Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 4, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA NCHINI TANZANIA. IKULU DAR


 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo.
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan,  wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo. 
********************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA

Ikulu jijini Dar es Salaam, Julai 03, 2014
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal leo Alhamisi Julai 03, 2014 amekutana na Waheshimiwa Mabalozi wa nchi za Oman na Syria wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Mheshimiwa Makamu wa Rais amekutana na Mabalozi hao ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Awali alikuwa ni Balozi wa Oman, Mheshimiwa Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish aliyefika kukutana na Mheshimiwa Makamu na kufafanua kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Oman unazidi kuimarika na kwamba wawekezaji kutoka Oman wamekuwa wakija kwa wingi kuwekeza Tanzania tofauti na siku za nyuma huku pia Tanzania ikionesha kufungua milango yake kwa uwekezaji mkubwa wa kati nchini Tanzania.

Kwa upande wa Balozi wa Syria Mheshimiwa Abdulmonem Annan yeye alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa Syria iko katika kipindi kigumu na kwamba nchi hiyo kwa sasa inatafuta kila linalowezekana kurejesha amani. Balozi huyo alifafanua kuwa nchi yake inahitaji msaada wa nchi za Kimataifa ili kusaidia kuweka pande zote zinazokinzana mezani kwa lengo la kufikia maazimio yatakayoifanya nchi hiyo isiparanganyike.
Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi za Syria kuwa, Tanzania inatamani sana kuona hali ya utulivu inarejea Syria na kwamba nchi hiyo inaendelea kujenga uchumi uliobomoka tayari. Pia alisema kuwa msimamo wa Tanzania unabakia katika kutaka pande zinazohusika katika mgogoro huo zinafuikia suluhu kwa amani ili wananchi wengi wasipoteze maisha.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...