BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita alibuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumdunda vibada Lizbeth Sivhaga wa nchini humu
huu
ni mpambano wake wa kwanza Lulu kucheza nje ya nchi na kufanikiwa
kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo uho ulioanza kwa kasi ya
mashambulizi ya uku na kule kila mmoja kutaka kumpiga mwenzie raundi za
awali
ata
hivyo ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu Kayage alimwelemea sana
mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa
kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili
ushindi
wa Llulu Kayage ulichagizwa na kocha maarufunchini Rajabu Mhamila
'Super D' ambapo siki mbili kabla ya kuondoka nchini alimzawadia vifaa
mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumwaidi ushindi kwa asilimia zote
bondia
huyo anatarajia kurudi nchini agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya
mapambano yake mengine ya kimataifa wakati uho uho bondia Ramadhani
Shauri amepoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na
bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini ambapo mpambano uho wa raundi nane ulijikuta ukisha katika raundi ya nne
Bondia Lulu Kkayage akiwashukuru mashabiki walio udhulia kwa kuwapigia magoti na kuwapungia mikono baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Refarii akiwa katikati uku akiwashika mikono mabondia Llulu Kayage na Lizbeth
Sivhaga wa Afrika kusini kwa ajili ya kutangaza mshindi Lulu alishinda
kwa TKO ya raundi ya pili kushoto ni Yassini Abdallah
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' akimnyoosha mkono juu bondia Lulu Kayage baada ya kuibuka mshindi |
Yassin Abdallah 'Ostadh' akimwinua juu mkono baada ya kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili |
No comments:
Post a Comment