Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 3, 2013

WAFUGAJI WATAKA KATIBA MPYA KUWARUHUSU KUUA SIMBA WANAOVAMIA MIFUGO YAO NCHINI.


Wafugaji  wakazi wa Mlowa  jimbo la Isimani  mkoa  wa Iringa  wakiwa katika mkutano wa kukusanya maoni ya katiba  mpya jana. PICHA http://richard-mwaikenda.blogspot.com/
Mfugaji  akitoa maoni yake  juu ya katiba  mpya  na  kulalamikia  simba  wanaoua mifugo  yao
Mwenzeshaji  Happy Kikoga  kutoka  kituo cha msaada cha sheria na  haki  za  binadamu akiwasomea  rasimu  ya  katiba wananchi  wa Mlowa Isimani
Mmoja kati ya  wanawake  wakazi wa Mlowa  akichangia katika mkutano huo kwa  kutaka  wanaopandikiza chuki  za kidini  kupewa adhabu kali.
WAFUGAJI jamii ya  kimasai na Mang'ati  wakazi  wa Mlowa  jimbo la Isimani  wilaya ya  Iringa  vijijini mkoani Iringa  wametaka katiba mpya ijayo  kuwaweza kuwatetea wafugaji kwa  kuingiza  kipengere  kitakachowaruhusu  wao  kuingia katika  hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha  kuwasaka  simba  wanaoua mifugo  yao  kuwaua.
Wafugaji  hao  walitoa  maoni hayo juzi  katika  ofisi  za serikali ya  kata  wakati  wakichangia rasmu ya katiba mpya  zoezi lililoendeshwa na kituo  cha  msaada cha sheria na  haki  za  binadamu.
Walisema  kuwa  Simba  wameendelea kuwatesa na  kila  wakati  wanaendelea  kuua mifugo yao na  pindi  wanapofanya msako  wa  kuwasaka  askari  wa  wanyamapori  wanawachukulia hatua  kali .
Hivyo  walisema  ili  katiba  ijayo  iweze kutambua haki za  wanyama  wengine na  pia  kutambua  uwepo  wa  wafugaji ni  vema kuingizwa  kipengere  kinachowapa nafasi  ya  kuwaua  simba wanaokula  wanyama  wao.
Mbali ya  kutaka  kuwekwa kwa  kipengere  hicho  bado  wafugaji hao  walitaka  kutambuliwa  rasmi  na katiba  ijayo badala  ya ilivyo sasa  ambapo  wamekuwa wakihamishwa  kama  wanyama . Pamoja na  wafugaji hao kwa upande  wake wananchi  wa kawaida  wameeleza  kusikitishwa na hatua  iliyofikiwa ya mchakato  huo wa katiba  mpya  hatua ya  kukusanya maoni  juu ya rasmu wakati  wao hata katiba  iliyopita  hawaijui na rasmu  hiyo  hawajapata  kuoina.

UCHAWI WATUMIKA MAONYESHO YA WAKULIMA KANDA YA MASHARIKI NANE NANE KUWAVUTA WATU KATIKA MABANDA MOROGORO.


 Msanii wa salakasi, Hassan Mkenjula a.k.a Spider Man akionyesha uchwi unaotokana na mazoezi katika moja ya mabanda kwenye maonyesho ya wakulima kanda ya mashariki namna anavyoweza kulala akiwa juu ya kamba yanayofanyika kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Nane Nane Manispaa ya Morogoro. 
PICHA WWW.JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
 Baada ya kuvaa nguo zote Spider Man akion
ekana huku akitembea juu ya kamba baada ya kuvaa nguo ikiwemo fulana, tai na suruali.
 Baada ya kuvaa zote juu ya kamba hiyo.
 akimalizia kuvaa mguu wa kushoto.
 akivaa mguu wa kulia.
 suari kabla ya kuivaa akiwa juu ya kamba hiyo.
 akivaa.
 Akionyesha fulana kabla ya kuivaa.
 
