Mghani mahiri wa mashairi hapa
nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo,masuala ya fursa
mbalimbali zinazopatikana katika suala zima la ujasiliamali mapema leo
kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa Student's
Center,uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo
iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la
NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Baadhi ya Wasanii wa muziki wa
kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo
kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora
mapema leo,kutoka kulia ni Msanii Godzilla,Baba Levo,Amin,Stamina na
wengineo.
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa
kampuni ya mafuta-Lake Oil,Bwa.Ben Temu akizungumza kwenye semina ya
Fursa,ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali ikiwemo suala la vijana
kuwa wenye moyo wa kujituma na kutokata tamaa,alieleza kwa kuwataka
vijana wawe wavumilivu na kutoka tamaa kwa kila fursa wanayokumbana
nayo,badala yake waitumie vizuri katika suala zima la kujikwamua na
kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Semina ya Fursa ikiendelea mapema leo ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Msanii wa Muziki wa Kizazi
Kipya,Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya fursa alizozipata mara baada
ya kujiunga na shirika la NSSF,mbele ya Washiriki wa Semina ya Fursa
(hawapo pichani),kulia kwake ni Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim
Khalfan akimsikiliza kwa makini.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Mwakilishi wa Shiriki la NSSF
kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan akielezea fursa
mbalimbali zinazopatika mara mtu yeyote anayejiunga ama amejiunga na
NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyeote atakayejiunga na shirika hilo
atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo na mengineyo
lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Baadhi ya Wakazi wa Tabora
wakifuatilia kwa makini semina ya ujasiliamali iliyokuwa ikiendelea
ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema
leo
Picha ya pamoja,kiukumbusho zaidi,Msanii Mrisho Mpoto akiwa amepozi na Diamond
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi
kipya,Diamond,akiwaimbisha washiriki wa semina ya Fursa waliojitokeza
kwa wingi mapema leo kwenye ukumbi wa Student's Center uliopo katikati
ya mji wa mkoa wa Tabora,kushoto kwake ni Bwa.Marco Vingila kutoka
shirika la TPSF. .
No comments:
Post a Comment