Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 31, 2011

PAMBANO LA KIMATAIFA LA NGUMI KUPIGWA TANZANIA…!!!


Bondia wa kumi nchini Tanzania Fransic Cheka akizungumza wa waandisha wa habari wakati wa kutambulisha mpambano wake wa kimataifa utakao pigwa Dar es Salaam 1/5/2011 kushoto ni Mratibu wa pambano hilo Shomari Kimbau




Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Aurora Shomari Kimbau (kushoto) akizungumzia kuhusu pambano la Kimataifa la ngumi baina ya Mtanzania Francis Cheka na Mmarekani Marcus Upshaw litakalofanyika Tarehe 1st,May, 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall jijini Dar es Salaam. Kulia ni Sales & Marketing Haris Omary.

BENKI YA POSTA YAZINDUA EASTER KAMPENI….!!!




Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Posta Bw. Andrew Chimanzi (kulia) akizindua Easter Kampeni ya kutoa huduma za Benki ya Posta ambazo zitawezesha wateja wa Benki hiyo kupata huduma kwa urahisi katika kipindi hicho cha sikukuu za Pasaka.Kushoto ni Meneja Mkuu wa Huduma za Mauzo na Wateja Bi. Grace Nkuzi

TBL yasaidia ukarabati wa jengo la UMIVITA






Meneja Mahusiano wa TBL,Edith Mushi (pili kushoto) akipeana mkono na Afisa Uhusiano wa UMIVITA,Tungi Mwanjala (tatu kulia) wakati wakati wa kukabidhi msaada wa Shilingi 2.5 Mil, kwa ajili ya ukarabati wa jengo la ofisi ya Chama cha Umoja wa Miradi ya Viziwi Tanzania (UMIVITA) iliyopo ndani ya Shule ya Viziwi Buguruni leo.wengine pichani ni Mkurugenzi wa Chama cha Kuhudumia Viziwi Tanzania,Matirda Ngonyani (kulia),Katibu Mtendaji,Rahim Othman pamoja na Judith Robert kutoka chama cha kusaidia Viziwi la TANZANEAR.

jengo linalotakiwa kufanyiwa ukarabati kwa msaada wa TBL

HAPPY BIRTHDAY SOPHIA ASHERY










LEO ni siku yangu ya kuzaliwa na ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kunipa pumzi na kuniongoza katika maisha yangu. Asanteni marafiki zangu wote ambao mmekuwa sehemu ya maisha yangu.

Wednesday, March 30, 2011

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA ATEMBELEA KAMPUNI YA ZANTEL


ofisa Mkuu wa Tekenorojia Kampuni ya Zantel Bw. Moncef Mettiji wa pili (kulia) akimuonesha moja ya mitambo ya mawasiliano ya Kampuni hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Bw. Charles Kitwanga alipotembelea kampuni hiyo Dar es salaam leo kuliani, Ofisa Mtendaji Mkuu Ali Bin Jarsh na kushoto ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa wa Zantel, Norman Moyo

Happy birthday uniqueentertz.blogspot.com

Am Magese,nawashukuru watizamaji wote kwa kunipa kampani yakutosha kwa mwaka mmoja uliopita pia mwenyezi mungu kunipa nguvu na uhai wakuwapa mavituz ya ukweli,taerhe 1 april tunatimiza mwaka mmoja. www.uniqueentertz.blogspot.com

ILALA WAENDELEA NA MCHAKATO WA KUTEUA TIMU YA WILAYA KATIKA MASHINDANO YA UMISETA


Mshambuliaji wa timu ya Kundi B, Dafroza Steven, akijaribu kumtoka beki wa timu ya kundi D, Halima Faustine, wakati wa mchezo wa mashindano ya Umiseta yanayoendelea katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa wasichana wa Shule za Sekondari za Wilaya ya Ilala. Michezo hiyo ni maalum kwa ajili ya kuteuwa wachezaji watakaounda kikosi cha timu ya Ilala itakayochuana na timu ya Ukonga katika michuano hiyo ya Umiseta.
http://sufianimafoto.blogspot.com/

*MATEMBEZI YA MAJI 'TIGO WALK FOR WATER' KUFANYIKA APRIL 16 MLIMANI CITY DAR



Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya ‘Spearhead Africa Ltd’, Bertha Ikua, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu matembezi ya Maji ‘Tigo Walk For Water 2011’ zinazotarajia kufanyika Aprili 16 mwaka huu katika Viwanja vya Mlimani City kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia miradi ya maji na juhudi za wazalendo kutatua janga la maji linalowakabili wakazi wa Bagamoyo, Katikati ni Ofia Uhusiano wa Kampuni ya simu za Mkononi Tigo ambao ni wadhamini wakuu, Jackson Mmbando na Msemaji wa Tigo wa Walk For Water, Jakate Mwegelo.


