Mrembo aliebuka kidedea kwenye shindano
la kumsaka barozi wa mkoa wa Kilimanjaro 2015,Yolanda Shayo ametembelea
vituo vya watoto yatima katika eneo la mamba Malangu moshi vijijini.
Shughuli hiyo ilifanyika mapema jana ambapo mrembo huyo alitembelea vituo vinee ambavyo ni Msoroe,Mrieni,Kikoro na kotela kwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto na kula nao chakula cha pamoja.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa na mrembo huyo ni kalamu,madaftari,rula na sabuni za kufulia na kuogea,Yolanda alipata fulsa ya kuongea na viongozi wa vituo hivyo ambapo alibaini changamoto balimbali zinazokabili vituo hivyo.
Yolanda ambae ni Miss Kilimanjaro Ambassador wa mara ya kwanza ameonesha jitihada zake za kuanza kazi ya urembo kwa kuitumikia jamii yake ambapo alikuwa ana wito huo tangu akiwa mtoto.
Kwa nafasi aliyoipata mrembo huyo ameaidi kuwa kinara kuutangaza utamaduni wa mkoa wa kilimanjaro na kuvitangaza kitaifa na kimataifa vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya mkoa huo.
"mbali ya kuwa mrembo na balozi wa mkoa wa kilimnjaro nitahakikisha natumia fulsa hii kupeleka ujumbe mbalimbali kwa jamii yangu ikiwemo kuwahimiza vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba" aliongea Yolanda.

Miss
kilimanjaro ambassador 2015,Yolanda Shayo akiwa katika picha ya pamoja
na mtoto ambae anaosha kalamu ikiwa ni sehemu ya zawadi zilizogawiwa na
mrembo huyo.
Yolanda Shayo akisaidia kugawa chakula kwa watoto na viongozi wa
vituo hivyo,ambapo alishiriki kwa pamoja nao katika chakula cha mchana.
No comments:
Post a Comment