Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 3, 2019

ROJAS MASAMU ATAMBA KUMZIMISHA KWA K,O IDD MKWERA YA MAPEMA SANA SIKU YA PASAKA APRIL 21


Bondia Ramadhani Mbegu 'kushoto' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Idd Mkwera wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika siku ya pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu magomeni Mapipa Mbegu atacheza na Rashidi Mnyagatwa na Mkwera atapambana na Rojas Masamu 

Bondia Idd Mkwera  'kushoto' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde naRamadhani Mbegu wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika siku ya pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu magomeni Mapipa Mbegu atacheza na Rashidi Mnyagatwa na Mkwera atapambana na Rojas Masamu 

Bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Shehe Azizi wakati wa maoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika siku ya Pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu Kiwale atapambana na Luckman Ramadhani na Azizi atapambana na Hussein Shemdoe


Na Mwandishi Wetu

Bondia Rojas Masamu ametamba kumsambalatisha Idd Mkwera katika raundi za awali kwani ataki kuwapa tabu majaji akisungumzia mpambano wake uho Masamu amesema kuwa kwa sasa yupo fiti na ana uchu wa kupambana yani kipigo nitakacho mpa mkwera atokuja kuki sahau mpaka anaingia kaburini najiamini kwa kuwa nimefanya mazoezi ya kutosha na nipo vizuri kila idara hivyo ajipange tu kwa kipigo

nipo kambini sasa yapata miezi miwili kwa ajili ya mpambano uhu asichukulie poa kabisa kwani kwa sasa nimeongeza dozi ya kufanya mazoezi nilikuwa nafanya mara mbili kwa siku lakini kwa sasa nafanya mara tatu kwa kuwa nataka kumpiga kwa K,O mbaya ambayo itawashangaza wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi


Mpambano uho ulioandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku ya sikukuu ya Pasaka limepewa nguvu na 

Bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia  bondia huyo ndie aliesababisha mabondia hawo wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio mana akaongeza nguvu ili mpambano uho ufanyike

Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia Hussein Pendeza atamkabili Juma Ramadhani 'Choki' na Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede wakati ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atakabiliana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Shabani Mbogo Hussein Shemdoe na Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atakumbana na Sandali Nyambala

Mapambano yote hayo yanaletwa kwenu na kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinuwa vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa

na kupitia kampuni ya Super D Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili kuwasaidia vijana mbalimbali kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...