Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, September 30, 2016

MABONDIA KUPIMA UZITO KESHO JUMAMOSI KWA AJILI YA MPAMBANO WAO WA OCTOBER 2 KIMARA KOROGWE


Na Mwandishi Wetu

BABONDIA mbalimbali watakaozipiga siku ya jumapili ya October 2 katika ukumbi wa White House Bar Kimara Korogwe watapima uzito pamoja na Afya zao kesho jumamosi katika ukumbi uho kwa ajili ya kuzipiga siku inayo fuata

akizungumzia mpambano uho kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote watapia uzito pamoja na Faya Zao siku ya jumamosi

aliwataja baadhi ya mabondia watakaozipiga na kesho watapima uzito ni Said Chino atakaezitwanga na haidar Mchanjo uzito wa kg 57 raundi sita wakati Abdallah Ruwanje atavaana na Shedrack Ignas mpambano wa raundi sita la uzito wa kg 63wakati bondia mkongwe kabisa katika mchezo wa masumbwi nchini Mustafa Doto atazipiga na bondia chipkizi Manyi Issa katika uzito wa kg 61 raundi sita

mipambano mingine itawakutanisha mabondia Mohamed Muhunzi atakaepambana na Kassim Ahmad na Hashimu Chisora atazipiga na Rojas Masam uzito wa kg 61 na Julias Jackson atapambana na Emilio Norfat mpambano wa raund 4 uzito wa kg 61  na Ellsame Mbwambo atazipiga na Emanuel Kisawani mpambano wa raundi 4 uzito wa kg 61

siku hiyo pia kutakuwa na elimu ya ujasiliamali kwa vijana wa mchezo wa masumbwi pamoja na kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kujikwamuwa na uchumi 

Mgeni rasmi katika mpambano uho atakuwa
Humphrey Polepole Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
 
Katika Mchezo huo kutakua na Uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. 

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...