Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 29, 2010

TBL ZAIDHAWADIA TASWA


Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milion 4.8 kwa Mwenyekiti wa TASWA FC,Majuto Omary kwa ajili ya mashindao ya Bonanza huko mkoani Arusha.katikati ni Afisa Uhusiano wa TBL,Lilian Erasmus


Meneja Uhusiano wa kampuni ya bia TBL Edith Mushi akizungumza na wanahabari katika ofisi za kiwanda hicho wakati alipokabidhi mfano wa hundi ya Shiilingi milioni 4 kama msaada kwa ajili ya Chama cha wandishi wa habari TASWA inayokewanda katika mashindano ya Bonanza yatakayofnyika mkoani Arusha jumapili.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetoa sh. 4, 875,000 kwa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (TASWA FC) kwa ajili ya kushiriki katika bonanza la waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha. Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omary katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TBL. Alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya usafiri wa kwenda na kurudi, chakula na posho kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa siku zote watakazo kuwa Arusha. Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Meneja Uhusiano wa TBL, Edith Mushi alisema kuwa msaada huo ni moja ya kazi za TBL katika kusaidia jamii na safari hii wameamua kufanya hivyo kwa waandishi wa habari. Mushi alisema kuwa mbali ya msaada kwa jamii, lengo la TBL pia ni kudumisha ushirikiano wa karibu kwa waandishi wa habari ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya michezo na katika sekta nyingine hapa nchini. Alisema kuwa wanaamini kuwa mchango huo utaleta mafanikio kwa timu hiyo na kuweza kutetea vyema taji lake. “TBL inatambua na kuthamini mchango wenu katika maendeleo ya sekta mbali mbali ikiwa pamoja na michezo, tunayo furaha kubwa kuona leo hii mmekuwa mfano wa kuonyesha kwa vitendo mchezo wa soka, tunawatakia kila la kheri katika mashindano hayo na katika kazi ya kuelimisha na kukosa jamii,” alisema Mushi. Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omary alishukuru TBL kwa msaada huo mkubwa ambao umeipa nafasi timu yake kutetea ubingwa wake ipasavyo. Majuto alisema kuwa TBL imeonyesha mfano wa kuigwa kwa jamii kwani imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia masuala mbali mbali ya jamii hapa nchini. “Hii ni faraja kuwa kwa TASWA FC kwa kuwa na kampuni yenye kujali waandishi kama TBL, tunaahidi kufanya vyema katika mashindano hayo na kuibuka na ushindi,” alisema Majuto. Alisema kuwa Tanzania kuna makampuni mengi sana, lakini kutokana na kutojua umuhimu wa waandishi wa habari, wameshindwa kuchangia punde waombwapo misaada, na mara nyingi wakitoa majibu ya barua ya maombi kwa njia ya simu siku tatu kabla ya safari ya kuwa ``ombi lenu halikufanikiwa’’. “Kwa kweli tumepata usumbufu mkubwa sana, kwani tulikuna vichwa ili kujua nini kifanyike ili kuikomboa timu na kufanikisha safari yetu,” alisema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...