KITUO
cha Utamaduni cha Jamhuri ya Irani jana kimewasarifisha vijana wawili wa
Kitanzania kwenda Iran kwa ajili ya Mashindano ya Kimataifa ya Kusoma Kuruan yatakayoshirikisha
nchi 40.
Akizungumza
wakati wa kuaga vijana hao, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
alisema vijana hao wanapaswa kuwa makini katika mashindano hayo kwani wamebeba
bebndera ya nchi.
Alisema
safari hiyo imegharimiwa na nchi ya Iran ambapo vijana hao wakati wakiwa nchini
humo kwa muda wa juma zima huduma zote za kijamii zitakuwa juu yao.
Alhad
Salum aliwataja vijana hao kuwa ni Saidi Idd Saidi na Omar Salumu ambapo Saidi
anatarajiwa kushiriki katika shindano la kusoma ,Tajuwid’ huku Salumu akishiriki
katika kosoma Kuruan ambapo shindano hilo litafanyika juma lijalo.
Alisema
vijana hao walipata fursa hiyo baada ya kushinda katika shindano lililoandaliwa
kwa kuwakutanisha na wenzao kutoka vyuo na taasisi mbalimbali hapa nchini.
“Leo
tunawaaga vijana hawa na tunaamini kuwa wataenda kufanya vizuri na watarudi
wanang’ara kwa kupata ushindi”alisema Salum.
Alhad
Salum anatarajia kuwa safari hii vijana hao watarudi na ushindi wakwanza
ukilinganisha na ule wa mwaka jana, Tanzania ilishika nafasi ya pili.
Aidha,
alisema anakishukuru kituo hicho cha Utamaduni kwa kuandaa mashindano hayo kila
mwaka ambapo ni jambo zuri katika kuwajenga vijana katika maadili mema
yatakayowakinga na vitendo viovu duniani.
Alisema
kwa kila mwenye kuifahamu kuruan anapaswa kumfundisha mwingine kitendo ambacho
ndicho kinachofanywa na nchi hiyo ya Irani.
Naye
Mkurugenzi wa Kituo hicho Morteza Sabouri aliwaasa vijana hao kwenda kufanya
kile kinachowapeleka huko kwani watambuwe nafasi hizo ni adimu ukichukulia wapo
vijana wengi wenye uwezo kama wao hapa nchini.
No comments:
Post a Comment