Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 3, 2010

MREMBO ALICE LUSHIKU AWA MISS KINONDONI


Miss Kinondoni 2010 Alice Lushiku akiwa katika picha ya pamoja na warembo wenzake baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Miss Konondoni lililomalizika Dar es salaam jana kwenye ukumbi wa Mlimani City, kulia ni mshindi wa pili Amisu Malick na mshindi wa tatu ni Irene Hezron na wa nne Edna Kwisasa na tano Carolene Mbembo
Miss Kinondoni 2010 Alice Lushiku akiwa katika picha ya pamoja na warembo wenzake baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Miss Konondoni lililomalizika Dar es salaam jana kwenye ukumbi wa Mlimani City, kulia ni mshindi wa pili Amisu Malick na mshindi wa tatu ni Irene Hezron na wa nne Edna Kwisasa na tano Carolene Mbembo
Alice Lushiku akijibu swali
Irene Helron akijibu swali
Edna Kwisasa akijibu swali

Caroline Mbembo akijibu swali wakiti wa onesho hilo ata hivyo alichemka kujibu baada ya kutaja mbuga ya Serengeti ni Mlima mkubwa alichemka vibayaa sanaaa
warembo walioingia 5 bora
Warembo 11 walioshiliki kinyanganyiro cha kumtafuta miss kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja
mrembo mwenye kipaji cha kucheza akicheza

Carolene Mbembo mrembo mwenye kipaji cha kuimba
ISSA MNALI AKIWA KAZINI

kamati ya miss Ilala wakiwa na warembo wa Ilala

wadau wa urembo warikuwepo Selemani Mbuguni na Khadija khalili
Miss Temeke walikuwepo kuangalia mchuano huu klabla ya kufanyika mashindano yao Ijumaa

wanenguaji wa bendi ya twanga pepeta wakiwajibika jukwaani

Suzan Chubwa Queen Suzi akifanya vitu vyake wakati wa kumtafuta Miss Kinondoni

Friday, July 2, 2010

KUMEKUCHA DODOMA


Kikundi cha Ngoma cha Wanawake cha Mjini Dodoma wakitumbuiza wakati wa mapokezi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi mjini Dodoma jana.

JK AZINDUA MRADI WA MAJI


JAKAYA KIKWETE akifunua kitambaa kushiria kuzindua rasmi mradi wa maji wa Mugumu Serengeti uliofanyika katika bwawa la Manchira, Mugumu,wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara leo asubuhi

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AFANYA ZIHARA KWENYE MIRADI YA MAJI



mh lukuvi akiwa anatangaza utekelezaji wa zihara aliyofanya Rais alipotembelea miradi ya maji hapo may 24.2010 na wa pili ni CEO wa DAWASCO JACKSON MIDALA.

WADAU WAFUNGA NDOA NA KUACHANA NA MAISHA YA UKAPELA


Wakiwa na nyuso za kuanza maisha mapya ni wadau wa blog hii Bi. Jamila Rajabu na Bw.Mohamed Hamza
JAMILA RAJABU ANAMEREMETA
WANAMEREMETAA

MAXIMO AAGWA NA KUTOA NENO LA MWISHO KWA WATANZANIA


Meneja Uhusiano na mawasiliano wa kampuni ya SERENGETI TEDDY MAPUNDA akiwa na MAXIMO wakati wa hafla ya kumuaga
wadau kutoka wizarani wakiwa na kocha wa taifa
Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa,Taifa Stars akiwa katika picha ya pamoja na Meneja mkuu wa Uhusiano na Mwasiliano Teddy Mapunda wakati wa sherehe ya kumuaga kocha huyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

MISS KINONDONI KUPATIKANA LEO


WAREMBO WANAOWANIA TAJI HILO WAKIWA NA WARATIBU WA SHINDANO

HOSPITAL YA MKOA DODOMA YAPIGWA TAFU NA CRDB


Waziri wa afya Mh. Prof. David Mwakyusa akiwasili katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa Dododma ili kupokea wodi na vifaa vilivivyotolewa na Benki ya CRDB, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dk. Charles Kimei, Naibu Waziri wa Afya Mh.Dr. Aisha Kigoda na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.James Msekela
Waziri wa Afya Mh.David Mwakyusa akikata utepe kufungua rasmi wodi ya kinamama ya hospitali ya mkoa wa Dodoma iliyokarabatiwa kwa msaada wa Benki ya CRDB.

