimu inayotolewa  ni bure kabisa bila gharama yoyote.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...