Mwandishi wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka mkoani Iringa ZAHRA SULEIMANI anaripoti kuwa tukio hilo limetokea leo .
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo shuleni hapo mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Kihesa Manispaa ya Iringa Bw.ZABIHU HASSAN amesema tukio hilo limetokea
baada ya mwalimu kutoa adhabu kali kwa mwanafunzi wake.
Mwalimu
HASSAN amewakumbusha walimu wa shule za msingi kupunguza na kuacha
tabia ya kutoa adhabu ukali wa wanafunzi na badala yake wametakiwa kutoa
adhabu zitakazoweza kuwanufaisha wanafunzi katika taaluma.
Mzazi
wa mwanafunzi huyo FATMA KIGUDA amesema lazima serikali kuangalia
upya suala la adhabu ili sheria iweze kuchukua nafasi na iwe fundisho
kwa walimu wengine ili waweze kujifunza.
Hata
hivyo, mwalimu ambaye ametenda kosa hilo ambaye amefahamika kwa jina la
Mwalimu KIFYOGA amekanusha madai hayo na kusema kuwa hakukusudia
kufanya tukio hilo bali ni sehemu ya maonyo kama wanafunzi wengine.
No comments:
Post a Comment