Alianza hivi wakati akifuata nguo ili aweze kuvaa.

Thursday, August 1, 2013

STARTIMES KUONGEZA VIPINDI NA CHANALI,MAADHIMISHO YA MIAKA MITATU



Ofisa Habari wa Kampuni ya Startimes  Erick Cyprian kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezaka kwa chanal wakati wa kipindi hiki cha kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe kampuni hiyo kulia ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Zuhura Hanif Picha na SUPER D

Ofisa Habari wa Kampuni ya Startimes  Erick Cyprian kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezaka kwa chanal wakati wa kipindi hiki cha kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe kampuni hiyo kulia ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Zuhura Hanif Picha na SUPER D
Ofisa Habari wa Kampuni ya Startimes  Erick Cyprian kushoto akizungumza  kwa msisitizo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuongezaka kwa chanal wakati wa kipindi hiki cha kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe kampuni hiyo kulia ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Zuhura Hanif Picha na SUPER D

Ofisa Habari wa Kampuni ya Startimes  Erick Cyprian kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezaka kwa chanal wakati wa kipindi hiki cha kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe kampuni hiyo kulia ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Zuhura Hanif Picha na SUPER D

EAST AFRIKA MELOD KUWASHA MOTO Traventine Hotel IDDI PILI

BENDI Kongwe ya muziki wa Taarabu Nchini East African Melody imetangaza kutoa burudani wakati wa shamra shamra za sikukuu ya iddi  pili  katika  ukumbi wa Traventine Hotel akizungumzia onesho hilo  mwandaaji wa onesho hilo Habbas Husseni 'Chezntembaa'

Amesema ameamua kuchukua bendi hiyo itoe burudani ili ikonge nyoyo za mashabiki mbalimbali wa taarabu ambapo walikosa raha hizo wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Katika Shamra shamra hizo za sikukuu ya iddi  watakuwa wakitambulisha nyimbo zao tatu mpya  ambazo ni Rabb nilinde ulioimwa na Mwanahawa Ally, Ukewenza sio dili,ulioimbwa na Mwanaidi Shabani na Stara ulioibwa na Sabaha Muchacho,

Ambapo siku hiyo wageni waalikwa ni Pr. Muhamed Elyas, Bi Shakirla ,Muhamed Issa Matona na wengine ambapo kiingilio 5000, ndani ya ukumbi wa Traventine Hotel iliyopo magomeni jijini Dar es salaam

Bendi hiyo imeakikisha kukonga nyoyo za mashabiki wao jukwaani kwa kuwa watakuwa wa kwanza kusikiliza nyimbo zao mpya wakiwa live jukwaani

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MAMA WA WATOTO WAWILI WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA WALIOLAZA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI NAIROBI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Aisha Omari (kushoto) Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao. Katikati ni Balozi wa Tanzania, nchini Kenya, Batrida Buriani. Picha na OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Aisha Omari, Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao.

NEY WA MITEGO ATUMA 'SALAMU ZAO’



Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ Anatarajia kuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Salamu zao’ hivi karibuni.

 Ney wa Mitego ni kati ya msanii ambaye anafanya vizuri katika soko hilo, na pia anasema ameamua kufanya kazi hiyo kwa lengo la kuburudisha na kuwaelimisha wapenzi wa kazi zake.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Ney wa Mitego alisema kazi hiyo anatarajia kuanza kuisambaza wiki ijayo ambapo kwa sasa anatarajia kuanza ‘kushuti’ picha mbalimbali kwa ajili ya video ya kazi hiyo.

“Wiki hii naanza kushuti katika sehemu mbalimbali, mashabiki wanatakiwa kuupokea vizuri wimbo huu kwani ni bonge la kazi, kama wanavyonijua mashabiki wangu sijawahi kufanya vibaya katika kazi zangu, naomba tu wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hiyo,” alisema Ney wa Mitego.


