Afisa
Wa Michezo ya bahati nasibu Abdallah hemed (kushoto) akiangalia moja ya
kuponi yenye jina ambalo lilitangazwa mshindi mara baada ya droo ya
kutafuta washindi watano wa kampeni ya Ongeza akiba yako inayoendeshwa
na benki ya Barclays nchini Tanzania anayeshuhudia Katikati ni Meneja
Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania Bi Sarah Munema
Mkuu
wa kitengo cha Matawi ya Benki ya Barclays Tanzania Bw Musa Kitoi
akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
kampeni hiyo Mpya iliyozinduliwa leo jijini Dar kwa Droo ya kutafuta
washindi watano. Kampeni hiyo ya Ongeza Akiba Yako na Barclays
imezinduliwa leo Jijini Dar.
Mmoja
wa Washindi Wa Kampeni ya Ongeza akiba Yako inayoendeshwa na benki ya
barclays Tanzania (wa pili kushoto) akisoma moja ya kuponi yenye jina la
mteja ambaye ameibuka mshindi katika kampeni ya Ongeza Akiba Yako
iliyozinduliwa leo kwa kuchezesha droo ya bahati nasibu katika ofisi ya
benki hiyo ya Barclays Tawi la Mwenge.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Uzinduzi wa Kampeni ya Ongeza
Akiba na Barclays ambayo imezinduliwa leo Katika Tawi la Barcalys Mwenge
leo
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
6, Novemba, 2013
Benki
ya Barclays Tanzania, Leo hii Imezindua Rasmi Kampeni ijulikanayo kama
“Ongeza Akiba Yako” kwa wateja wake. Kampeni hii ilizinduliwa Mnamo
Tarehe 16, Septemba, 2013, na inatarajiwa kuendelea Mpaka Tarehe 16,
Januari, 2014.
Kampeni
hii itawapa fursa wateja watano, (5) kila mwezi, kujishindia mpaka
kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni moja kwa kila mmoja katika
kipindi chote cha kampeni. Droo ya kampeni itakuwa ikifanyika katika
kila wiki ya mwisho wa mwezi, ikiangalia vigezo vya kila mteja.
Akiongea
na waandishi wa Habari leo hii, Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wa
kawaida, Bwana Musa Kitoi alisema, “Kampeni hii iko wazi kwa wateja wote
wa Benki ya Barclays, na wale wapya, kupitia akaunti zao mbali mbali za
fedha za Tanzania. Kwa mteja kujipatia nafasi ya kushiriki, mteja
anapaswa kutokushuka chini ya kiwango cha shilingi Laki Tatu (300,000).
Kiwango hiki kinatakiwa kiwekwe ndani ya mwezi toka kampeni izinduliwe,
na kinatakiwa kisishuke kiwango kilichotajwa. Wateja wapya wanaweza
kuingia kwenye droo hii pindi tu watakapofungua akaunti zao, na kuweka
kiwango kisichopungua shilingi laki tatu. Baada ya kufungua akaunti, na
kuweza kubakisha kiwango kilichotajwa kwenye akaunti, wateja, (wa zamani
na wapya) wataingizwa kwenye droo ya kila mwezi, na wateja watano (5)
watapata bahati ya kuongezewa mara mbili akiba zao, na katika droo kubwa
ambayo itakuwa mwisho wa kampeni, mshindi atajinyakulia kiasi kipatacho
milioni thelathini, (30,000,000)”.
Aliendelea
na kusema, “Leo hii tutapata washindi wetu wa kwanza watano (5) wa
kampeni hii, na Benki ya Barclays inawapongeza wote waliojishindia, na
kuwasihi wateja wote kushiriki katika kampeni hii, wakati tukikaribia
kipindi cha sherehe za mwisho wa mwaka”.
No comments:
Post a Comment