Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 1, 2010

SHULE ZA MSINGI ZAENDELEA KUTAABIKA WABUNGE WAKIMBIRIA KUOMBA KULA KWA WANANCHI


Wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi Mtoni Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika masomo yao ya kila siku nje ya madarasani chini miti wakati wakifundishwa na mwalimu wao leo mchana.

Walimu wa shule hiyo baada ya kuona kamera ya Sufianimafoto ikiwa kazini walijitetea kuwa wameamua kuwakusanya wanafunzi hao wa mikondo minne na kuwafundisha kwa pamoja, ili waweze kuelewa kwa pamoja kuelekea kujiandaa na mitihani ya darasa la saba ya mwaka huu. Lakini cha kushangaza ni kwamba kama hivyo ndivyo imekuwaje wanafunzi hao wote wafundishwe na mwalimu mmoja je wataweza kuelewa na lengo lao litatimia kweli?
Wanafunzi hao wakiendelea kufundishwa na hapa wamepigwa kwa nyuma ili kuonyesha uhalisia wa mahala penyewe na uwingi wao ambao bado wamekatwa kulingana na kamera kwa kweli ni wengi mno.Picha na hisani ya www.sufianimafoto.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...