Msanii huyo ambaye kwasasa anatamba na kibao chake cha ‘Nasema nao’, aliwaomba mashabiki waipokee kazi hiyo kwani ina ujumbe mzito kwa jamii yote

PAULINE ZONGO AVUNJA UKIMYA



BAADA ya ukimya wa muda mrefu, mwimbaji nyota wa muziki wa kizazi kipya na  dansi, Pauline Zongo ameibuka upya na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Misukosuko ya mapenzi.

Pauline amerekodi kibao hicho na kundi jipya la muziki linalojulikana kwa jina la Ndege Watatu, linaloundwa na wanamuziki wengine wawili wa kike, Khadija Mnoga na Joan Matovolwa.

Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Pauline alisema tayari kibao hicho kimeshaanza kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini na kupokewa vizuri na mashabiki.

Mwanadada huyo, aliyekuwa mmoja wa wasanii wanaounda kundi la East Coast amesema, wameamua kuunda kundi hilo kwa lengo la kuleta changamoto mpya katika muziki.

Pauline alisema aliamua kuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu ya kulea mtoto wake wa pili mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu. Mtoto wake wa kwanza ana umri wa miaka sita.

Alisema ukimya wake huo pia ulilenga kusoma mwelekeo wa muziki na pia kujipanga upya kabla ya kurudi ulingoni akiwa na vitu tofauti.

Mwanamama huyo, ambaye ni mwajiriwa wa bendi ya TOT Plus alisema, wameamua kuliita kundi lao kwa jina la Ndege Watatu kwa sababu sauti zao zinafanana na wanakijua wanachokifanya.

Pauline alisema uamuzi wake wa kujiunga na TOT Plus ulilenga kukuza kipaji chake cha muziki na pia kuwaonyesha mashabiki kwamba ana uwezo mkubwa katika fani hiyo.

"Kusema kweli, huwezi kuwa mwanamuziki kama hujui kupiga ala yoyote ya muziki,"alisema mwanamama huyo, ambaye ana uwezo wa kupiga gita, drums na kinanda.

Licha ya kundi lake la TOT kumruhusu kuwa mwanamuziki huru, Pauline alisema hawezi kutoa albamu kila mwaka kwa vile akifanya hivyo, hawezi kupata manufaa makubwa.

Alisema mwanamuziki anatakiwa kusonga mbele akiwa na mabadiliko badala ya kufanya kitu kile kile kila mwaka.

Mwanamama huyo alisema hakujifunza muziki kutoka kwa mtu yoyote. Anasema kuna siku alilala akaota ndoto anapiga gita, drums, kinanda na kuimba na alipozinduka usingizini, akaamua kutimiza ndoto yake hiyo.

Pauline anakiri kuwa, asili yake ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Anasema mama ni Mcongo na baba yake ni Mtanzania.

"Mimi nilizaliwa Congo. Wakati huo baba alikuwa akija Congo kibiashara ndipo akakutana na mama na kwetu tupo watoto wengi tu. Baadaye ikatokea kutokuelewana kati ya baba na mama, hivyo mimi na mdogo zangu tukaja Tanzania na baba na ndugu zangu wengine walibaki na mama Congo,"alisema.

Pauline anasema pia kuwa ni kweli kwamba anaye pacha wake wa kiume anayeitwa Paul Zongo, ambaye kwa sasa ni prodyuza wa muziki nchini Afrika Kusini. Alisema Paul ameshiriki kutengeneza nyimbo za kundi la Malaika la Afrika Kusini na wanamuziki wengine wa nchi hiyo.

Alipoulizwa iwapo ni kweli amezaa mtoto wake wa pili na mwigizaji filamu nyota wa Bongo, anayejulikana kwa jina la Mtunisi, alikiri kwamba ni kweli.

