Ni asubuhi tulivu katika fukwe za bahari
ya hindi kusini mwa Tanzania ambapo vijana wengi wamejitokeza kufanya
usaili wa mashindano ya Maisha Plus East Africa 2016. Wapo wanaoonekana
kujiamini na wengine wamejawa uoga. "Ni siku niliyoisubiri kwa hamu
sana" anasema Faustine Komba miongoni mwa washiriki kutoka Mtwara.
Safari ya msimu wa tano wa mashindano ya
Maisha Plus imeanza rasmi kwa kuanza na usaili uliofanyika katika hotel
ya NAF Beach iliyoko Mtwara. Washiriki kutoka mikoa ya jirani nao pia
walijitokeza. "Maisha Plus kwangu ni ndoto ya muda mrefu sana,
niliposikia mnakuja Mtwara nikasema piga ua lazima nishiriki" Anasema
Ismail Likando aliyesafiri kutoka Lindi.
Maswali mengi yalilenga kupima uelewa wa
vijana kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo mtazamo wao juu ya
mwenendo wa kiuchumi. Mengine yalilenga kuwachanganya tu.
No comments:
Post a Comment