Marquee
tangazo
Thursday, July 1, 2010
WASHINDI DONDOKA SAUZ YA ZANTEL WAONDOKA LEO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la Leo
WASHINDI WA DONDOKA SAUZ WAELEKEA ROBO FAINALI
Dar es Salaam, Julai1, 2010: Washindi 3 wa promosheni ya Dondoka Sauz na Hyundai na Zantel leo wameondoka nchini kuelekea Johannesburg, Afrika Kusini kwenda kutazama mechi ya robo fainali itakayochezwa siku ya Ijumaa, tarehe 2, Julai 2010. Mechi watakoyoshuhudia washindi hawa ni ile itakaoyochezwa uwanja wa Soccer City kati ya timu pekee ya Afrika iliyobaki kwenye michuano hiyo, Ghana itakoyocheza na timu ya taifa ya Uruguay.
Washindi hao 3 ni Abri Khalid, Mohammed Mohammed na Shehe Said na watakaa Afrika Kusini kwa siku 3 wakiwa wamelipiwa gharama zote ikiwa ni malazi, chakula, usafiri pamoja na fedha za matumizi.
“Siamini muda wa kwenda umewadia na nimekuwa nikiusuburia kwa muda mrefu siku hii na ninafuraha isiyo na kifani kwani mechi ambayo tunaenda kuiona ni ile ya timu pekee ya kiafrika iliyobaki kwenye michuano Ghana. Ningependa kuwashukuru Zantel kwa fursa hii na ninamatumaini makubwa na safari hii kwani nategemea kushuhudia mambo mengi ya kihistoria.” alielezea Bw. Abri, mmoja wa washndi hao.
Washindi hawa wanatarajiwa kukaa jijini Johannesburg kwa muda wa siku 3 na watarejea nchini siku ya Jumapili. Wakiwa Afrika Kusini watapata fursa ya kutembelea sehemu maarufu za mji wa Johannesburg pamoja na kujifunza historia, mila na desturi za watu wa Afrika Kusini. Kundi la pili la washindi litaondoka siku ya Jumatatu kuelekea Cape Town ambako watashuhudia mechi ya nusu fainali itakayochezwa tarehe 6 Julai.
Promosheni ya Dondoka Sauz bado inaendelea na kwani Zawadi kubwa ambayo ni gari aina ya Hyundai Tuscon ya mwaka 2010 yenye thamani ya milioni 50 bado hajapata mshindi. Mteja wa Zantel anaweza kujishindia gari hili kwa kutuma ujumbe mfupi FIFA kwenda namba 15726 na kujilimbikizia pointi zitakazomuwezesha kushinda gari. Droo ya kupata mshindi wa gari itachezwa tarehe 30 Julai, 2010.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Sharon Costa, PR Manager, ZANTEL, sharoncosta@zantel.co.tz
Kuhusu Zantel:
Hadithi na historia ya kampuni ya simu za mikononi ya Zantel inahusu uwekezaji, ubunifu wa bidhaa bora na za kisasa, na yenye uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja wake. Licha ya hayo, ni hadithi inayohusu ukuwaji na uwezo wa kutoa faida kubwa kwa watumiaji wa simu za mikononi nchini Tanzania. Ikianzishwa mwaka wa 1999, kampuni ya simu ya Zanzibar ina ubia kati ya serikali ya Zanzibar kwa 18%, kampuni ya simu ya Emirati (ETISALAT) kwa 65%, na kampuni ya Meeco International kwa 17%.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment