Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 3, 2010

IRENE UWOYA AOMBA WASANII WACHANGA WAJITOKEZE




IRENE UWOYA



IRENE UWOYA


MCHEZA filamu wakike maarufu nchini Irene Uwoya, amesema kwasasa inabidi wasanii wachanga wajitokeze kurithi mikoba yao ambao kwasasa ni maarufu Afrika nzima.

Akizungumza na jarida hili Irene alisema, kutokana wao kutingwa na majukumu inabidi wasanii wachanga wajitokeze waweze kurihi mikoba yao kwani kwasasa wanashindwa kujikita moja kwa moja katika fani ili kuweza kuhudumia familia zao.

Alisema ukiangalia wacheza filamu wengi kwasasa wanamajukumu ikiwa wengine wameolewa na wengine kuwa na watoto pamoja na kuwaza maisha zaidi kuliko umaarufu.

"Iwapo watajitokeza wachanga ni lazima watajikita zaidi katika fani kwani ukiwa ndio unaibukia unakuta uanatamani umaarufu jambo ambalo hujikuta wanafanya kazi zao kwa kujituma zaidi tofauti na sisi," alisema Irene.

Alisema kwasasa wao wamekuwa wakisubiria kushirikishwa zaidi badala ya kutunga kama awali livyokuwa wakati wanautafuta umaarufu, pia hata katika hafla mbalimbali weanashindwa kuhudhuria kutokana na majukumu yao ya kila siku.

Irene alisema yeye yupo tayari kuwapa mbinu zote za ucheza filamu pamoja na kuutafuta umaarufu kwa mtu ambaye atataka kufanya hivyo, ikiwa ni njia mojawapo ya kuinua vipaji vya watanzania.

Irene ambaye kwasasa ni mke wa ndoa wa mcheza soka kutoka nchini Kongo Ndikumana, bado anaaendelea kucheza filamu pamoja na kushirikishwa katika shuting mbalimbali za wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini huku akihudumia familia yake ambapo mpaka sasa ameshacheza filamu nyingi pamoja na shuting ya muziki wa tax bubu wa msanii Matonya.

VODA COM KUTOA MAGARI 100 KWA WATEJA WAKE


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Francois Swart (kulia) , na Miss Vodacom Tanzania 2009, Miriam Gerald wakiwa wameshika moja ya mabango kuashiria uzinduzi wa promosheni mpya ya ‘Chizika na Mkoko’ ambapo mteja atajishindia kila siku gari jipya aina ya Hundai i10 yenye thamani ya sh. Milioni 12 kwa kutuma ujumbe wa Mkoko kwenda namba 15544. Hafla hiyo ilifanyika Mlimani City, Dar es Salaam. Magari 100 yatashindaniwa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa KAMPUNI HIYO, Ephraim Mafuru.


KAMPUNI pendwa ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kuanzia Agosti 2 mwaka huu imepanga kuwazawadia wateja wake gari moja aina ya Hyundai i10 kila siku katika promosheni itakayochukua siku 100 (takribani miezi mitatu) baada ya uzinduzi wa kihistoria unaofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Promosheni hiyo itakayofahamika kama ‘Chizika na Mkoko’ ni moja kati ya shughuli zitakazoambatana na maadhimisho ya miaka kumi ya utoaji huduma wa Vodacom Tanzania nchini. Mpaka promosheni hiyo itakapokamilika tayari magari 100 ambayo kila moja litakuwa na thamani ya milioni 12/- yatakuwa yameshatolewa.

Akizungumzia kuhusiana na promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema shindano hilo litawahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini na kwamba kila siku mtu atakuwa anajipatia gari moja.

“Katika kusherehekea maadhimisho haya ya utoaji huduma zenye mafanikio kwa wateja wetu na jamii kwa ujumla, tumeona tutumie fursa hii kumbukumbu ya miaka kumi ya utendaji wa Vodacom Tanzania kwa kurudisha faida iliyopatikana kwa wateja wetu,” alisema Mafuru.

Aidha aliongeza kwamba washindi katika promosheni hiyo watapatikana baada ya kuwa na pointi nyingi watakazojikusanyia ambazo zitachezeshwa kwenye droo ili kumpata mshindi wa promosheni hiyo kila itakapochezeshwa.

Ili kushiriki kwenye promosheni hiyo Mafuru alisema, washiriki wote watatakiwa kujiunga kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15544 kwa gharama ya shilingi 550 itakayotoa nafasi kwa wateja wa kampuni hiyo kujishindia kila siku Hyundai i10 zitakazotolewa kwa siku 100 mfululizo.

