Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 1, 2013

DIMPOZ AISAMBAZA 'TUPOGO’


Na Elizabeth John

BAADA ya kushindwa kuitambulisha mara kadhaa ngoma yake mpya inayofahamika kwa jina la ‘Topogo’, mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ameisambaza ngoma hiyo katika vituo mbalimbali vya redio.

Dimpoz amehairisha utambulisho wa ngoma hiyo zaidi ya mara moja ambapo mara ya mwisho alitakiwa kuitambulisha katika ukumbi wa Kimataifa Club Bilicanas, Juni 30 kabla hajausambaza wiki iliyopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ommy Dimpoz alisema ameamua kuusambaza wimbo huo bila kuutambulisha kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake na anawaomba wapenzi wa kazi zake waupokee wimbo huo kwa mikoni miwili.

Alisema katika wimbo huo, kamshirikisha nyota kutoka Nigeria, J Martin na kwamba anaamini kutakuwa na changamoto nyingi kwa wasanii wa bongo kutokana na uwepo wa mkali huyo.

 “Kiukweli J Martin ni msanii mkubwa na ana uwezo wa kulitawala jukwaa anapokuwa kazini; naamini nitafanya vizuri zaidi, ndiyo maana nimeamua kushirikiana naye, cha muhimu ni sapoti katika kazi zangu,” alisema Dimpoz.

Licha ya kutoka na nyota huyo, Dimpoz kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Me and You’ alichomshirikisha chipukizi wa muziki huo, Vanesa Mdee, mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vimefanya vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...