*****************

WALK FOR WATER 2011- MWAKA WA PILI WA JUHUDI ZA WAZALENDO KUTATUA JANGA LA MAJI LINALOWAKABILI TAKRIBAN WAKAZI 100,000 WA BAGAMOYO.

Baada ya mafanikio makubwa ya Dow Live Earth Run for Water 2010- sehemu ya mradi wa kimataifa wa kutatua tatizo la janga la ukosefu wa maji ulimwenguni kote, kampuni ya simu za mkononi tiGo Tanzania pamoja na Spearhead Africa Limited inaamini kwamba mwamko huu upewe kipaumbele kwa kuzingatia kwamba janga hili la ukosefu wa maji bado halijatokomezwa. Huu ni mwaka wa pili kwa shughuli hii ya uchangajishaji fedha kuendeshwa nchini na kampuni ya Spearhead.


Lengo la shughuli hii kwa mwaka huu ni kuchimba visima vyenye urefu wa mita 200 na 100 ili kutoa ufumbuzi kwa zaidi ya wakazi 100,000 waishio Bagamoyo ambao hawana uwezo wa kupata maji safi na salama.


Mwaka huu kampuni ya simu za mkononi ya tiGo imejitolea kusimamia shughuli nzima ya Walk for Water na kampuni ya Spearhead na imefurahia mchango huo wenye lengo la kutokomeza janga hili. tiGo Tanzania kama moja ya wadhamini wa Dow Live Earth Run for Water 2010, pamoja na kuona mwamko wa wananchi kujitokeza kwa wingi kutokomeza janga hili, tiGo wameamua kutoa msaada huu kama sehemu ya huduma zao kwa jamii ambayo imewazunguka.


Malengo ya matembezi haya ya hisani ni:


1. Kutaarifu umma na wadau wa maji kuhusu janga la maji na ufumbuzi wa janga hili.


2. Kutoa fursa kwa wadau wote wa maji kutoa elimu ya kutunza maji ,matumizi mazuri ya maji na kutoa taarifa kuwa ni wajibu wa kila mmoja wetu kusaidia kutatua janga hili.


3. Kuhamasisha mashirika kushiriki kwenye mbio/matembezi ya hisani, kuonesha bidhaa au huduma zao na kutoa mchango kwa mradi teule wa naji.


4. Kuchangisha fedha kwa ajili ya mradi endelevu wa maji utakaotoa huduma kwa jamii kwa muda mrefu.


Afisa uhusiano wa Tigo Tanzania, Mr. Jackson Mmbando alisema,” Tunafuraha kuwaletea shughuli hii ya kuchangia mradi wa maji na tunawahamasisha waandaaji wengine kuwa na moyo kama huu. Pia hii sio changamoto tu kwa Bagamoyo bali kwa maeneo yote ya Tanzania. Tunawahimiza wachangiaji na watu binafsi kujisajili na kuchangia mradi huu.


“Kupitia Tigo Walk for Water, tunatarajia kupata fedha taslim shiligi Milioni 60 za Tanzania kwa ajili ya mradi huu, kwa msaada wa Ifakara Health Institute, tumeweza kutambua maeneo ya kuyapa kipaumbele ya kuchimbwa visima vyenye urefu wa mita 200 na 100 ili kuipatia jamii maji salama katika kata za Bagamoyo.”


tiGo Walk for Water itafanyika kwenye uwanja wa maegesho ya magari ya Mlimani City Mall siku ya jumamosi, 16 Aprili 2011. “Tunawashukuru Tigo kwa kutuletea shughuli hii ya kuchanga fedha. Tunategemea wale wote walioshiriki mwaka jana kwenye uwanja wa taifa watatuunga mkono kwa kujisajili kwa matembezi au mbio za kilometa 6, umbali ambao unakadiriwa ni wastani wa umbali wanaotembea wanawake wengi na watoto kila siku kutafuta maji safi ya kunywa.” alisema Bertha Ikua- Meneja Huduma kwa wateja wa Kampuni ya Spearhead Africa.


