Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 7, 2012

Shirika la Bima la Taifa (NIC) lakabidhi Mifuko 100 ya Saruji kwa Wahanga wa Mafuriko Mabwepande


Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Ltd, Henry Machoke (wa pili kulia), akikabidhi mifuko 100 ya saruji kwa Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam (Serikali za Mitaa), Method Mkoba ikiwa ni msaada uliotolewa na shirika hilo kupitia kitengo cha huduma kwa jamii kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wanaoishi katika kambi ya Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Wahanga hao, Khalid Msuya, Meneja Masoko wa NIC, Adelaida Muganyizi na (Kulia) ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa NIC, Elisante Maleko.

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Ltd, Henry Machoke (wa pili kulia), akifafanua jambo baada ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam (Serikali za Mitaa), Method Mkoba (wa tatu kushoto), ikiwa ni msaada uliotolewa na shirika hilo kupitia kitengo cha huduma kwa jamii kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wanaoishi katika kambi ya Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Wahanga hao, Khalid Msuya, Meneja Masoko wa NIC, Adelaida Muganyizi na (Kulia) ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa NIC, Elisante Maleko.

Maofisa wa NIC wakiagana na wenyeji wao baada ya makabidhiano.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...