MSONDO JUMAPILI HII KUTUMBUIZA KWENYE MBIO ZA MWENGE MBAGALA


Msondo ngoma wakiwa jukwaani
Waimbaji wa msondo wakiwajibika kushoto ni Eddo Sanga na Isihaka Katima

Mkurugenzi wa msondo ngoma akiwa na jk
BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma inatarajia kutoa burudani katika sherehe za mbio za mwenge zitakazofanyika jumapili Mbagala Zakiem, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema, kutokana na kushiriki katika maadhimisho hayo hivyo bendi hiyo haitaweza kutoa burudan katika onesho lao la kila jumapili linalofanyika katika Ukumbi wa Africenter, Ilala jijini Dar es salaam.

Alisema, kutokana na sababu hizo uongozi wa bendi hiyo unawaomba radhi wapenzi wa bendi hiyo kwa usumbufu utakaojitokeza ambapo wataendelea na burudan hiyo kwa jumapili ya wiki itayofuata.

"Tunawaomba radhi mashabiki wetu kutokana na hali hiyo kwa hiyo ni moja ya utendaji na majukumu ya bendi hiyo katika kutoa burudan katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na shughuli za kiserikali hivyo wataungana nao katika jumapili ya wiki itaakayofuata," alisema Super D.

Super D amewataka wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake kuhudhuria kushuhudia burudan hiyo watakayoitoa ikiwa ni pamoja kusikia nyimbo zao mpya ambazo ni miongoni mwa nyimbo zitakazo kuwa katika albamu yao mpya ya mwaka huu ikiwa ni pamoja kusikiliza nyimbo zao za zamani.

Alizitaja nyimbo hizo mpya kuwa ni Mjomba, Dawa ya deni kulipa na lipi jema ambapo albamu hiyo inatarajia kuachiwa mwishoni mwa mwaka huu.

Thursday, July 1, 2010

RAIS WA NIGERIA ASIMAMISHA TIMU YA TAIFA KUTO SHIRIKI MICHEZO YOYOTE YA SOKA KIMATAIFA


Na alice ngubwene
Ndugu mpenzi au mshabiki wa soka popote ulimwenguni , nimesikitishwa sana na kauli ya Rais wa nigeria kuifungia timu yake ya taifa kutocheza mechi za kimataifa kwa muda wa miaka miwili. Katika utaratibu huu napata maswali mengi ambayo yananifanya niulize ni jinsi gani ushiriki wa Serikali katika swala zima la michezo popote duniani, na napata wasiwasi kuwa tunakokwenda kama FIFA haitajizatiti katika kanuni zake basi kila nchi itakuwa inajichukulia maamuzi yake , maana unaweza kusikia hata mpira miguu ukafungiwa bila sababu za msingi!

Katika kauli iliyotolewa juzi na Rais wa nigeria Goodluck Jonathan , inabidi nipate wasiwasi huyu Mshauri wa Rais katika maswala ya michezo ana ufahamu gani haswa katika nyanja hizi, Wakati michezo na haswa soka ni mchezo ambao unatumika duniani kote kama kivutio katika kuleta amani na mshikamano duniani kote, hata nchi zenye vita inapofika swala la michezo watu huweka silaha chini na kufurahia burudani.

Kauli hii naifananisha na ya mtu ambaye hana ufahamu kabisa katika maswala michezo hasa soka na michwezo mingineyo kuwa michezo ni burudani , kama ameshauriwa na mgonjwa labda wa kili hivi yaani sipati picha kabisa. ukifuatilia kwa makini nchi ya Nigeria imekuwa na wachezaji maarufu tanug miaka ya 90 na ulimwengu mzima umekuwa ukitambua mchango wao katika soka. Mchakato wao na chama chao cha soka kimekuwa kiligubikwa na mambo mengi katika uteuzi wa kocha mpya baadaya kumfukuza kocha wao aliyewapeleka katika kombe la mataifa ya afrika Bw. shaibu Amodu na kukaa muda mrefu bila kocha huku cha mpira wa miguu cha nigeria NFF kikiangaika kupata kocha mwingine kwa ajili ya kuongozana timu yao katika mashinda ya WOZA 2010.

kila mtu anatambua ni muda gani Bw Lagerbacks amepokea timu hiyo ya nigeria, inasikitisha sana maana tunasahau kuwa hata uteuzi wake aliofanya katika kikosi hicho uligubikwa na presha kutoka chama chao cha mpira wa miguu NFF. sasa iweje nigeria ifanye maamuzi magumu kama haya ambayo hayaleti kuimarisha bali kubomoa kabisa, kwanini asiunde kamati ambayo itachunguza kwa nini timu imeshindwa kuendelea katika hatua ya pili katika mashindano hayo na baada ya kujua mapungufu hayo yakatafutiwa tiba yake. Mfano hata kuwahusisha wanasoka wa zamani ambao walipata mafanikio ndani na nje ya nchi zao katika ufanya mabadiliko na mapinduzi ndani ya vyama vyao vya mpira.

