Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 10, 2010

MISS TEMEKE HAPATIKANA


Miss Temeke 2010 Geneviva Emmanuel akipungia mashabiki mkono mara baada ya kumtangaza mshindi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam kushoto ni mshindi wa pili Anna Daud na kulia ni mshindi wa tatu Britania Urasa, Mwenyekiti wa kamati ya Miss Temeke Bw. Benny Kisaka alisikika akisema hizi ndiyo pini za Miss Temeke zitakazo wakilisha shindano la taifa la Vodacom Miss Tanzania hapo baadae na tuna uhakika na pini hizi kwamba zitatikisa katika shindano hilo kubwa nchini na kushinda hatimaye kumpata Miss Tanzania kutoka kandaTemeke.
tano bora ya Miss Temeke 2010 mara baada ya majaji kutangaza matokeo hayo www.fullshangwe.blogspot.com

Friday, July 9, 2010

WAISLAM WAANDAMANA KUDAI MAHAKAMA YA KADHI NCHINI


Waislamu wakiandamana na Bango lenye ujumbe unaosomeka Tunataka Kadhi anayetambulika Kikatiba na si BAKWATA na CCM Kadhi lazima hata kwa Jihad" maandamano hayo yameanzia katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia maeneo ya Manzese jijini Dar es salaam.
Waislamu wakifanya Maandamano katika barabara ya Morogoro wakidai mahakama ya Kadhi leo mara baada ya swala ya Ijumaa www.fullshangwe.blogspot.com

FRANCIS KIFUKWE ATANGAZA KULETA MAENDELEO KWA KIPINDI CHA MIEZI 6 TU


Francis Kifukwe
Francis Kifukwe akizungumza na waandishi wa habari kuusu makakati yake ya kuleta sakos yanga na maendeleo kwa kipindi cha miezi 6 tu endapo wana yanga watampa nafasi kuingia madarakani


MGOMBEA nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Francis Kifukwe anapewa nafasi kubwa ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Julai 18, mwaka huu.

Uchaguzi mkuu wa klabu hiyo umepangwa kufanyika katika ukumbi wa PTA uliopo kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wachama wa klabu hiyo Mohamed Sadiq Muddy Kala, alisema kuwa, Kifukwe ana nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kutokana na kuwa na uzoefu wa uongozi katika klabu hiyo.

“Huyo jamaa pamoja na mapungufu yake, bado ana nafasi ya kuwa Mwenyekiti wetu, uzoefu wake na mikakati aliyonayo, inatupa imani wana Yanga,” amesema.

Mwanachama huyo amesema hivi sasa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga, anaendelea na mipango yake ya kumsajili mchezaji nyota ambaye mambo yakikamilika, atatangazwa.

Wagombea wanaowania nafasi ya uenyekiti ni Kifukwe, Abeid Abeid, Lloyd Nchunga, Mbaraka Igangula na Edgar Chibura.

Nafasi ya makamu mwenyekiti inagombewa na Costantine Maligo, Ayoub Nyenza na Davis Mosha wakati nafasi za ujumbe wa Kamati ya Utendaji zinawaniwa na wanachama 29.

“Kifukwe baada ya kurejeshwa kwenye mbio za uchaguzi na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sasa njia ni nyeupe kwake,” amesema.

Awali, Kifukwe na Abeid waliondolewa katika mbio za uchaguzi wa klabu hiyo na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo baada ya kushindwa kuwasilisha vielelezo vilivyokuwa vikitakiwa, lakini Kamati ya TFF iliwarejesha kufuatia rufani yao.

Mgombea nafasi ya uwenyekiti wa Yanga Francis Kifukwe (kushoto) akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa kumwaga sela zake leo

ZANTEL NA TIGO ZAJIUNGA NA NMB MOBILE


BENK ya NMB imeungana na Kampuni ya simu za mkononi Zantel na Tigo kwenye huduma ya NMB Mobile ili kuwapa nafasi wateja wa NMB kutumia huduma hiyo kupitia mitandao hiyo.

Hadi sasa idadi ya mitandaa ambayo imeunganoshwa na huduma hiyo ya NMB Mobile imefikia minne ambapo mbali na Zantel na Tigo pia huduma hiyo ilikuwa ikitolewa na NMB kwa wateja waliokuwa wanatumia mtandao wa Vodacom na Zain.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya NMB Mobile kwenye mtandao wa Zantel na Tigo Mkurugenzi wa NMB Bw. Ben Christiaanse alisema hadi sasa huduma ya NMB Mobile imetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ikiwa inatumia mitandao ya Zain na Vodacom.

"NMB Mobile inatimiza kwaka mmoja sasa ikiwa na jumla ya wateja 250,000 wakati tukiwa tumeungana na wateja wanaotumia mtandao wa Vodacom na Zain lakini sasa tumeongeza mitandao mingine miwili ambayo ni Zantel na Tigo ili kuwapa fursa wateja wetu wanaotumia mitandao yote kupata huduma ya NMB Mobile,"alisema Bw. Christiaanse.

Alisema kwa wateja wa huduma hiyo ambao bado hawajajiunga na NMB Mobile watatakiwa kujiunga kwa kuandika alama ya nyota kisha 150 nyota 66 nyota 123 halafu alama ya reli ambapo moja kwa moja atakuwa ameungwa katika huduma hiyo.

Alisema huduma ya NMB Mobile inamuwezesha mteja kutuma fedha, kuangalia salio, kununua luku, kununua muda wa hewani wa Zantel, Tigo, Vodacom na Zain.

Alisema pia mteja anaweza kujiunga na huduma ya NMB Mobile kwa kutumia mashine za kutolea fedha ATM ambapo kwa sasa Benki hiyo inamashinne zaidi ya 300 na kwamba hadi mwishoni mwa mwaka huu wanatarajia kuwa na ATM 380.

OLIMPIKI AFRIKA KUANZA JUMATATU


bendera ya Tanzania ikipepea wakati wa michuano hiyo iliyofanyika miaka iliyopita
WATANZANIA wameombwa kuwaunga mkono na kuwaombea dua wanamichezo wanne ambao wanaondoka nchini kesho kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kwanza kwa vijana ya Olimpiki Afrika (ANOKA) yanayoanza jumatatu Rabat nchini Morocco.



Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa kuwakabidhi wanamichezo hao bendera ya Taifa , ambao watashiriki katika mchezo wa riadha na kuogelea, Mkurugenzi wa Michezo Zanzibar Gulam Rashid alisema, wanamichezo hao wanatakiwa kuungwa mkono na kila mtanzania kutokana na kwamba wanashiriki kwa mara ya kwanza mashindano makubwa kama hayo huku wakiwa ni vijana wadogo.



"Tunatakiwa kuwaunga mkono na kuwaombea dua ili waweze kufanya vizuri na kuiwakilisha vyema nchi, hivyo kila mtanzania anatakiwa kuwaunga mkono kwa kuwapa sapoti hata watakapokuwa wameshindwa kwani hayo ni mashindano na nchi nyingi zinashiriki na si kuwaandika vibaya katika vyombo vya habari,"alisema Rashid.



Wanamichezo hao kwa upande wa riadha ni Marwa Mwita atakayekimbia meta 1,000 na 3,000 ambao wataambatana na mwalimu wao Meta Petrol ambapo wanariadha hao waliweka kambi mjini Arusha.



Kwa upande wa kuogelea ni Adam David atakayeogelea umbali wa meta 50 pamoja na Mariam Foum ambaye pia ataogelea umbali huo huo kwa stail ya Freestyle.



Naye Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi alisema Kwa mara ya kwanza Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilizindua kwa mara ya kwanza michezo ya Olimpiki kwa vijana chini ya miaka 17 mwanzoni mwa mwaka 2008 na kupendekezwa Singapore kuwa mwenyeji wa michezo hiyo.


"Kamati za Olimpiki za nchi wanachama zilialikwa kushiriki aidha kwa kufikia viwango vilivyotolewa na vyama vya kimataifa au kuomba nafasi za upendeleo ,"



"Kwa kuzingatia vyama vyetu kutokuwa na idadi kubwa ya vijana wenye umri huo ambao wangeweza kufikia viwango, TOC, iliomba nafasi ya upendeleo kwa vyama vya riadha, kuogelea, mpira wa meza na ngumi lakini IOC ilitupa nafasi kwa michezo miwili rianda na kuogelea,"alisema Bayi.



Wanamichezo hao wanatarajia kuondoka leo na ndege ya shirika la Qatar ambapo mkuu wa msafara atakuwa ni Peter Mokani ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC.

Thursday, July 8, 2010

FIESTA JIPANGUSE YATIKISA MOROGORO


Hamisi Mwijuma mwana FA alikuwepo
watu kibao walikuwepo si mchezoooo
Unapoona Jahazi lataka kuzama nahodha huingia kati...Huyu ni DJ Ruge akijipangusa na maskrach ya ukweli katika tamasha la Fiesta Jipanguse mambo yote haya yalikuwa usiku wa kuamkia leo.
Mshindi wa tuzo 3 za Kili Music Award 2010 almaarufu mzee wa Mbagala Diamond akiimba nyuma ya jukwaa.

JK AIFAGIRIA BLAZIL


Rais Luiz Lula Da silva wa Brazil akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi namba 9 iliyosainiwa na Mwanasoka nyota wa timu ya Brazil Ronaldo de Lima jana mchana ikulu jijini Dar es Salaam.

EXTRA BONGO KUWASHA MOTO SAVOY HOTEL MOROGORO


BENDI YA EXTRA BONGO.

Bendi ya muziki EXTRA BONGO ambayo iliyokuwa itambulishwe katika ukumbi wa BWALO LA UMWEMA sasa itatambulishwa katika ukumbi wa SAVOY HOTEL, kutoka na ukumbi wa UMWEMA kuwa katika marekebisho.

WAREMBO WA MISS TEMEKE WATEMBELEA TBL


MISS TEMEKE

Meneja wa kinywaji cha Redd's Kabula Nshimo akizungumza na warembo

Injinia wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL) Tumain Moses (kulia) akiwaelekeza warembo wanaowania taji la miss Temeke walipotembelea kiwanda hicho jana Dar es salaam

RASHIDI MATUMLA MADA MAUGO KUMALIZA UBISHA JULAI 18



Mwandaji wa mpambano wa ngumi, Selemani Semunyu katikati akiwa na mabondia Rashidi Matumla (kushoto) na Mada Maugo wakati wa kutangaza mpambano wao wa kirafiki utakaofanyika julai 18


BONDIA mkongwe wa ngumi za kulipwa nchini, Rashid Matumla 'Snake Man', anatarajia kuzichapa na mpinzani wake Mada Maugo 'Junior', katika pambano lisilokuwa la ubingwa litakalofanyika Julai 18 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.
Akuzingumza na waandishi wa habari jana, Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania'TPBO', Yassin Abdalah 'Ustaadh' alisema kuwa mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni Julai 18 mwaka huu.

Alisema kuwa pambano hilo la uzito wa Middle lenye raundi 10, linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na historia za mabondia wote.
Abdalah alisema kuwa wameamua kuandaa pambano hilo ili kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa ngumi nchini.

Alisema kuwa pambano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Media Entertainment & Sports Promotion na linaratibiwa na TPBO.
Alisema kuwa maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na mabondia wote kuendelea na mazoezi katika kambi zao ambapo limedhaminiwa na Kampuni ya Business Times ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Majira, Spoti Starehe, Business Times na Dar leo na wamiliki wa kituo cha Redio cha 100.5 Times FM na Kampuni ya Uchapishaji ya Business Printer, PSI na Konsalt..

“Tumeandaa pambano la Maugo na Matumla kwa ajili ya kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa mchezo huo, ambapo maandalizi yote yameshakamilika na tunatajia kuwa mabondia hao watatoa burudani safi” alisema Abdalah.
Alisema kuwa pia pambano hilo litatanguliwa na mapambano mbalimbali kutoka kwa mabondia chipukizi kwa ajili ya kuendeleza na kuibua vipaji vya mchezo huo.

Alisema kuwa katika pambano hilo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ambapo bondia Abdalah Mohamed atazichapa na Said Zungu katika pambano la uzito wa Light Weight la raundi nne, Fadhil Maji atapigana na Sadick Abdulaziz katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne
Wengine ni Juma Afande atazichapa na Kitandula Zuberi katika pambano la Super Bantam la raundi nne, Juma Selema atapigana na Iddy Mgodomi katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne, Anton Mathias atazitupa na Hemed Mohamed wa Ashanti boxing ilala katika pambano la Super Fly la raundi nne na Kijepa Omari atazichapa na Joseph Richard wa Ashanti.

