Na Peter Mwenda
WAHITIMU
wa Shule za Sekondari na Vyuo vikuu nchinin wameshauriwa kutokata tamaa
kutokana na uhaba wa ajira nchini bali waendelee kujishughulisha kwa
kufanya kazi za ubunifu.
Hayo walisema jana Dar es Salaam na aliyewahi kuwa Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa DAr es SAlaam, Bw. John Guninita kwenye mahafali ya
Kidato cha Nne kwa Wanafunzi waliohitumu masomo ya Kidato cha Nne Katika
Shule ya Sekondari ya Dkt. Didas Masaburi iliyocho Chanika Dar es
Salaam.
Bw. Guninita alisema tatizo la kukosekana kwa ajira nchini ni
kubwa lakini linaweza kutatulika endapo wahitimu wakiacha kusubiri ajira
za Serikali badala ya kubuni njia ya kuendesha maisha yaokutumia akili
waliyonayo.
Alisema Serikali ilitoa fursa kwa watanzania wenye uwezo
wa kufungua shule wafanye hivyo na matokeo yake kuna shule ngingi za
binafsi ambazo zinachangia kupatikana kwa elimu bora kama ya Dkt. Didas
Masaburi ambayo inatoa vijana wengi wenye vipaji kwenda kidato cah nne,
sita na Chuo Kikuu.
"Shule zaidi ya asilimia 95 zinamilikiiwa na Serikali lakinin
kutokana na ongezeko la watu, serikali pekee isingeweza kukidhi mahitaji
ya elimu nchini imetoa nafasi kuanzishwa kwa shule binafsi nchini"
alisema Bw.Guninita.
Alisema vijana wanaohitimu mafunzo na kukata tamaa ya kukosa
ajili baadhi yao wanajiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na
ngono zembe zinazosababisha matukio ya vifo vya kutisha vinavyotokea
nchini.
Katika mahafali hayo ya saba ya shule ya Sekondari, Dkt. Didas
Masaburi wanafunzi waliomaliza masomo yao waliomba Serikali kutoa vifaa
kwa shule binafsi ambazo zinafanya vizuri katika ufundishaji.
Mkuu
wa Shule hiyo, Bw. Michael Owiti alisema wanashirikiana vizuri na
wazazi kuhakikisha mwanafunzi anayeiungia kusoma katika shule hiyo
anapata elimu ya kutosha ili mwisho wa simu akumbuke kuwa elimu
aliyonayo inatokana juhudi za shule hiyo kuwalea kwa lengo la kuishi
maisha bora baadaye.
No comments:
Post a Comment