"Ndio ni kweli, lakini kwa sasa tumeshaachana, kila mtu ana maisha yake. Nina mchumba wangu, ambaye Mungu akitujalia, mwishoni mwa mwaka huu tutafunga pingu za maisha. Tumeshakaa kwenye uchumba kwa miaka miwili sasa.Mchumba wangu naye ni pacha kama mimi, tunapendana sana,"alisema.

Je, ni kitu kipi ambacho Pauline anakijutia katika maisha yake?

"Kiukweli sitaki kuficha, uhusiano nilioingia na baba mtoto wangu naujutia sana. Laiti ningesikiliza ushauri wa watu wengi, yasingenikuta yaliyonikuta,"alisema.

"Nilikuwa sisikilizi yote niliyokuwa naambiwa juu ya tabia za mwanaume huyo, lakini baada ya kuyaona, niliishia kujuta maana mapenzi yake yalinipotezea hata mwelekeo wa maisha yangu. Lakini kwa sasa nina nguvu mpya na nipo huru, nimejifunza siku nyingine sitafanya makosa,"alisisitiza.

Pauline alianzia muziki akiwa na kundi la East Coast lililokuwa na wasanii mahiri kama vile Crazy GK, Khamis Mwinjuma 'Mwana FA' na Ambwene Yesaya 'AY' kabla ya kuhamia TOT.

Akiwa East Coast, alijipatia umaarufu mkubwa aliposhiriki kuimba kibao cha Sister Sister akishirikiana na Crazy GK wakati akiwa TOT, aling'ara kupitia kibao cha Mnyonge Mnyongeni, alichokiimba kwa kushirikiana na Badi Bakule na Abdul Misambano.

DIMPOZ AISAMBAZA 'TUPOGO’


Na Elizabeth John

BAADA ya kushindwa kuitambulisha mara kadhaa ngoma yake mpya inayofahamika kwa jina la ‘Topogo’, mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ameisambaza ngoma hiyo katika vituo mbalimbali vya redio.

Dimpoz amehairisha utambulisho wa ngoma hiyo zaidi ya mara moja ambapo mara ya mwisho alitakiwa kuitambulisha katika ukumbi wa Kimataifa Club Bilicanas, Juni 30 kabla hajausambaza wiki iliyopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ommy Dimpoz alisema ameamua kuusambaza wimbo huo bila kuutambulisha kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake na anawaomba wapenzi wa kazi zake waupokee wimbo huo kwa mikoni miwili.

Alisema katika wimbo huo, kamshirikisha nyota kutoka Nigeria, J Martin na kwamba anaamini kutakuwa na changamoto nyingi kwa wasanii wa bongo kutokana na uwepo wa mkali huyo.

 “Kiukweli J Martin ni msanii mkubwa na ana uwezo wa kulitawala jukwaa anapokuwa kazini; naamini nitafanya vizuri zaidi, ndiyo maana nimeamua kushirikiana naye, cha muhimu ni sapoti katika kazi zangu,” alisema Dimpoz.

Licha ya kutoka na nyota huyo, Dimpoz kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Me and You’ alichomshirikisha chipukizi wa muziki huo, Vanesa Mdee, mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vimefanya vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.

Juma Kaseja kutua Lupopo FC -DRC


Mlinda mlango wa Taifa Stars Juma Kaseja
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Juma Kaseja amesema kwamba amefanya mazungumzo tu na wakala wa klabu ya St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini bado hajaingia Mkataba na klabu hiyo ya Lubumbashi.

Akizungumza jana mchana, Kaseja amesema kwamba mtu aliyejitambulisha kwake kama wakala wa Lupopo alimfuata wakafanya mazungumzo na kufikia makubalino juu ya dau la usajili, mshahara na mambo mengine ya msingi.

Hata hivyo, kipa huyo namba moja Tanzania amesema kwamba baada ya mazungumzo hayo na maafikiano, wakala huyo amepeleka majibu Lupopo ambao wakiafiki ndipo masuala ya Mkataba yatafuatia.

