Marehemu Willy Edward akipokea zawadi kwa Mshindi yake kama mshindi wa Ujumla wimbo wa Jojina
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepokea kwa masikito makubwa
kifo cha Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde
ambaye alikuwa ni miongoni mwa wadau muhimu wa Mfuko huo.
Willy Edward enzi za uhai wake alitoa kipaumbele katika
kuuhabarisha umma kwa kutoa habari zinazohusiana na sekta ya Afya
hususan za kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Mfuko utaendelea kukumbuka na kuenzi yote yaliyofanywa na Willy kupitia nafasi yake ya uhariri katika gazeti la Jambo Leo.
Marehemu kwa mara ya mwisho alihudhuria mkutano wa saba wa
waandishi waandamizi na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika mjini
Morogoro mkutano ambao hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwaelimisha
juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko.
Kutokana na hayo, wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
wanaungana na tasnia ya habari, familia, ndugu na jamaa kuomboleza msiba
wa mhariri huyo.
Akimzungumzia marehemu, Ofisa anayeshughulikia Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF), Athuman Rehan, alisema kuwa marehemu alikuwa ni mtu mtulivu
na aliyependa kushirikiana na wenzake kwa hali na mali hivyo kuondoka
kwake ni pigo kubwa kwa tasnia ya habari.
Katika kufanikisha shughuli za msiba, Mfuko umetoa rambi rambi yake
kupitia uongozi wa Jambo Leo. Mungu ailaze roho yake pema poponi amina.
|
No comments:
Post a Comment