Wednesday, July 7, 2010

VIOLET MZINDAKAYA SISTA V KUGOMBANIA UBUNGE VITI MAALUMU RUKWA



SISTA V
AKITOA SHUKLANI KWA WASANII KWA KUMPA SAPOTI
Mwanamziki wa kizazi kipya Abwene Yesaya akimkabidhi shilingi laki moja kwa Katibu msaidizi wa Idara ya Itikadi na Uwenezi pia ni Mjumbe wa NEC Chama cha Mapinduzi CCM, Violet Mzindakaya kwa ajili ya kwenda kuchukulia fomu ya kugombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa Rukwa pesa hizo zimetolewa na wasaniaa Hamisi Mwijuma 'mwana FA na Abwene Yesaya AY kwa ajili ya kumpa sapoti kijana mwenzao ili aende kuwawakilisha vema bungeniMSANII wa Muziki wa kizazi kipya nchini Ambwene Yesaya 'AY' na Hamisi Mwinjuma 'Mwana FA', kwa pamoja wamemchangia sh. 100,000 mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) Violet Mzindakaya 'Sister V' kwa ajili ya kuchukua fomu ya ugombea wa nafasi ya viti maalum Mkoa wa Rukwa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango huo AY alisema, wao wamehamasika kumchangia kutokana na kwamba ni kijana mwenzao na kwamba anajua matatizo ya vijana hivyo atawakilisha vyema matatizo ya vijana Bungeni.

"Tumeamua kwa pamoja kutoa mchango huu kwa mwenzetu ili kuweza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo pia tunawaomba na watu wengine ambao wanaona yupo mtu atakayeweza kuwawakilisha vyema kutoa mchango wao kama tulivyofanya sisi,"alisema AY.

Kwa upande wake sister V amewashukuru na kuwapongeza wasanii hao kwa kuonesha na kuahidi atawawakilisha vijana wote vema pindi atakapopata nafasi ya kuchaguliwa ya kuingia Bungeni.

Sister V ambaye pia alikuwa mtangazaji wa avituo mbalimbali vya redio nchini ikiwemo KItuo cha redio cha 100.5 Times FM, redio Uhuru na Clouds FM amewaomba watanzania kumuunga mkono ili aweze kufanikiwa na kutimiza malengo ya vijana wote.

SHY-ROSE BHANJI NAE AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI


• Asema mwaka 2010 ubunge unahitaji tafsiri mpya
• Aainisha maeneo nane atayoyafanyia kazi
• Kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana
• abainisha umuhimu wa ofisi kila kata ndani ya jimbo

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Sadruddin Bhanji ametangaza kujitosa katika nafasi ya ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia CCM na lengo lake kubwa ni kuwa kiungo muhimu katika jamii ya wanakinondoni.

Akitangaza azma yake ya kuomba ridhaa kwa wanachama wa CCM katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Shy-Rose alisema kwa mtazamo wake neno ubunge kwa mwaka 2010 linahitaji tafsiri mpya kabisa. `…kwa sasa mbunge anatakiwa kuwa ni kiungo cha jamii badala ya kuwa mwakilishi wa jimbo kama ilivyozoeleka` alifafanua Shy-Rose.

`Mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko na ndio maana nimeona kwamba ili kila mwananchi kuweza kuwajibika, nafasi ya mbunge inahitaji kutafsiriwa upya ili iendane na wakati na matatizo ambayo yanayotukakabili wananch` alisema.

Kwa maana hiyo amesema kwamba hata sifa za mbunge zinahitaji kutafsiriwa upya kabisa, kwani majukumu yake yamebadilika kuendana na wakati. Ametaja baadhi ya sifa hizo mpya ni kuwa mhamasishaji, kiungo muhimu, kufanya kazi usiku na mchana na kuwa na ofisi katika kila kata ndani ya jimbo husika ili kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi.

`naomba nitoe tafsiri mpya ya neno ubunge..mbunge anatakiwa sasa awe ni kiungo muhimu kati ya walio na kipato kikubwa, kipato cha kati na wasio na kipato kabisa ili kwa pamoja jimbo liweze kupiga hatua za kimaendeleo. Mimi nitahakikisha kwamba nina ofisi katika kila kata ili niweze kuwafikia wananchi wangu katika kata zote kwani wakati napita kuomba kura ninawafuata na baada ya kufanikiwa kutimiza azma yangu ni wakati wa kuendelea kuwafuata na si wao kunifuata` alisema.

Kada huyo amesema sera yake kubwa itakuwa ni kumshirikisha kila mwananchi wa Kinondoni katika shughuli za kuleta maendeleo ili kila mtu aweze kutoa maoni, mawazo na mchango wa hali na mali katika kuleta maendeleo ya ukweli. Amesema hata mwananchi ambaye atakuwa hana uwezo, atabeba tofali kutoka upande mmoja hadi sehemu husika.

