Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 8, 2014

AIPS YAANDAA MAFUNZO KWA WANAHABARI CHIPUKIZI


Habari wadau, Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), kimeandaa mafunzo kwa ajili ya waandishi wa habari za michezo chipukizi wa umri kati ya miaka 19-25 yatakayofanyika Doha Qatar mwishoni mwa mwaka huu wakati wa mashindano ya Dunia ya Mchezo wa Kuogelea.

Kutokana na hali hiyo, AIPS imetoa nafasi chache kwa watakaokidhi vigezo vyao katika mabara mbalimbali duniani. Hivyo nimeattach barua yao na nini kinatakiwa katika mafunzo hayo, ambayo wahusika watagharamia nauli ya kwenda Doha na kurudi mji husika anaotoka mhusika, chakula na malazi muda wote atakaokuwa huko.

Kwa vile hatua ya mwisho itahusisha chama cha nchi husika kumthibitisha muombaji, naomba wote watakaofikiri wana sifa zinazotakiwa wasome vizuri hiyo attachment, kisha watume kwa Makamu Mwenyekiti TASWA, Egbert Mkoko ambaye ndiye atasimamia jambo hilo kwa email: njali5@yahoo.com nataswatz@yahoo.com

Lakini pia kama utamudu unaweza ukaomba binafsi bila kutumia chama na mwisho wa kufanya hivyo ni Agosti 15 mwaka huu na watume kwa email:youngreporters@aipsmedia.com. Kwa watakaotaka kupitia TASWA wajitahidi kabla ya Agosti 10 mwaka huu.

Tusihofie kuomba kwani mwaka 2011 aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mtanzania mwenzetu, Mwita Mwaikenda aliomba nafasi hiyo na aliipata. Ukiwa unahitaji ufafanuzi tuwasiliane 0713-415346.

Nawasilisha,
Katibu Mkuu TASWA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...