Mbali na hilo promosheni hiyo pia itaenda sanjari na washiriki kuulizwa maswali ya ziada watakayohitajika kuyajibu ili na kupata ambapo kila swali sahihi litakuwa na pointi 20 kama zinazotolewa kwa washiriki watakaokuwa wakijiunga kila siku. Pointi hizo zitahesabiwa kadri zinavyoongezeka.

Idadi ya pointi atakazokuwa nazo mshiriki zitawakilisha idadi ya siku ambazo mteja ameshiriki kwenye droo hiyo. Aidha kila SMS mtu atakayoituma itamuongezea idadi ya pointi kwa siku husika na si vinginevyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru, ni kwamba kadri mshiriki atakavyojikusanyia pointi nyingi ndivyo atakuwa na nafasi kubwa ya kujishindia gari kwenye promosheni hiyo kadri itakavyokuwa ikiendeshwa.

“Kama itatokea mshiriki ama mshindi anajitoa ama kujitoa au asiyetaka kujipatia zawadi, itatulazimu kutomtangaza ama kumtaja,” alisema Mafuru.

Hyundai i10 ni gari inayohimili mazingira ya mijini (hatchback) ambayo imetengenezwa na Kampuni ya magari ya Hyundai Motor Company, na lilizinduliwa rasmi nchini Oktoba 31, mwaka 2007.

Gari hiyo ya gharama nafuu ni rahisi kuihudumia kwani inatumia kiwango kidogo cha mafuta ikiwa pia tofauti na magari mengine ambayo unapoyatumia unajisikia raha na kukuweka huru.

SIKINDE WAENDELEA KUTUMBUIZA KATIKA UKUMBI WA DDC KARIAKOOO



KASEJA CHUJI WARUDISHWA STARS


KOCHA MPYA WA STARS, JAN PAULSEN MWENYE FULANA NYEUSI AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO, KULIA NI RAIS WA TFF, LEODGER TENGA

MGOMBEA URAIS ACHIWA BAADA YA KULIPA DENI LA MILIONI 9.6


Mchungaji Christopher Mtikila
Mgombea Urais kwa tiketi ya DP, Mchungaji Christopher Mtikila akitoka katika mahakama ya Ilala, Dar es Salaam leo. Mtikila ambaye aliukumiwa na Mahakama ya Ilala kwenda kutumikia kifungo cha miezi sita jela baada ya kushindwa kulipa deni la sh. milioni tisa jana na kuachiwa leo baada ya kulipa deni hilo

Kida Waziri Juma Karudi tena Uwanjani


Ni mmoja ya wanamziki wanawake wachache sana ! ambao wamezaliwa na vipaji mwanadada Kida Waziri,
maarufu kama "Stone Lady" ambaye ana sauti ya kumtoa nyoka pangoni!.
Mwanamziki Kida Waziri ni mjukuu wa Mshairi maarufu barani Afrika marehem Shaban Robert,pia ni mtoto aliyekuwa mwanadiplomasia miaka ya 70s na 80s balozi Bw.Waziri Juma.
Habari za uhakika zinasema kuwa Dada Kida Waziri karudi umpya katika ulimwengu wa mziki baada ya kumpumzika kwa miaka,Mwanamziki Kida Waziri "Stone Lady" ambae amerudi na Album ya nyimbo 6,ambayo inamziki uliojaa mdundo na sauti ambayo ni almasi tupu.....
Labda ungependa kuwa moja ya wadhamini ,au Kufanya Kazi na mwanamziki huyo Kida "Stone Lady" Waziri.
Mwanadada huyo yupo tayari kupiga Tour ya ndani na nje ya Tanzania
anapatikana kwa simu namba 0754697114 ukipiga nje ya Bongo Tel. + 255(0)754697114

Monday, August 2, 2010

HUSEN JUMBE MZEE WA DODO AIBUKIA SIKINDE


HUSEN JUMBE MZEE WA DODO

Husein Jumbe mzee wa Dodo akimba sambamba na Abdallah Hemba

MGOMBEA URAIS WA TANZANIA JERA MIEZI SITA KWA DENI LA MILIONI 9


Mgombea Urais kwa tiketi ya DP, Mchungaji Christopher Mtikila akiWA KATIKA DIFENDA YA POLISI KWA AJILI YA KUELEKEA Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar es Salaam leo. Mtikila amehukumiwa na Mahakama ya Ilala kwenda kutumikia kifungo cha miezi sita jela baada ya kushindwa kulipa deni la sh. milioni tisa


Mgombea Urais kwa tiketi ya DP, Mchungaji Christopher Mtikila akipelekwa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar es Salaam leo. Mtikila amehukumiwa na Mahakama ya Ilala kwenda kutumikia kifungo cha miezi sita jela baada ya kushindwa kulipa deni la sh. milioni tisa