Katika mashindano lazima tukubali kuwa kuna kushinda na kushindwa , nigeria kama timu za nchi nyingine mfano ureno,ufaransa, uingereza, mexico, italy na nyinginezo nyingi tena bora sana zimeshindwa kufuzu nakuendelea na mashindano hayo. FIFA imeweka wazi kabisa kanuni zake ambazo zinaeleza wazi namna serikali kutokuingilia mambo michezo
.
Nafikiri kukiwa na misingi ya utawala bora katika nchi yeyote ndani ya vyama vya mpira, hiyo tu inatosha kuweka mikakati bora ya kusaidia timu za mpira pamoja michezo mingine kufanya vizuri kitaifa na kimataifa. na Kuzuia sio jawabu litakalosaidia aina yoyote ya mchezo kuunda timu bora hapo siku za usoni , bali ni sawa na kubomoa hata kilo ulichonacho kitaharibika. ni sawa kusimamisha wanafunzi wa shule ambao siku za usoni utegemee watatoa matokeo bora ya mtihani!!

kwa maoni zaidi wasiliana na 0733 660669

MAHADHIMISO YA SIKU YA SERIKALI YA MTAA YAFANYIKA MNAZI MMOJA LEO


Imma Mbuguni akiangaria vitu mbalimbali wakati wa sherehe hizo
Diwani wa Kata ya ukonga akiwapa maelekezo waandishi wa habari
wadau wa usafi wa Wilaya Ilala walikuwepo
Mkuu wa Wilaya Ilala Leonidas Gama akipewa zawadi
watoto wakicheza Kiduku
Mkuu wa Wilaya Ilala Leonidas Gama akipata maelekezo

Kikundi cha ngoma cha Lumuma kikitoa burudani wakati wa Maadhimisho ya Sherehe ya siku ya Selekali ya mtaa iliyofanyika Dar es salaam

URENO HAIKUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA

Na alice ngubwene
kama kawaida ureno nayo imefungasha virago kama timu zingine baada ya ya kupigwa bao moja bila na timu ya hispania.
Pamoja na kuingia kwa kishindo katikano hatua ya pili ya mashindano hayo Woza WC2010, ureno imeshindwa kuonyesha cheche zake na kuishia kuonyesha mchezo usiovutia kwa kushindwa pia kumfanya mshambuliaji wao kinara Christiano Ronaldo ang'are katika mashindano hayo kwa kukosa kuwa mpachika mabao bora kama alivyozoeleka akitokea klabu yake ya zamani ya Manchester united.

Ukilinganisha na vijana wa Vicente DeleBosque ambao baada ya kushtukizwa na kipigo cha goli moja kutoka kwa waswisi, hispania walijitahidi kuonyesha kiwango tofauti katika mechi zake zilizosalia katika mashindano hayo huku kinara wao wa kupachika magoli David villa aking'ara.

Timu zote zinajifunza kutokana na makosa kadri mashindano yanavyoendelea kupamba moto. Lakini haikuwa hivyo kwa vijana wa Quieroz ambao walionyesha udhaifu huo katika mpangilio wawapo uwanjani. ni aibu kidogo kwa wachezaji wa ureno ambao waliingia kwa kishindo katika mtoano wa raundi ya pili. Mechi hiyo na hispan ilianza kwa kasi nzuri ambapo vijana Del Bosque kina Torres na Villa wakipeleka mashambulizi maakali ambayo yaiokolewa na kipa wa ureno Eduardo.

Ukiangalia vema utagundua kuna tofauti kubwa kati aina ya uchexzaji na ubora ulioonyeshwa na hispania ukilinganishwa na wachezaji wa hispania. Hata kocha Dunga wa Brazil naye alijaribu kuwasema wareno kuwa walionyesha uchezaji ambao ni wa uzuiaji zaidi na sio wa kufurahisha!! ni mchezo ambao umeanzishwa na "the Special one" kocha wa baadaye wa ureno kwa asilimia 99 wa kuweka bus golini kama waingereza wasemamavyo, ingawa yeye anapinga hilo. mchezo huo ulionyeshwa zaidi na wachezaji wa ureno haukufurahisha na kufanya mchezo usiwe na mvuto na kasi yoyote!