`nimeamua kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge kwa jimbo la hili ili niweze kuleta mageuzi makubwa sana katika jimbo la Kinondoni…naomba mfahamu kwamba kila mwananchi amebarikiwa akili, vipaji uwezo na Mwenyezi Mungu lakini asiposhirikishwa hataweza kutoa mchango wake, hivyo mimi nitahakikisha kwamba kila mmoja kwa uwezo wake na nafasi yake anachangia katika kuleta maendeleo`, alifafanua.

Shy-Rose alibainisha mambo makubwa ambayo atayapigania kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi ni elimu, afya, ajira kwa vijana, kupiga vita utumiaji wa madawa ya kuleta kwa vijana, kupigania haki za wasanii, kusaidia wajane katika kujikwamua kiuchumi na kuleta msukumo mpya kabisa katika masuala ya mahusiano na jamii ambayo kwa mtazamo wake eneo hili linahitaji msukumo mpya.

Shy-Rose amesema kwamba kutokana na uzoefu wa kazi zake tangu akiwa mwandishi wa habari, mtangazaji na Meneja uhusiano katika sehemu alizofanyia kazi, anaamini amekuwa mwanafunzi mzuri katika kutambua matatizo yanayoikabili nchi nzima na hususan na jimbo la Kinondoni.

`kwa kuzingatia uzoefu wangu ndani ya jamii ya kitanzania na baada ya kufikiria ni jinsi gani nitaweza kutumia akili, elimu yangu, uwezo, busara na vipaji vingi nilivyojaliwa na Mwenyezi Mungu na nafasi yangu katika jamii, hatimaye nikafikia uamuzi wa kujitosa kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hii.

`nimejifanyia tathmini ya kutosha, nimejiuliza maswali mengi na kutaka ushauri kutoka kwa viongozi wa chama, familia yangu, marafiki, na wanachama wenzangu. Nimefarijika kwa namna ya pekee walivyonihamasisha kutoka pande zote na ndiyo sababu ya kupata ujasiri wa kujitokeza na kuomba kuteuliwa ili nitimize azma yangu` alisema Shy-Rose.

Shy-Rose amesema ana kila sifa ya kujitosa na kuchaguliwa katika nafasi hiyo kwani yeye amekulia kwenye chama tangu akiwa kwenye Umoja wa Vijana wa CCM sehemu ambayo ni tanuri la kupika vijana kushika nafasi za uongozi na hatimaye kuiingia kwenye chama na viungo vyake.

`Mkiangalia CV yangu mtaona kwamba nimekulia kwenye chama, sijapitia tu kwenye chama, nimetokea ndani ya UVCCM, nimezunguka na viongozi mbalimbali wa chama na serikali nchi nzima na nimejifunza masuala mengi sana ya kutumikia jamii, na jinsi sera na ilani ya chama changu inavyofanya kazi zake za kila siku katika kutumikia wananchi.`, aliongeza.

Shy-Rose amesema sababu ingine iliyompa ujasiri wa kujitokeza katika nafasi hiyo ni kutokana na kauli mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi akiwemo Rais Jakaya Kikwete, za kuwataka wanawake kujitokeza katika kuwania nafasi za uongozi ili Tanzania iweze kufikia hatua ya kuwa na wabunge asilimia 50 wakiwa ni wanawake.

` kwa makusudi kabisa nimeamua kujitokeza kujitosa kwenye jimbo nikiamini kwamba ninaweza…iwapo nitashinda nitakuwa ni mfano mzuri kwa vijana wenzangu ambao wanapenda siasa lakini wametawaliwa na uoga wa kuingia hasa kwenye majimbo…kwangu mimi nataka niwe mfano wa kuigwa na kuhamasisha wanawake hasa wanawake vijana kuingia kwenye majimbo. Iwapo nitashinda basi mwaka 2015 vijana wengi zaidi watajitokeza kuingia majimboni tofauti na hivi sasa mwamko wao ni mdogo`. Alisema Shy-Rose ambaye kwa hivi sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Benki ya NMB Tanzania.

`kwa kuzingatia yote haya, nina kila sababu ya kuamini kwamba nina sifa za kutosha za kuteuliwa katika nafasi ya ubunge kwa jimbo la Kinondoni hasa kwa sera ya chama chetu ya kutaka kuwezesha wanawake kuingia katika nafasi za kutoa maamuzi (decision making bodies). Naamini kwamba iwapo chama kitanipitisha na hatimaye kushinda katika uchaguzi mkuu nitaweza pasipo shaka kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo makubwa ya kutatua kero za wananchi katika jimbo hili.