Mradi wa maji wa Bagamoyo iliyopo chini ya Ifakara Health Institute ndio utakaonufaika na Tigo Walk for Water 2011.


Bertha Ikua aliongezea “Kuna vijiji vingi Bagamoyo ambavyo wananchi wake hawawezi kupata maji safi na salama.Visima vingi ni vifupi na vinakauka wakati wa kiangazi, mito siyo salama na ipo mbali na makazi ya watu, maji ya mvua ni ya msimu na maji ya bomba ni kwa ajili ya watu wachache wenye uwezo wa kulipa bili ya kila mwezi.


Baadhi ya maeneo ambapo kina cha maji ni kirefu, mara nyingi ni rahisi kuchimba visima venye sifa ya ubora kwa gharama nafuu lakini maeneo ambayo kina cha maji ni kifupi tutahitaji kuchimba vissima venye vina virefu zaidi ya mita 100 ili kupata maji.”


Usajili wa mtu binafsi kwa ajili ya matembezi ya maji ni shilingi 3000 na usajili huo utaanza tarehe 28 Machi katika Makao Makuu ya Tigo yaliyopo barabara ya Nyerere na mtaa wa Ohio, Shoppers Plaza Masaki na Mikocheni, City Supermarket iliyopo Harbour view, Shoprite ya barabara ya Pugu, Village Supermarket iliyopo Sea Cliff Village, Novel Idea yiliyopo mtaa wa Ohio, maduka na ofisi zote za hoteli ya Oysterbay pamoja na Mlimani City Mall.


Kampuni mbalimbali, Balozi, mashirika ya serikali na yasiyo ya kiserikali yanahamasishwa kushiriki siku hii kwa kuifanya iwe siku ya pamoja ya wafanyakazi na kujisajili kutembea kwa pamoja kama kampuni au shirika kupitia anuani ya barua pepe kahenga@spearheadafrica.com au kwa kupiga simu 0713 252 254.


Asilimia 50 ya ada ya kujisajili na maonesho na asilimia 100 ya michango yote itapelekwa kwenye mradi wa maji.


Wadhamini wakuu wa tiGo Walk for Water ni Tigo Tanzania, na wadhamini wengine ni Konyagi na AngloGold Ashanti- Geita Gold Mine pamoja na support sponsors wengine, ambao ni: Uhai, Hugo Domingo, Image Masters, Digital, A1 Outdoor, Mlimani City, Ultimate Security, Synovate, Davis & Shirtliff, Africa Beat, Advertising Dar, M2 Advertising na BMTL.


Shughuli hii ya tiGo Walk for Water 2011 imechukua sura tofauti ikilinganishwa na mwaka jana. Mwaka huu kutachezeshwa droo ya bahati na sibu siku hiyo baada ya kukimbia au kutembea. Zawadi zitatolewa kwa washindi baada ya kuchezeshwa droo hiyo kutokana na fomu zao za usajili. Hivyo ukijisajili unapata nafasi ya kuweza kushinda zawadi ambazo zimetolewa na Tigo, Samsung, Ideal Computers, Mr. Price, Little Impression, Movenpick na wengineo.


“Nina ipa moyo familia yangu, marafiki, wanamuziki, wanaminitindo na watu wengine mbalimbali mashunguli pamoja na wenzangu wote kuniunga mkono katika mpango huu. Sote kwa pamoja tutembee na kukimbia ili tusaidie kuweka utofauti kwa namna moja au nyingine katika kubadili hali hii, siyo tu kwa ajili yetu pekee bali pia kwa watoto wetu. Jitokeze leo kujisajili,kuchangia na kufanya maonesho.” Alisema Miss Jokate Mwagelo ambaye ni balozi wa matembezi ya maji ya tiGo 2011.


