Baadhi ya waandishi wa habari hao wakipiga picha na baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliofanya mahojiano mbalimbali na wanahabari."] |
Baadhi ya waandishi wa habari hao wakipiga picha na baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliofanya mahojiano mbalimbali na wanahabari."] |
Na hapa ndipo alipo muwekezaji mkubwa wa madini ya almasi anayeendesha shughuli zake eneo la
Mwandui."]Hapa tukipata picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari wa
mkoani Shinyanga katika ofisi yao ya mkoa (Shinyanga Press Club)"]
Baadhi ya wanahabari hao wakiponza tumbo eneo la Mwandui walipokuwa kazini katika mahojiano na wananchi."]
Waandishi wanaofanya habari za uchunguzi maeneo ya vijijini Kata ya
Songwa, Wilaya ya Kishapu mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kumaliza warsha ya siku mbili iliyoendeshwa na Mtandao wa
Jinsia Tanzania (TGNP) kabla ya kuingia kazini."]
Na Mwandishi wa Thehabari.com, Songwa-Shinyanga
BAADHI
ya waandishi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoani Shinyanga
wametembelea machimbo ya almasi yanayofanywa na wananchi eneo la mjini
mdogo wa Songwa.
Ziara ya waandishi hao imekwenda sambamba na kufanya uchunguzi juu ya
huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na Serikali kwa wakazi wa
maeneo hayo, yaliomo ndani ya Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.
Waandishi hao wameshuhudia namna wananchi na hasa vijana
wanavyojishughulisha na shughuli nzima za machimbo ya madini ya almasi
licha ya Kata ya Songwe kukabiliwa na huduma duni za maji safi na salama
kwa matumizi yao pamoja na yale ya shughuli za machimbo.
Mtandao huu utawaletea mahojiano ya wananchi eneo hilo pamoja na hali
halisi ya huduma anuai za kijamii kwa wakazi wa Kata hiyo ya Songwa
iliyopo Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga muda si mrefu.
No comments:
Post a Comment