Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 6, 2012

NAPE:ARDHI IKIMILIKIWA NA WATU BINAFSI WANYONGE WATATAABIKA


NA BASHIR NKOROMO, NJOMBE
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kusiistiza juu ya msimamo wake wa ardhi kuendeleakumilikiwa na serikali kwa maslahi ya taifa zima.

Msimamo huo ulielezwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Turbo mjini Njombe.

Nape alisema, tofauti na mapendekezo ya baadhi ya vyama vya siasa kwamba ardhi imilikiwe na wananchi, CCM inaona kwamba bado kuna ulazima wa ardhi kuwa chini ya miliki ya Serikali, kwa sababu kuwafanya hivyo kuna faida kubwa zaidi.

"Sisi Chama Cha Mapinduzi, baada ya kutafakari kwa kina, katika rasimu yetu kuhusu katiba mpya ya Tanzania tumependekeza pamoja na mambo mengine, kwamba ardhi iendelee kumilikiwa na serikali kwa sababu tunaona kwamba utaratibu huu ndiyo unaifanya ardhi kuwa mali ya wanancho wote", alisema Nape.

Alisema, madhara ya ardhi kumilikiwa na watu binafsi katika nchi ni jambo la hatari sana, kwa sababu inaweza kumilikiwa na mabepari wachache hata wasiozidi wanne nchi nzima kama ilivyo katika baadhi ya nchi jirani hatua inayowafanya raia kulazimika kuwapigia magoti mapepari wanapohitaji hata eneo dogo tu kufanyia shughuli zao.

Nape aliwataka Watanzania kuunga mkono hoja ya CCM ya  kuendelea kuifanya ardhi kuwa chini ya miliki ya watu binafsi na kuachana na ile ya Chadema inayosisitiza kutaka ardhi imilikiwe na watu binafsi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...