Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 1, 2010

WAZANZIBAR WAPIGA KULA YA MAONI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid
Karume,akitumbukiza kura yake,katika kituo cha kupigia kura ya Maoni, ya kuwezesha Uundwaji Serikali ya Kitaifa ya Zanzibar,katika Skuli ya Msingi ya Kiembesamaki Wilaya Magharibi jana,Uundwaji wa Serikali hiyo ya Kitaifa ni baada ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Octoba mwaka 2010.
Dk. Gharib Bilali, akitoka kwenye Chumba cha kupigia kura ya Maoni katika Kituo cha Shule ya Msingi, Kiembe Samaki mjini Zanzibar lemchana. ambapo vituo vingi wamekuwa wakijitokeza wananchi mmoja mmoja na kupiga kura na kisha kuondoaka kwa usalama tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kwamba huenda ingezuka vurugu kutokana na baadhi ya watu kuipinga hoja hiyo ya kura ya maoni ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Ama kwa hakika Wakazi wa Visiwa vya Zanzibar wameitikia wito na kuipokea kwa mikoni miwili hoja hiyo n kuifanyika kazi ili kuweza kuleta mabadiliko visiwani humo.
Mwandishi wa habari wa Televisheni ya Chanel Ten Munir akipiga kura ya Maoni. NA SUFIANIMAFOTO BLOGSPOT

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...