Lakini pamoja ukuta uliowekwa na wachezaji wa ureno David villa alifanikiwa kuwadhihirishia kuwa yeye ni mshambuliaji mwenye uchu wa magoili wakati wote pale alipoipatia timu yake goli zuri baada ya kupokea pasi nzuri upande wa kushoto kutoka kwa mchezaji mwenzie na kuwezesha mabingwa hao wa ulaya kutoka kifua mbele na kuwavusha kuingia katika hatua ya robo fainali

Sawa Kocha wa ureno na wachezaji wake wanastahili kupata pongezi kwa kiwango chao cha uzuiaji lakini ingefurahisha kama wangeonyesha mchezo huo kama tayari wangelikuwa na mabao ya kutosha kuyalinda, tatizo lao walikuwa wanalinda hewa maana hawakuwa na chochote!

kwa maoni zaidi wasiliana na 0733 660669

WASHINDI DONDOKA SAUZ YA ZANTEL WAONDOKA LEO


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la Leo
WASHINDI WA DONDOKA SAUZ WAELEKEA ROBO FAINALI
Dar es Salaam, Julai1, 2010: Washindi 3 wa promosheni ya Dondoka Sauz na Hyundai na Zantel leo wameondoka nchini kuelekea Johannesburg, Afrika Kusini kwenda kutazama mechi ya robo fainali itakayochezwa siku ya Ijumaa, tarehe 2, Julai 2010. Mechi watakoyoshuhudia washindi hawa ni ile itakaoyochezwa uwanja wa Soccer City kati ya timu pekee ya Afrika iliyobaki kwenye michuano hiyo, Ghana itakoyocheza na timu ya taifa ya Uruguay.
Washindi hao 3 ni Abri Khalid, Mohammed Mohammed na Shehe Said na watakaa Afrika Kusini kwa siku 3 wakiwa wamelipiwa gharama zote ikiwa ni malazi, chakula, usafiri pamoja na fedha za matumizi.
“Siamini muda wa kwenda umewadia na nimekuwa nikiusuburia kwa muda mrefu siku hii na ninafuraha isiyo na kifani kwani mechi ambayo tunaenda kuiona ni ile ya timu pekee ya kiafrika iliyobaki kwenye michuano Ghana. Ningependa kuwashukuru Zantel kwa fursa hii na ninamatumaini makubwa na safari hii kwani nategemea kushuhudia mambo mengi ya kihistoria.” alielezea Bw. Abri, mmoja wa washndi hao.
Washindi hawa wanatarajiwa kukaa jijini Johannesburg kwa muda wa siku 3 na watarejea nchini siku ya Jumapili. Wakiwa Afrika Kusini watapata fursa ya kutembelea sehemu maarufu za mji wa Johannesburg pamoja na kujifunza historia, mila na desturi za watu wa Afrika Kusini. Kundi la pili la washindi litaondoka siku ya Jumatatu kuelekea Cape Town ambako watashuhudia mechi ya nusu fainali itakayochezwa tarehe 6 Julai.
Promosheni ya Dondoka Sauz bado inaendelea na kwani Zawadi kubwa ambayo ni gari aina ya Hyundai Tuscon ya mwaka 2010 yenye thamani ya milioni 50 bado hajapata mshindi. Mteja wa Zantel anaweza kujishindia gari hili kwa kutuma ujumbe mfupi FIFA kwenda namba 15726 na kujilimbikizia pointi zitakazomuwezesha kushinda gari. Droo ya kupata mshindi wa gari itachezwa tarehe 30 Julai, 2010.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Sharon Costa, PR Manager, ZANTEL, sharoncosta@zantel.co.tz

Kuhusu Zantel:
Hadithi na historia ya kampuni ya simu za mikononi ya Zantel inahusu uwekezaji, ubunifu wa bidhaa bora na za kisasa, na yenye uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja wake. Licha ya hayo, ni hadithi inayohusu ukuwaji na uwezo wa kutoa faida kubwa kwa watumiaji wa simu za mikononi nchini Tanzania. Ikianzishwa mwaka wa 1999, kampuni ya simu ya Zanzibar ina ubia kati ya serikali ya Zanzibar kwa 18%, kampuni ya simu ya Emirati (ETISALAT) kwa 65%, na kampuni ya Meeco International kwa 17%.

WAANDISHI WATOA SAPOTI KWA KOCHA MPYA WA ZANZIBARI


Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Zanzibar, Stewart Hall, kutoka Uingereza akisaini mkataba wa miaka mitano wa kuifundisha timu hiyo katika hafla iliyofanyika kisiwani. kushoto kwake ni Rais wa Shirikisho la Soka la Zanaibar (ZFA) Ali Ferej Tamim
waandishi wa habari wakiwa makini wakati wa kusaini mkataba wa kocha mpya wa ZANZIBAR
SOPHIA ,MWANI, JAKIPEMBA ,TOLE wakiwa na nyuso za furaha kabla ya kufika ZANZIBARA lakini walipofika mambo yalikuwa tofauti wakanuna bwana
BAADA YA STEWART KUSAINI MKATABA WA MIAKA MITANO SASA RAIS WA ZFA ALI FEREJ TAMIM AKISAIN.na jenejohn5.blogspot
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...