Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 8, 2014

BENKI YA NBC YAFUTURU NA WATEJA WAKE HOTELI YA SERENA JIJINI DAR


 Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokewa na Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC Tanzania, William Kallaghe na Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Mussa Assad (kulia) alipoalikwa kama mgeni rasmi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam, Ijumaa ya wiki iliyopita katika Hoteli ya Serena.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (wa pili kushoto) Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale (kushoto), wafanyakazi na wateja wa benki hiyo wakijumuika pamoja katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu ( kushoto) akiwaongoza baadhi ya wateja wa benki hiyo kushiriki futari waliyowaandalia jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali na kuwa karibu wateja wao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...