Meneja
wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo katikati akiongea na waandishi wa habari
wakati wa kutangaza washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya VUMBUA HAZINA
CHINI YA KIZIBO inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Mkaguzi kutoka bodi ya taifa ya
bahati nasibu, Bw. Abdallah Hemedi kulia akikagua jinsi droo hiyo inavyochezeshwa.
Kushoto ni meneja wa bia ya Serengeti Bw Allan Chonjo na katikati ni mwakilishi
kutoka PWC Bw.Tumainieli Malisa.
Ni katika droo ya tatu ya promosheni ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL.
Wiki mbili zilizopita zilikuwa za aina
yake baada ya kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kuendelea kukonga nyoyo
za wateja wake na watanzania kwa ujumla kwa kuwapa zawadi washindi wa
promosheni inayoendelea inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya
kizibo’ ambapo watanzania wengi wameshuhudia kampuni hiyo ikiwakabidhi
washindi wa promosheni hiyo zawadi zao katika promosheni hii kubwa.
Amadeus Minja na Agness Msengi wakazi wa
Dar es salaam, walijishindia jenereta (kangavuke) kubwa ambapo
walikabidhiwa zawadi hizo mwisho mwa wiki iliyopita. Ibrahim Kimambo
mkazi wa tabata jijini Dar es salaam alibahatika kujinyakulia pikipiki
mpya na ya kisasa ambapo naye alikabidhiwa zawadi yake mwishoni mwa wiki
iliyopita katika ukumbi unaovuma sana ujulikanao kama Dar LIVE pale
Mbagala Zakhem.
Bw.
Ibrahim ambaye hakuwa na kazi yoyote mpaka bahati iliyobebwa na
promosheni hii ilipomdondokea alikuwa na haya ya kusema, “kwa kweli
nilipopata taarifa ya kushinda zawadi ya pikipiki sikuamini lakini sasa
nimeamini na nawashukuru sana SBL kwa kuwa sasa naweza kujiajiri na
kuendeleza maisha yangu na wale wanaonitegemea”. Kutoka jijini Mwanza
Godfrey Shao ambaye alijinyakulia bajaj ya gurudumu tatu anaendelea
kusubiri taratibu za usajili zikamilike ili aweze kukabidhiwa bajaj
yake.
Asubuhi ya leo droo
ya tatu katika promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’
imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL zilizopo
maeneo ya Oysterbay jijini.
Droo hiyo ya tatu kama ilivyo kawaida
katika droo zilizopita, ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi
kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya
kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH
MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers
kuhakikisha washindi wote watapatikana kihalali.
Kampuni
ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium
Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni nchi nzima
ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’ Na kuleta mabadiliko
yakinifu kwa wateja wake.
Akiongea na waandishi wa habari katika
hafla hiyo, Mkurugenzi wa mawasiliano na mahusiano wa kampuni ya SBL Bi.
Teddy Mapunda, amesema kwamba “mpaka sasa tumeshawapata washindi wawili
wa jenereta ambao tayari tumewakabidhi zawadi zao, wengine ni washindi
wa bajaj moja na wa pikipiki moja ambao nao wameshakabidhiwa zawadi zao”
“Tunawashauri wateja wetu na watanzania
wote wenye sifa za kushiriki katika promosheni hii ya aina yake
waendelee kushiriki bila kukata tamaa na hatimaye nao waweze kushinda
kwani promosheni yetu ni ya kweli na ya uhakika.” alisema Mapunda na
kuongeza kuwa mpaka sasa tayari watu zaidi ya 2000 wamejishindia pesa
taslimu na wakafanikiwa kupata pesa hizo kwa urahisi kabisa kupitia
mtandao wa kutuma na kupokea pesa wa kampuni ya mawasiliano ya simu za
mkononi Vodacom MPESA ndani ya masaa ishirini na nne. Pia, washindi
wamepatikana ambao wamejishindia zawadi za vinywaji vilivyopo katika
promosheni hiyo.
Washindi wetu katika droo ya tatu ni
Fadhili Manzi mkazi wa Mafinga mywaji wa bia ya Serengeti Premium Lager
nambaye amejishindia bajaj na Raymond Denis mkazi wa Iringa ambaye
amejinyakulia jenereta kupitia bia ya Tusker Lager.
MAELEKEZO:
Nunua bia ya Serengeti lager, Tusker
lager au Pilsner Lager fungua kisha angalia chini ya kizibo utapata
namba zilizopo chini ya kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi
kwenye simu yako, nakili namba zilizochanganyika na herufi mfano AB55550, kisha
tuma kwenda namba 15317 na unaweza kujishindia pesa taslimu kati ya
shilingi 10,000, 50,000 au 100,000 au unaweza kujipatia bia ya bure kati
ya bia zilizoainishwa katika promosheni hii . Fanya
hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na magazeti.
Wanaoruhusiwa kushiriki promosheni hii ni walio na umri wa miaka kumi
na nane na kuendelea.
No comments:
Post a Comment