Tuesday, July 6, 2010

VIJANA JAZZ WAENDELEA KUTUMBUIZA KIINGILIO KINYWAJI CHAKO


Waimbaji Athumani Kambi na Ismail aholeke
Wanamziki wa bendi ya vijana jazz wakitumbuiza wakati wa onesho lao mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa vijana kinondoni kushoto ni mwimbaji Ismail aholeke na Shomari Ally
Wanamziki wa bendi ya vijana jazi wakikunguta magitaa wakati wa onesho lao kushoto ni Shomari Ally na SAid Kizunga

RAIS KARUME ATEMBELEWA NA MWAKILISHI WA UN NCHINI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania,Alberic Kacou,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.Picha na Ramadhan Othman Ikulu,Zanzibar.

ZANZIBAR MORDEN TAARAB YAJIPANGA UPYAA


waimbaji wa zanzibar morden taarabu wakitoa burudan wakati wa onesho lao kushoto ni Mwanamkuu Zayumba na Pilli Saidi
Mwimbaji wa kundi la taarabu la Zanzibar morden, Salma Khasimu akimba wakati wa onesho la kundi hilo lililofanyika katika ukumbi wa mango garden kinondoni Dar es salaam

ZAIN YATOA MSADA WA MADAWATI 100 KWA SHULE YA MSINGI KASULU ILALA DAR ES SALAAM


MBUNGE WA ILALA MH. ZUNGU
Baadhi ya wanafunzi wakishusha madawati
Meneja wa Huduma za Jamii wa Kampuni ya simu ya Zain Bi.Tunu Kavishe (kulia) akimkabidhi madawati mwalimu mkuu wa shule ya Kasulu iliyopo Ilala Dar es salaam, Bi. Moshi Mikidadi, hafla ya makabidhiano hayo ya madawati 100 yenye thamani ya milion saba ilifanyika shuleni hapo jana

EXTRA BONGO YAENDELEA KULISHIKA JIJI LA DAR ES SALAAM


Mpigaji wa bess wa bendi hiyo Alfan Kamodee na mpiga ngoma wakitoa burudan wakati wa onesho lao
Wasanii wa bendi ya Extra bongo wakiwajibika wakati wa onesho lao kushoto ni Salum Issa 'chakuku' na mwimbaji Rashidi Mwezingo 'Silver Boy
Wanenguaji wa bendi ya extra bongo wakiwajibika wakati wa onesho lao
Waimbaji wa Bendi ya Extra bongo, Atanas Montanabe (kushoto) na Ally Choki wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa mango garden juzi

Sunday, July 4, 2010

NCCR MAGEUZI WATANGAZA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR


Mgombea urais kupitia tiketi ya chama cha NCCR MAGEUZI ZANZIBAR Bw. Haji Ambar Khamis

Hamisi Dambaya wa Mlimani tv akizungumza na viongozi wa NCCR MAGEUZI
Katibu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi wa NCCR Mageuzi. Bw,Faustin Sungura (kulia) akimkabidhi fomu Mgombea Urais kupitia chama hicho Bw. Haji Ambar Khamis Dar es salaam jana katikati ni Katibu wa Idara ya Itikadi na Mafunzo Bw, George Kahangwa

VODA COM YAMPONGEZA MISS KINONDONI


Afisa udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahimu Kaude akimpa mkono wa hongera Miss kinondoni Alice Lushiku baada ya kuibuka kuwa mshindi wa shindano hilo,Vodacom ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania

Saturday, July 3, 2010

MISS UTALII WATOA ELIMU WA ZAO LA MLONGE


Mrembo wa utalii wa mkoa wa Dar es Salaam, Sophia Dio, akimwelekeza mteja jinsi ya kutumia dawa iliyotengenezwa kwa mitishamba, wakati wa maonyesho ya 34 ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini.
Kutoka (kushoto) ni Edina Andrew, Latifah Bakari na Pendo Ernest wakiwa katika banda jingine la vitu asilia wakipanga na kusubiri wateja.

Warembo Marry Nguma (kulia) na Grace Lucas, wanaotarajia kushiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Utalii wa Taifa wa mwaka 2010-2011, wakiwa katika Banda la kuuza vipodozi na dawa, wakitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda hilo la Makai Moringa (Mlonge). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya Makai Moringa Enterprises, Eileen Kasubi

MKE WA RAIS ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA


Mke wa rais, Mama Salma Kikwete, akisikiliza maelezo ya Mjasiliamali, Zaida Issa wa Kampuni ya Fatma Mkangara wa Tawi la Buguruni, wakati Mama Salma alipotembelea kwenye banda la Pride katika maonyesho hayo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...