-MWISHO-


Kuhusu tiGo


tiGo ni kampuni ya kwanza ya simu za mkononi Tanzania, ilianza shughuli zake mwaka 1994,ni mtandao wa gharama nafuu na ubunifu wa hali ya juu kiutendaji.



tiGo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) ,inatoa huduma kwa gharama nafuu na hupatikana kirahisi katika maeneo mengi, pia inaurahisi wa kulipiwa huduma ya kabla kwa wateja wa zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanayoibuka Afrika na Latin America.


Mafanikio ya tiGo yamejikita katika msingi wa mkakati wa “Triple A” ambao unasimama badala ya Affordability, Accessibility na Availability. Tunatengeneza ulimwengu ambao huduma za simu za mkononi unakuwa nafuu na unapatikanaji wake ni rahisi mahali pote na kwa watu wote. Hii inatoa dhamana kwa wateja wetu ambao wanapata huduma bora kwa gharama nafuu katika mikoa yetu yote 26 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

MBUNGE WA JIMBO LA LUDEWA AENDELEA KUTEKELEZA SEHEMU YA AHADI ZAKE

Mbungea wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombee, akijaribu uwasha Trekta, wakati wa hafla fupi ya kukabidhiana iliyofanyika leo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (kushoto) akimkabidhi kadi ya Trecta, mratibu elimu wa kanda ya Lugarawa,Vitaris Haule kwa ajili ya kuwezesha kulima mashamba ya shule ili kutoa chakula mashuleni. Picha na Francis Godwin

Diwani wa kata ya Lugarawa wilaya ya Ludewa mkoani Iringa, Fromena Haule akipokea kombe litakaloshindaniwa katika kata yake katika mashindano ya mbunge Deo Filikunjombe wa jimbo hilo ambapo mshindi atapata kombe hilo la dhahabu na Ng'ombe mashindano kama hayo ni kwa kata zote za jimbo hilo.

BENDI YA MASHUJAA KUTAMBULISHA WAPYA APRIL 1 KIJIJI CHA MAKUMBUSHO


BENDI ya Mashujaa Musica Aprili 1 mwaka huu inatarajia kufanya onyesho la utambulisho wa wanamuziki wake wapya waliojiunga na bendi hiyo wakitokea bendi mbalimbali za nchini na Kinshasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Mgahawa wa Hadees, Meneja wa bendi hiyo, Mujibu Hamis, alisema kuwa maandalizi ya onyesho la utambulisho wa wanamuziki limekamilika kwa asilimia 99 na aslimia moja ikibaki kuwa ni onyesho lenyewe litakalofanyika katika Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho.


Aidha alisema kuwa onyesho hilo ni maalum kwa ajili ya kutambulisha wanamuziki wapya, lakini pia ni maalum kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wa bendi hiyo na kuonyesha kile kilichowafanya kukaa kimya kwa kipindi wakijipanga zaidi.


“Tumejiandaa vilivyo kuwaonyesha mashabiki wa muziki wa dansi ujio mpya wa bendi yetu iliyokuwa kimya kwa ajili ya kujipanga ili kuweza kwenda na wakati katika jukwaa la ushindani la Muziki wa dansi, na pia tumejitahidi kuongeza wanamuziki katika kila idara kuanzia waimbaji hadi wanenguaji ili kuweza kutoa burudani iliyokamilika kwa mashabiki wetu” alisema Mujibu.


Aliwataja wanamuziki hao wapya wanajiunga na bendi hiyo kuwani pamoja na, Kajo anayetoka katika Kundi la Boziboziana, Jimmy Adol kutoka kwa Koffee Olomide, Profa Kariakoo kutoka Kinshasa, Kama Simba Komilion, kutoka kwa Felix Wazekwa.


Wengine ni Rapa mahiri Sauti ya Radi, Kelvin, Salma Shaban ‘Teketeke’ Mariam Lelapel na Corando wote kutoka bendi ya Diamondi Musica.


Katika onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa bendi inayoongozwa na vijana watatu ‘Mapacha 3’, bendi yenye umri wa mwaka mmoja tangu ilipoanzishwa na kuweza kujizolea sifa kem kem baada ya kutwaa Tuzo mbili katika Kili Music Awards 2010, ambazo ni Tuzo ya Wimbo Bora wa bendi wa 2010 pamojana Tuzo ya Rapa bora wa bendi wa mwaka 2010.

Rapa Mahiri wa bendi ya Mashujaa Musica, aliyejiunga na bendi hiyo akitokea bendi ya Diamond Musica, Yanick Noa ‘Sauti ya Radi’ (kulia) akigahan sehemu ya rap zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu onyesho la utambulisho wa wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo, linalotarajia kufanyika April 1 kwenye ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho. Katikati ni Meneja wa bendi hiyo, Mujibu Hamis na Kiongozi wa bendi hiyo, Jado Fidforce pamoja na wanenguaji wa bendi hiyo. ******************************** Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa Musica Salma Shaban ‘Teketeke’ (kulia) na mariam Ramadhan ‘Lelapee’, wakionyesha umahiri wao wa kushambulia jukwaa wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana, kuhusu onyesho la utambulisho wa wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo, linalotarajia kufanyika April 1 kwenye ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho
http://sufianimafoto.blogspot.com/

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO SAYANSI YA TEKNOLOJIA ATEMBELEA KAMPUNI YA AIRTEL



Mkurugenzi wa Kampuni ya Airtel Bw. Sam Elangallooe (katikati) akimwonesha mitambo ya Kampuni hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Bw. Charles Kitwanga kushoto na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Mawasiliano, Eng. Clarence Ichwekeleza walipotembelea Kampuni hiyo Dar es salaam

Sunday, March 27, 2011

DVD YA SUPER D BOXING COACH SASA INAPATIKANA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI




BONDIA wa Zamani na Kocha wa Ngumi wa Klabu ya ngumi ya Ashanti, Rajabu Mhamila'Super D' ameingiza Video inayozungumzia maisha yake ya mchezo huo.Akizungumza Dar es Salaam leo, Super D alisema video hiyo ilikua sokoni kuanzia sasa ikizungumzia maisha yake tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 1984 hadi 2010 sasa.Alisema Video hiyo itaonesha mapambano mbalimbali aliyocheza na dhidi yamabondia Mbwana Matumla, Rashidi Ali na Ajibu Salumu.Alisema lengo la kuandaa video ni kutaka kutimiza malengo yake ya kuendelezamchezo wa ngumi kwa kuwapatia vijana nafasi ya kujifunza kupitia kwake.Alisema kutokana na nchi ya Tanzania kuwana vipaji vingi atashindwa kuwafikiakila mmoja wao na badala yake amewapa fursa ya kujifunza kwa kuangalia video.Alisema Video ya katika kuhaikisha hiyo DVD inafanya vizuri sokoni ameongezeavionjo vingine kutoka kwa mabondia maarufu duniani kama Mike Tyson, Michael Mo,Junior Myweather, Mohamed Ally, Man aqyao na Joe Fleizer ambapo kuanzia sasa ipo mtaani ususani makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Dar es salaam

MATUKIO MBALIMBALI YA TUZO ZA KILI

Mchezaji wa timu ya Simba Juma Kaseja Akimkabidhi tuzo ya nyimbo bora ya mwaka kwa msanii Mzee Yusufu kulia na Shedrak Msajigwa wa Yanga
Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya wakiimba wakati wa onesho la tuzo za muziki nchini zilizoandaliwa na Kampuni ya bia nchini 'TBL' kupitia bia yake ya Kilimanjaro kutoka (kushoto) ni Ali Kiba, Banana Zoro na Nassib Abdul ‘Diamond’
Mashabiki Wakishangilia tuzo hizo
Mussa Hassani Mgosi wa Simba kushoto na Jerson Tegete wa Yanga kulia wakimkabidhi tuzo ya video bora ya mwaka msanii Khalfan Ilunga CPWA
Saidi Mabera akishangilia tuzo hiyo
Saidi Mabera akikunguta gita la Solo wakati wa tuzo hizo
Msanii Cpwaa akitoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki wake walioweza kumpigia kura mpaka kuweza kupata tuzo ya Video Bora ya Muziki ya Mwaka.Cpwaa pia amechukua tuzo nyingine ya Ragga/Dancehall.
Tuzo ya Wimbo Bora wa Reggae ilienda kwa Hardmad.
Mbungu wa Viti Maalum wa CCM,Mh. Vicky Kamata akimkabidhi tuzo ya Wimbo Bora wa R&B msanii Ben Poul.
Msanii wa vichekesho toka kundi la Orijinal Comedy,ambaye pia ni Mwanamuziki akitoa shukrani zake kwa mashabiki wake waliomuwezesha kupata tuzo ya Wimbo Bora wa Asili wa Tanzania.

WAKAZI WA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO WATAKA MKUCHIKA AJIHUZURU KWA KUMUONGOPEA RAIS


Mwanasheria wa Kampuni ya Kibasila Estates Public Limited Dkt. Sengondo Mvungi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa dharula na wateja wake wa Kota za Bandari Gerezani Kariakoo Dar es salaam juzi baada ya taarifa iliyotolewa na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. George Mkuchika kwa rais Jakaya Kikwete alipotembelea ofisini kwake na kusema imeshinda Serekali na wananchi hao wamekata rufaa wakati kesi hiyo imeamliwa iongelewe nje ya mahakama kwanza

TUZO ZA KILI ZAMALIZIKA KWA FURAHA


Mkuu wa Vipindi va EATV , Lydia Igarabuza akimkabidhi tuzo ya heshima kwa mwanamuziki wa dansi nchini Saidi Mabera anaeye shughudia katikati ni Mkuu wa Udhamini Kampuni ya Voda Com George Lweumbiza
Stara Tomasi akitoa burudani
Banana Zoro kushoto na Nassib Abdul ‘Diamond wakishambulia jukwaa

mambo yetu ya kuselebuka

Rabia Bakari akitoa ai
Grecy Michael akiselebuka

Tamasha la Uzalendo lilivyofana


Wanamuziki Hassani Moshi akiwa na Shabani Dede wa band ya Msondongo mawakiimba pamoja katika tamasha la Uzalendo katika viwanja vya Biafra Dar es Salaam.
Mashabiki wakifuatilia tamasha hilo leo licha ya jua kali lililokuwa likiwaka.

Meli ya wanamaji za China yawasili Dar es Salaam


Raia wa nchini China waishio Tanzania wakiwa katika shamrashamra za kuipokea Meli za Kijeshi

MKUU wa msafara wa jeshi la wanamaji kutoka nchini China Zhang Huachen akiwa na Mkuu wa Jeshi la wanamaji la hapa nchini Meja Jenerali Said Shaban Omar mara baada kupokelewa leo (jana) asubuhi katika Bandari ya Dar-Es-Salaam. Wakiwa hapa nchini jeshi hilo la wanamaji kutoka China.

Ziara ya Makamu wa Rais Wilayani Magu


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akikata utepe kufunguwa Shule ya Sekondari Kitumba katika kijiji cka Kisesa Wilayani Magu wakati alipokuwa kwenye mfululizo wa ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Mwanza leo, Makamu wa Rais ameahidi kuchangia jumla ya shilingi milioni tatu kwa ajili ya kuanzisha utengenezaji wa miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua Shuleni hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Kabila Wilayani Magu baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la upasuaji mdogo katika kituo cha Afya Kabila leo, Makamu wa Rais yupo Mkoani Mwanza kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo ya Wananchi.

Pinda azindua Kliniki ya macho KCMC

Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL),Teddy Mapunda akimkaribisha mgeni rasmi,Waziri Mkuu Mh Pinda pamoja na wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa kliniki ya Macho ya KCMC mapema leo asubuhi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Richard Wells baada ya Waziri Mkuu kuzindua Kliniki ya Macho iliyojengwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mjini Moshi katika Hopitali ya KCMC Machi 25,2011.

Friday, March 25, 2011

WAISLAM WAFANYA MAANDAMANO YA KUIPINGA MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE KUISHAMBULIA LIBYA

Isharaa ya Umoja ya kuilinda Nchi ya Libya ikionekana na sura ya Rais Mo'ammar Al-Gaddafi
Baadhi ya Waislam wakiwa katika viwanja vya biafra Kinondoni Dar ES salaam jana kuipinga Marekani na washirika wake kuishambulia Libya
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiandamana kutoka Msikiti wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam jana kwenda viwanja vya Biafra ambako kulikuwa na mkutano wa kulaani mashambulizi ya majeshi ya Marekani na washirika wake dhidi ya Libya

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...