Marquee
tangazo
Friday, August 13, 2010
VODA COM YATOA VIFAA KWA LIGI KUU
Vodacom Tanzania leo imekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 290 kwa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa mwaka 2010 -2011,akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo, Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehebuza alisema ni matumaini ya Vodacom kwamba vifaa hivyo vitakuwa kichocheo cha kuinua kiwango cha soka nchini.Alisema huu ni msimu wa tisa tangu Vodacom ianze kudhamini ligi hiyo na kwamba Vodacom inafarijika kuona kiwango cha soka kikipanda.Mbali na kukabidhi zawadi hizo, alivishauri vilabu kutafuta njia nyingine za kuongeza mapato ikiwamo kutafuta wadhamini wengine ili kukabiliana na kupanda mara kwa mara kwa gharama za uendeshaji wa vilabu.Alisema msimu huu Vodacom imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kudhamini ligi hiyo, alisema kati ya fedha hizo milioni 667 zimetengwa kwa shughuli za uendeshaji wa lihi ikiwemo nauli za timu pamoja na gharama nyingine kama posho za marefa.Rwehumbiza alisema msimu huu vifaa vimeboreshwa zaidi na kuvitaka vilabu kuvitumia vifaa kuboresha ligi, aidha alivipongeza vilabu vya simba na yanga kwa kufanya vizuri msimu uliopita na kuvitakia kila la kheri katika msimu huu.Aidha mdhamini huyo alitoa rai kwa vilanu kuvitumia vifaa hivyo kama changamoto ya kufanya vizuri katika Ligi ya Vodacom msimu wa mwaka 2010 hadi 2011 na hivyo kumpata mwakilishi bora katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment