Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 2, 2011

HAFLA YA KUCHANGIA HOSPITALI ZA AMANA NA CCBRT YAFANYIKA MOVENPICK USIKU HUU.

Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Taasisi ya Mkapa Faoundation Anna Senkoro akifuatilia kwa makini wakati kundi la Mutati kutoka nchini Kenya, likitumbuiza katika hafla ya Shear Charrity Ball kwa ajili ya kuchangia matibabu ya wanawake wenye ugonjwa wa Fistula kwenye hospitali ya CCBRT, na ukarabati wa miundombinu katika wa Hospitali ya Amana, inayofanyika kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam Tanzania, kushoto ni Mkurgenzi wa kampuni ya Shear Illusion Shekha Nasser.
Kundi la THT likicheza muziki wa Salsa katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Taasisi ya Mkapa Faoundation Anna Senkoro akiingia katika hoteli ya Movenpick kwa ajili ya kushiriki katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Shear Illusion Shekha Nasser.
Kundi la Mutati kutoka nchini Kenya liktumbuiza katika hafla hiyo.
Waalikwa wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakijadiliana jambpo katika hafla hiyo.
THT wakitumbuiza katika hafla hiyo.
Mdau Khadija akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Shear Illusion Shekha Nasser.
Wageni mbalimbali wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Picha zaidi Fullshangwe Blog.

TUSKER ALL STARS ILIVYO FANA NAIROBI KENYA



Mfalme wa miondoko ya Dance Hall Raia wa Jamaica Shaggy akikamua jukaani.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga kushoto akiwa na Mkewake ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Prime Time Promotions Juhayna Ajmy na Ofisa Mwandamizi wa Kampuni Prome Time Promotions God Kusaga.








IGUNGA WAPIGA KURA LEO


Watu wakiwa kwenye foleni kituo cha Ukumbozi Igunga mjini katika uchaguzi mdogo jimbo la Igunga mkoani Tabora leo

WAZIRI DK. NCHIMBI AZINDUA MFUMO WA DIGITAL WA KAMPUNI YA VING'AMUZI YA STARTIME MEDIA KWA KUSHIRIKIANA NA TBC


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda katikati, akizindua mfumo wa Kidigital utakaotumiwa na kampuni ya Televisheni kupitia Ving'amuzi Startime Media usiku huu, katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Godfrey Nyachia Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi TBC, Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng na kutoka kushoto ni Clement Mshana Mkurugenzi wa TBC na Mwenyekiti wa Bodi ya Startime Bw. Pang Xingxing wakishiriki pamoja na Waziri kuzindua mfumo huo.
Hapa tayari wameshazinduza kama linavyoonekana neno Startime katika tufe hilo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi katikati akigonganisha glasi kama ishara rasmi ya uzinduzi wa mfumo wa Kidigital utakaotumiwa na kampuni ya Televisheni kupitia Ving'amuzi Startime usiku huu kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Godfrey Nyachia Mwenyekitiwa Bodi ya wakurugenzi TBC, Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng na kutoka kulia ni Clement Mshana Mkurugenzi wa TBC na Mwenyekiti wa Bodi ya Startime Bw. Pang Xingxing wakishiriki wakishiriki kwa pamoja katika kugonganisha glasi
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi huo.
Kutoka kulia ni Davis Mwijage Meneja Masoko Msaidizi, Pamela, Kidali na Freddy Mlay wakipozi kwa picha.
Makamanda wa Startime Media wakiwa katika picha ya pamoja.
Kutoka kulia ni Freddy Mlay afisa masoko, Zuhura Meneja Masoko na Davis Mwijage Meneja masoko Msaidizi.
Eeh Pozi lingine tena kutoka warembo wa Startime Media.
Mwigizaji Steven Kanumba akiingia katika hafla ya uzinduzi huo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na balozi wa China nchini Tanzania Balozi Liu Xinsheng, kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Time Media Bw. Pang Xingxing.
Vimwana wa kampuni ya Startime wakipozi kwa picha.
Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana kulia na Mwenyekiti wa bodi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Godfrey Nyachia wakijadilia jambo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Digital wa kampuni hiyo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi akiingia ukumbini, tayari kwa kuzindua kampuni ya Televisheni kwa njia ya Ving'amuzi, kulia ni Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana.
Bw Davis Mwijage meneja msaidizi wa Masoko akieleza jambo mbele ya mitambo ya kurushia matangazo ya kampuni hiyo kwa waandishi wa habari kulia ni Zuhura Meneja Masoko wa Startime , wengine kutoka kushoto ni Salum Shomari fundi na Terry Du Meneja mkuu wa ufundi.
Meneja mkuu wa ufundi Terry Du kushoto na moja wa mafundi wa kampuni hiyo Salum Shomari , Davis meneja msaidizi wa masoko na Zuhuru Meneja Masoko wa Star Time wakiwaongoza waandishi wa habari, wakati walipotembelea eneo la mitambo ya kupokelea matangazo na kurusha iliyopo mikocheni jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu wa ufundi wa kampuni ya Startime Media Bw Terry Du akiwaelezea waandishi wa habari, jinsi mitambo ya kampuni hiyo inavyorusha matangazo yake katika ziara waliyoifanya kabla ya kampuni hiyo kuzinduliwa rasmi leo.

KAMPUNI YA SIMU TANZANIA TTCL YATOA TAARIFA KWA UMMA


UHAMISHAJI NJIA ZA MAWASILIANO

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) inapenda kuwafahamisha wananchi na wateja wake kwa ujumla kuwa kwa sasa kuna kazi ya uhamishaji wa njia za mawasiliano kandokando ya barabara mpya ya Bagamoyo ( Mwenge – Tegeta).

Kazi ya kuhamisha njia za mawasiliano ni inafanywa na wakala wa barabara (TANROADS) aliyeingia mkataba namba QTN/AE001/2009/2010/DSM/E/146 na mkandarasi.

Katika mkataba huu, Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) jukumu lake kubwa ni kuelekeza na kushauri njia mpya ya mtandao wa simu utakapopita tofauti na njia za awali.

Tunaomba ieleweke kuwa hadi hapo njia mpya ya simu itakapokamilika ndipo ile ya zamani itaondolewa kuepusha wateja kukosa huduma.

Tayari wakala wa barabara(TANROADS ) amekwishakamilisha awamu ya kwanza ya kuhamisha njia za simu kutoka Mwenge mpaka njia panda ya Africana. Na sasa kazi inaendelea kuanzia njia panda Africana kuelekea Tegeta.

Kwa vile kazi inahusisha njia za mawasiliano zilizopo juu na za chini ya ardhi, kitaalam kazi hii lazima iende sambamba na ujenzi wa barabara mpya kwa kuwa katika ujenzi , mkandarasi wa barabara anajenga njia za kupitisha mawasiliano baada ya kupima kina cha kwenda chini, kwani kina cha barabara kinafahamika tu pale udongo unapokuwa umechimbuliwa na mkandarasi wa barabara.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

NBC yachangia ununuzi wa gari la wagonjwa kituo cha Afya cha Mt. Benedict.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 10 kutoka kwa Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja zilizotolewa na NBC kama sehemu ya mchango wake kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict kilichoko Kitunda nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. NBC pia imefungua akaunti maalumu kupata fedha zitakazosaidia kufanikisha ununuzi huo. Kushoto ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Songea, Norbet Mtega na wa tatu kushoto ni Mama Mkuu wa Shirika la Masista Wabenedictini, Sr. Maria Shukrani Mkonde.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili kushoto) akizungumza na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Songea, Norbet Mtega (kushoto) wakati wakitembelea jengo jipya la Kituo cha Afya cha Mt. Benedict katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho ambako Benki ya NBC kupitia Mshauri wake wa Mambo ya Habari, Redemptus Masanja (kulia) ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 zitakazotumika kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo hicho. Wa pili kulia ni Sr. Maria Agnesia wa kituo hicho. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Wacheza ngoma ya asili wakitoa burudani katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict hafla ambayo Benki ya NBC ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa gari la wagonjwa wa kituo hicho. NBC pia imefungua akaunti maalumu ili kukusanya fedha zitakazotumika kukamilisha ununuzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza kabla ya kupo mfano wa hundi ya shs milioni 10 kutoka kwa Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja (kulia kabisa nyuma) zilizotolewa na NBC kama sehemu ya mchango wake kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict kilichoko Kitunda nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Kushoto ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Songea, Norbet Mtega na kulia ni Mama Mkuu wa Shirika la Masista Wabenedictini, Sr. Maria Shukrani Mkonde.

WIKI YA NENDA KWA USALAMA


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaban Kayungilo na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani, Kamishana Mohamed Mpinga wakionesha stika zitakazo saidia katika wiki ya nenda kwa usalama
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani akikabidhiwa stika na Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya
Kamishna Mohamed Mpinga na Beatrice Singano Mallya

MAFURIKO MWANANYAMALA KISIWANI,MTO NG'OMBE WAACHA NJIA JIJINI DAR ES SALAAM.


Wakazi wa Mwananyamala wakivuka Mto Ng'ombe kwa tabu ulioacha njia yake na kutengeneza njia nyingine baada ya mvua kunyesha maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam.Wakivuka kwa taabu
Wanafunzi na watu wazima wakivuka kwa hofu
Ni hatari ......
Hatariii hii kwa Watoto
Tazama watoto wako peke yao ni hatari hii
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...