Timu
ya wasichana Arusha wakifurahia ushindi baada ya kuwafunga timu ya
kinonodoni wasichana mabao 2 – 0 jana katika michuano ya Airtel Rising
Stars inayofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es Saalam
Mwenyekiti
wa DRFA Amin Bhakresa akiongozana na Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane
Matinde wakisalimia na timu za wasichana kabla ya kuanza mechi thidi ya
timu ya wasichana wa Arusha na Mbeya katika michuano ya Airtel Rising
Star inayofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es Saalam. Katika
mechi hiyo Mbeya iliifunga Arusha 3-2
Michuano
ya Airtel Rising stars bado inaendelea ambapo jana timu za Temeke
zilishindana na timu ya ilala na kisha kufatiwa na timu za Kinondoni
kuchuana na timu za Arusha
Matokeo yaikuwa kama ifuatavyo Ilala
wasichana walishinda 2 na temeke0 na kwa upande wa wavulana Temeke
walishinda 3 na ilala 0, katika mechi zidi ya Kinondoni na Arusha ,
timu
ya Arusha wasichana ilshinda bao 2 kwa 0 thidi ya Kinondoni na kwa
upande wa wavulana Arusha ilishinda 3 na huku Kinondoni ikiondoka na
mabao 2. Michuano bado inaendelea Leo siku ya Alhamishi Asubuhi Ilala
itachuana na LindiNa ijumaa itakuwa nusu fainali kati ya timu
zitakazoshinda kwenye magroup yao
siku
ya Jumapili ndiyo itakuwa finali ya mashindano hayo ambapo timu
itakayoshinda itapata nafasi ya kushiriki mashindano ya Africa –
intercontinental tournament ambayo yatakayofanyika mwenzi wa nane nchini
Kenya, na pia katika fainali hiyo wachezaji sita nyota watachaguliwa
kujiunga na clinic chini ya mafunzo makocha wa klabu ya Manchester
united inategemea kufanyika pia mwenzi wa Agasti nchini Kenya
Wote mnakaribishwa kushuhudia
michuano hii inayofanyika katika viwanja vya karume kila siku,
kiingilio ni bure, njooo ushuhudie mashindano haya ya Airtel Rising
stars yenye hamasa na muamko mkubwa
No comments:
Post a Comment