“Nimezisikia hizo habari, kwamba mimi tayari ni mchezaji wa Lupopo, hapana, si kweli. Ni kwamba tumefanya mazungumzo tu na wakala wao na tumefikia makubaliano, nasubiri hadi nisaini Mkataba ndipo nitajihesabu tayari ni mchezaji wa Lupopo,”alisema Kaseja.

Baada ya kuitumikia Simba SC tangu mwaka 2003, Kaseja hakuongezewa Mkataba klabu hiyo mwishoni mwa msimu naye ameamua kwenda kuanza maisha mapya sehemu nyingine.

Pamoja na Simba SC kutomuongezea Mkataba Kaseja, ameendelea kuwa kipa chaguo la kwanza timu ya taifa mbele ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen.

Iwapo Kaseja atafanikiwa kuingia Mkataba na Lupopo atakwenda kuwa mpinzani mkuu wa wachezaji wenzake wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea Tout Puissant Mazembe ya Lubumbashi.

Kaseja alicheza pamoja na Samatta na kiungo Mganda wa Mazembe, Patrick Ochan katika klabu ya Simba mwaka 2010 kabla ya 2011 wachezaji hao kuuzwa DRC. 

NAPE AFUTURU NA MABALOZI WA NYUMBA KUMI LEO KIGOMA MJINI


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akifuturu pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk.Amani Kaborou,Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma Mohamed Nyawenga na Mbunge wa Manyovu Albert Obama.
 Baadhi ya Mabalozi wa nyumba kumi na wakazi wa Kigoma mjini wakifuturu leo 31Julai 2013 katika ofisi za CCM wilaya ya Kigoma Mjini.
 Baadhi ya Mabalozi na wakazi wa Kigoma mjini wakipata futari
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache baada ya kufuturu na Mabalozi wa nyumba 10 ambapo alisisitiza Watanzania kutunza amani waliokuwa nayo.
 Sheikh Mustafa Halfan Kiumbe akisema maneno machache kabla ya kumkaribisha Sheikh Mkuu wa Kigoma.
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi akishiriki dua iliyoongozwa na Sheikh Hassan Idd Kiburwa leo baada ya kufuturu na mabalozi wa nyumba 10 wa Kigoma mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya mabalozi wa nyumba 10 kutoka Kigoma mjini ambao alifuturu nao pamoja.
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji kutoka wilaya ya Kigoma mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufturu .

MTEMVU AGAWA MISAADA YA VYAKULA KWA VITUO VYA YATIMA TEMEKE


 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akiwakabidhi msaada wa vyakula watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Dar Alqaama Tandika katika sherehe ya kutoa misaa kwa vikundi mbalimbali vya yatima, Dar es Salaam hivi karibuni.
                                        Akiwakabidhi watoto wa Kituo cha Hiyari Chang'ombe
                                              Upendo Maganga wakipata msaada huo
                                                                  Upendo Bokolani wakipata msaada huo
                                        Kituo cha WAVIBA KILAKALA wakipokea msaada
                                               Kituo cha Faraja kikipokea msaada huo
 Mwenye ulemavu wa viungo, Zamda akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Mtemvu
                                                  Aisha Shabani akipokea msaada huo
                                        Mwasiti Mtebwa akipata msaada
 Mama Mwandoro akipata msaada
                                                           Ashura Sadiki


CCM YAIPONGEZA SERIKALI KURUDISHA NYUMA SUALA LA WANANCHI KULIPIA KODI LAINI ZA SIMU


NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza serikali, kwa uamuzi wake kurejesha bungeni kwa ajili ya mdajala zaidi, muswada wa sheria ulioanzisha kodi mpya ya tozo ya sh. 1,000 kwa laini ya simu.

Taarifa ya CCM iliyotolewa leo mjini Dodoma, na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye imesema uamuzi huo umedhihirisha kwamba serikali inawasikiliza na kuwajali wananchi wake.

Akiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari leo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amekaririwa akisema kwamba mjadala kuhusu muswada wa sheria ya kodi hiyo ya tozo hiyo utafanyika wakati wa mkutano wa Bunge unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Baada ya kupitishwa na bunge Juni mwaka huu, na utekelezwaji wake kuanza rasmi Julai mwaka huu, CCM ilikuwa miongoni mwa wadau waliopinga vikali kuanzishwa kwa kodi ya tozo hiyo, ikieleza kwamba ni mzigo na usumbufu usio wa lazima kwa watumiaji wa simu ambao wengi matumizi yao ni ya kawaida.

Katika taarifa hiyo, CCM imesema kwa kuwa wabunge wengi ni wa chama hicho, watumie fursa hiyo kuhakikisha sheria ya tozo hiyo inaondolewa na wakati huohuo watumie uwezo wao wote kuhakikisha wanaishauri serikali vizuri kupata njia mbadala itakayotumika kuziba nafasi itakayokuwa imeachwa kwa kuondolewa tozo hiyo.

"Kimsingi hatua hii imetupa faraja na hivyo CCM inaipongeza Serikali kwa kuamua kusitisha sheria ya kodi ya tozo hiyo ya sh. 1,000 kwa laini ya simu kwa kuwa ingesababisha usumbufu na adha isiyo ya lazima kwa wananchi", imesema CCM katika sehemu ya taarifa yake.

MTANZANIA KWENDA SAUZI SIKU HIZI TEGEMEA KUSACHIWA SANA



Kwenye Exclusive interview na millardayo , Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana (Akina Masogange )  waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.


Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.



Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.



Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.



Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.



Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.

MISS ILALA WAANZA KUJINOA KWA FAINALI



JUMLA ya warembo 15 kutoka katika vitongoji vinne vya wilaya ya Ilala, wameanza mazoezi ya kujiandaa na kumsaka mrembo wa wilaya ya Ilala ‘Redd’s Miss Ilala 2013’ yanayofanyika katika ukumbi wa klabu Billicanas uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower tarehe 16 Agosti mwaka huu, kati ya hao warembo watatu ndio wanaowania nafasi ya kushiriki shindano la Redds Miss Tanzania, shindano linalotarajia kufanyika baadae mwezi Septemba.

Warembo hao ambao wanatoka katika vitongoji vya Mzizima, Tabata, Ukonga na Dar City Centre wamekuwa wakijifua na kufanya onesho hilo kuwa la kuvutia zaidi, tofauti na miaka iliyopita.

Maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na wamepania kuonesha vipaji vyao kwa kufanya shindano la kuoesha vipaji ambalo linatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Sisi kama kamati tunaowaomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia muonekano mpya wa mashindano ya urembo, lakini pia kuangalia jinsi Ilala ilivyosheheni warembo watakaoleta ushindani mkubwa Redds Miss Tanzania 2013.

Warembo waliopo katika kambi ya Miss Ilala ni pamoja na Alice Isaac, Clara Poul,Anna Johnson,Iren Mwelolo, Munira Mabrouk,Rehema Mpanda, Shamim Mohamed, Martha Gewe, Diana Joackim, Natasha Mohamed, Dorice Mollel, Pendo Lema, Kazumbe Mussa na Kabula Kibogoti.

Hadi sasa kampuni zilizojitokeza kudhamini ni Redd’s, Dodoma wine,CXC Tours,Chilly Will,Tanzania Daima,Jambo Leo,Clouds FM,Tanzania Daima,City Lounge na Times FM. 

WATOTO KUMENYANA TOTO PARTY IDD MOSI


Kampuni ya Glitz Entertainment imeandaa Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake linayotarajiwa kufanyika katika Art Gallery iliyopo Mbezi Beach siku ya Iddi Mosi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, Deniss Ssebo alisema kuwa hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto, na wanatarajia kuanza kulipeleka na mikoani.

Katika Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.

Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.
Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...