Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo na Mh.Sadifa
Juma mbunge wa Donge mapema hii leo bungeni mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Gregory Teu
(kushoto) akiwasili katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mapema hii leo,
kulia ni mbunge wa Rombo (CHADEMA) Mh. Joseph Selasini.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Godluck Ole Medeye akiwasili
katika viwanja vya bunge mapema hii leo kuhudhuria mkutano wa kumi na tatu wa bunge unaoendelea mjini
Dodoma. Picha zote
na Eliphace Marwa ,Maelezo Dodoma
*************************************************
Frank
Mvungi-Maelezo Dodoma
Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendeelea kutoa kipaumbele kwenye Sekta ya
Uvuvi ili kuwawezesha wavuvi wadogo kupata zana za kisasa.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh.Dr. Mathayo
David Mathayo wakati akijibu swali la mbunge wa (CUF) viti maalum Mh.Amina
Abdallah aliyetaka kujua kwa nini Serikali Haiwezeshi wavuvi wadogo zana za
kisasa .
Akitoa
ufafanuzi wa hatua zilizochukuliwa Dk Mathayo alisema wavuvi wadogo 4,000
waliwezeshwa kutekeleza miradi ya uvuvi 240 na Serikali imeshaainisha maeneo ya
utekelezaji unaolenga kuwa na uvuvi wenye tija ambayo ni pamoja na mradi wa
usimamizi wa mazingira ya bahari na ukanada wa pwani (MACEMP).
Aliongeza
kuwa zaidi ya shilingi milioni 300 zimewanufaisha wavuvi 634 wanaoishi katika bahari za mafia,
Ghuba ya mnazi na maingilio ya mto Ruvuma waliopewa ruzuku ya kununua injini za
boti 22,madema 20,maboya26,000,boti 28 za uvuvi na nyavu 1,403 .
Dr. Mathayo
alibainisha kuwa Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilitoa zaidi
ya milioni 59 kwa vikundi 8 kwa ajili kununulia injini za boti na zana za uvuvi .
Akifafanua
zaidi Dr. Mathayo amesema katika eneo la
mbambabay kutajengwa kiwanda cha kutengeneza boti ili kuwawezesha wavuvi wadogo
kupata boti imara na zana bora za uvuvi.
Katika
kuendeleza Sekta ya Uvuvi Dr. Mathayo
anasema kwa mwaka wa fedha 2013/14 Serikali itaanzisha mfumo wa kutoa
ruzuku kwa wavuvi wadogo wadogo ili waliosajiliwa ili kuwawezesha kununua zana
bora ambapo chini ya utaratibu huu maboti 50 na viambata vyake na nyavu za
uvuvi 15,562 vitatolewa kwa wavuvi.
No comments:
Post a Comment