NGUMI BINGWA WA MABIGWA WAPIGANA LEO KATIKA UKUMBI WA DDC KEKO


bondia Bondia Sunday Elias akipigana na Ibrahimu Abdaah wakati wa mashindano za bingwa wa mabingwa zalizofanzika jana kwa ajiri za kutafuta wawakilishi wa Tanyania katika michuano za EAST AFRIKA
kocha wa timu za magereya Kameda Antoni akimwekeya bondia wake
Bondia Bondia Sundaz Elias akipigana na Ibrahimu Abdaah wakati wa mashindano za bingwa wa mabingwa zalizofanzika jana kwa ajiri za kutafuta wawakilishi wa Tanyania katika michuano za EAST AFRIKA kushoto akipigana na Rashidi Kimela wakati wa mashindano za bingwa wa mabingwa zalizofanzika jana kwa ajiri za kutafuta wawakilishi wa Tanyania katika michuano za EAST AFRIKA
Bondia sundaz Elia akingia uwanjani

PATRICK PHIRI AWASILI KWA MATUMAINI KIBAO KWA SIMBA


KOCHA AKIONGEA NA WANA HABARI BAADA ZA KUWASILI LEO


Kocha Mkuu wa Timu ya Simba ya Dar es Salaam, Patrick Phiri akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo akitokea kwao Zambia alikokuwa mapumziko. Kulia ni Msemaji wa klabu hiyo, Cliford Ndimbo. Baadhi ya wanachama wa Simba walipoteza matumaini ya kumpata kocha huyo baada ya kuchelewa kwa zaidi ya wiki tatu.ambapo anaungana na kambi za simba ilizopo yanyibar moja kwa moja

Shamba la Bibi latua na Stahili za Ngosha Mosha na Mbasha Wasome Wameahaishwa vipi !!!




Ni kava la kitabu kipya cha katuni kilichochorwa na Bashir Adams
'Mors'. Kimetolewa na kusambazwa na Bantu Entertainment Ltd. chini ya
mkurugenzi wake Marco Tibasima. Kitapatikana mitaani kuanzia Jumatatu
tarehe 2 Agosti, 2010 kwa bei ya tsh. 3000/- tu. Kwa maelezo zaidi jinsi
ya kukipata 0765927833.


Marco Tibasima
Artist/Graphic Designer
PO Box 9974
Dar es Salaam, Tanzania
tel: +255 754 308221 (in Tanzania)
tel: +256 756 417507 (in Uganda)
webpage: www.raisingvoices.org/marco.php

Wasifu wa Mchoraji wa Shamba la Pesa
Bashir Adams a.k.a Mors alizaliwa mwaka 1985 huko Ngarenaro, jijini
Arusha. Alianza elimu ya msingi Ngarenaro Shule ya Msingi Mwaka 1994 hadi
mwaka 2000. Elimu ya sekondari alisoma Kaloleni Shule ya Sekondari kuanzia
mwaka 2001 hadi 2003, kisha akamalizia Temboni Shule ya Sekondari ya
jijini Dar es Salaam mnamo mwaka 2005.

Alianza kupenda uchoraji alipokuwa na miaka minne tu baada ya kumwona
kijana mmoja wa rika lake waliyeishi naye mtaa mmoja aliyeitwa Yassini
akichora picha mbalimbali zilizomvutia. Pia alipata hamasa kutoka kwa dada
yake aitwaye Hidaya Adams ambaye Bashir anakiri alikuwa akichora picha
ambazo zilimpa hamu ya yeye kujifunza pia. Bashir aliweza kwa nyakati
tofauti kuwakilisha shule yake ya Ngarenaro kwenye mashindano mbalimbali
ya uchoraji Mkoani Arusha na kushinda zawadi kadhaa.

Kazi zake zilianza kuonekana rasmi kwenye jarida la Bantu mwaka 2007 na
baadaye gazeti la Ambha.

SHAMBA LA PESA ni kitabu chake cha kwanza na anatarajia kuendelea kutoa
mfululizo wa mikasa hii ya Ngosha, Mosha na Mbasha.

Hakusita kuwashukuru wafuatao katika safari yake ya kufikia mafanikio haya
ambao ni: Marco Tibasima wa Bantu Entertainment Ltd, Nicolaus Munga
‘Nicoman’ wa Arusha, Karim Swago ‘Kakakeri’, Abubakary Mustapha ‘Mandelaa’
na Abedi K. Kimolo wa Ngarenaro, Arusha na Francis John wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.

Anapatikana kwa simu: 0754 546964 / 0658 546964.
Baruapepe: mossadam@yahoo.com

Goldstar YATOA WASHINDI WA 'JISHINDIE MAPESA'


mwali ibrahimu akichanganya namba ili apate mshindi

amina athumani



Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Goldstar Bw. Kulathu Srinivasan (kushoto) akielekeza mchakato mzima wa promosheni ya 'JIshindie Mapesa na Goldstar' iliyofanyika Dar es salaam jana kulia ni Msimamizi kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw, Humudi Abdulhusssein


Msimamizi kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw, Humudi Abdulhusssein (kushoto) akiakiki namba za washindi waliochaguliwa katika droo ya promosheni ya jishindie mapesa na Gold Star iliyofanyika Dar es salaam jana kulia ni Msimamidhi wa Fedha wa kampuni hiyo Bw. Raj Thkur na msimamizi wa shughuli za kampuni hiyo kutoka SCANAD Bw. Ramadhan Omar

NGUMI ZAENDELEA KUPANDA CHATI NCHINI





NGUMI ZA KULIPWA ZALETA MSISIMKO KATIKA UKUMBI WA DDC KARIAKOO

Sunday, August 1, 2010

FAINAL ZA MCHEZO WA POOL ZINAZODHAMINIWA NA BIA YA SAFARI KUFANYIKA TEMEKE LEO



Mchezaji wa pool wa timu ya village Amiri Ngayana ya kurasini akipiga mpira wakati wa mashindano ya mchezo huo kuelekea fainali katika mkoa wa Temeke Dar es salaam juzi mashindando hayo yanadhaminiwa na bia ya safari

Mchezaji wa pool wa timu ya Chipolopolo Baraka Mohamed ya kurasini akipiga mpira wakati wa mashindano ya mchezo huo kuelekea fainali katika mkoa wa Temeke Dar es salaam juzi mashindando hayo yanadhaminiwa na bia ya safari
jamaa akijinyakulia t shet ya SAfari
Mshereshaji wa michezo na burudan akiuliza maswali

SHULE ZA MSINGI ZAENDELEA KUTAABIKA WABUNGE WAKIMBIRIA KUOMBA KULA KWA WANANCHI


Wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi Mtoni Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika masomo yao ya kila siku nje ya madarasani chini miti wakati wakifundishwa na mwalimu wao leo mchana.

Walimu wa shule hiyo baada ya kuona kamera ya Sufianimafoto ikiwa kazini walijitetea kuwa wameamua kuwakusanya wanafunzi hao wa mikondo minne na kuwafundisha kwa pamoja, ili waweze kuelewa kwa pamoja kuelekea kujiandaa na mitihani ya darasa la saba ya mwaka huu. Lakini cha kushangaza ni kwamba kama hivyo ndivyo imekuwaje wanafunzi hao wote wafundishwe na mwalimu mmoja je wataweza kuelewa na lengo lao litatimia kweli?
Wanafunzi hao wakiendelea kufundishwa na hapa wamepigwa kwa nyuma ili kuonyesha uhalisia wa mahala penyewe na uwingi wao ambao bado wamekatwa kulingana na kamera kwa kweli ni wengi mno.Picha na hisani ya www.sufianimafoto.blogspot.com

WAZANZIBAR WAPIGA KULA YA MAONI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid
Karume,akitumbukiza kura yake,katika kituo cha kupigia kura ya Maoni, ya kuwezesha Uundwaji Serikali ya Kitaifa ya Zanzibar,katika Skuli ya Msingi ya Kiembesamaki Wilaya Magharibi jana,Uundwaji wa Serikali hiyo ya Kitaifa ni baada ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Octoba mwaka 2010.
Dk. Gharib Bilali, akitoka kwenye Chumba cha kupigia kura ya Maoni katika Kituo cha Shule ya Msingi, Kiembe Samaki mjini Zanzibar lemchana. ambapo vituo vingi wamekuwa wakijitokeza wananchi mmoja mmoja na kupiga kura na kisha kuondoaka kwa usalama tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kwamba huenda ingezuka vurugu kutokana na baadhi ya watu kuipinga hoja hiyo ya kura ya maoni ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Ama kwa hakika Wakazi wa Visiwa vya Zanzibar wameitikia wito na kuipokea kwa mikoni miwili hoja hiyo n kuifanyika kazi ili kuweza kuleta mabadiliko visiwani humo.
Mwandishi wa habari wa Televisheni ya Chanel Ten Munir akipiga kura ya Maoni. NA SUFIANIMAFOTO BLOGSPOT

MDHAMINI MKUU WA YANGA MANJI AKABIDHI LIPOTI YA UDHAMINI


Yusufu Manji akimkabidhi ripoti ya udhamini makamu mwenyiki wa yanga davis mosha
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...