Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 28, 2012

COCA-COLA YAANZISHA TUZO KWA WAANDISHI BORA COPA COCA-COLA



Mkurugenzi mahusiano Coca Cola Kwanza( wa katikati )Bw. Evans Mlelwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za Coca Cola zilizoko moroco jijini Dar es salaam juu Tuzo kwa waandishi wa habari COPA COCA COLA,(na wa kwanza kulia) Katibu msaidizi Taswa Bw. George John,Wakwanza kushoto Meneja Masoko  Coca Cola Tanzania Bi.Salome Mabirizi.(
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
 

Coca-Cola Tanzania leo imetangaza kuanzisha tuzo kwa waandishi bora wa michuano ya soka ya vijana ya Copa Coca-Cola kwa kwa lengo la kuwazawadia wanahabari wanaofanya kazi nzuri hivyo kuwa chachu ya mashindanoya Copa-Cola yenye lengo la kujenga msingi wa maendelea ya soka nchini Tazanania.
Akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Coca Tanzania Salome Mabirizi amesema”Coca-cola inmatambua mchango mkubwa uliofnaywa na waadishi wa habari kwa miaka mitano iliyopita katika kuwahamasiha kushiriki mashindano haya.  Kuanzishwa kwa tuzo hizi ni njia moja wapo ya kuwahukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri ya kutangaza Coca-Cola.
Mabirizi alizitaja tuzo hizo kuwa ni mwandishi bora wa magazeti, mwandishi bora wa luninga, mwanahabari bora wa radio, mpig apicha bora (magazeti) na blogs, bora ambapo kila mshidi atazawadiwa Tsh 2m fedha taslimu.
Mchakato wa kuwapata washindi utafanwa kw akushirikiana na Chama cha waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na Coca-Cola na tayari zoezi hilo limeshaanza tangu Jumapili juni 24 wakati fainali za Copa Coca-Cola Taifa zilipozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam Fainali hizo zimepangwa kumalizika Julai 15.
Katika Mkuu Msaidizi wa TASWA, George John aliwaambia waanishi wa habari kuwa kamati ya tuzo za Copa Coca-Cola itafanya kazi kwa kuzingatia vigezo ili kumpata mshindi anayestahili katika kila kundi.  Amevitaja baadhi ya vigezo hivyo kuwa ni pamoja na stori au makala zinazohamasisha na kuwatia moyo vijan kuonyesha na kuendeleza vipaji vyao.
Johan ameipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kushirikiana na Shirika la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuenesha mashindano ya nchi nzima kwa lengo la kuibua vipaji vya wnasoka chipukizi nchini Tanzania.
Copa Caca_Cola imesaidia kubadili sura ya mpira wa miguu nchini Tanzania kwa kuwa chanzo cha kutegemewa cha wachezaji wenye viapaji wka timu za ligi kuu na timu za Taifa.  NI mashindano prkee nchini ambayo huchezwa nchi nzima kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa yakishirikisha maelefu ya vijana kila mwaka.
Ili kuwaeneeleza vijana zaidi.  Coca-Cola imekuwa ikipeleka wachezaji bora wa Copa Coca-Cola kwenye kambi za kimataifa za mafunzo ya soka nchi za nje.  Mwaka 2007 na 2008 wachezaji bora wa Copa Coca-Cola walikwenda nchini Brazil na kuanzia 2008 hadi mwaka jana walipelekwa Afrika Kusini.
Coca-Cola ni kampuni yenye historia ndefu ya kusaidia michezo ilianza kudhamini michezo ya olimpiki tangu 1928 na mpira wa miguuu tangu 1930.  Kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikidhamini Shirikisho la pira wa miguu duniani (FIFA) tangu 1974 na kuwa mdhamini rasmi wa FIFA tangu 1978 hadi sasa.

3 comments:

  1. Some girls order their prom dress and accessories fully online. Others use the Internet for research, narrowing down styles and price.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...